25 May 2012

Shule zilizozofanya vizuri Dar 'tiba' ya kuacha kusomesha nje


 Na Reuben Kagaruki

MWAMKO wa wazazi kutambua umuhimu wa elimu unazidi kuongezeka nchini, ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Umuhimu wa elimu kwa watoto umechangia uwekezaji katika sekta hiyo kuongezeka kwa kasi ya aina yake. Jambo hili ni kati ya mambo ya kujivunia.

Watu binafsi, mashirika ya dini na wadau wengine wameonesha wazi kusaidia juhudi za Serikali za kuinua elimu nchini. Kinachotia moyo zaidi wazazi wengi kuhitaji watoto wao wapate elimu bora si bora elimu.

Kwa kufahamu hilo, wazazi wamekuwa wakihaha kutafuta shule bora za kusomesha watoto wao hasa zile zitakazokidhi matakwa wanayohitaji. Mfano, miaka ya nyuma kulikuwa na kasi kubwa ya wazazi kupeleka watoto wao kusoma nje ya nchi.

Mfano mzuri ni kwenye nchi za Uganda na Kenya. Kasi hiyo inazidi kupungua baada ya shule zinazoanzishwa nchini kukidhi viwango ambavyo wazazi wengi wanahitaji. Katika eneo hili tunastahili kuipongeza Serikali kwa kufungua milango ili watu wawekeza katika sekta hiyo.

Kuanzishwa kwa shule hizo pia kumesaidia kuwapunguzia wazazi gharama, kwani awali walikuwa wakitumia fedha nyingi kwenda kusomesha watoto nje ya nchi.

Kinachodhihirisha kuwa shule zenye ubora zipo nchini ni matokeo ya mitihani yaliyotangazwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mkoa wa  wa Dar es Salaam  ulitangaza shule 10 bora zilizofanya vizuri zaidi katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2011, ambapo Tusiime iliyopo Tabata iliongoza kimkoa.

Katika matokeo hayo rasmi ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam shule hiyo ilikuwa ya kwanza baada ya kufaulisha wanafunzi wake wote 139 waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka jana.

Matokeo hayo rasmi yanaonesha shule zilizofuatia kimkoa ni St Joseph,
Montfort, Masaka, Filbert Bayi, Azanaki, Mountain Hill,  Hollycross,
Moga na Canossa. Matokeo hayo yalitangazwa rasmi wakati wa mkutano kati ya Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Benard Makali na Maofisa Elimu na walimu wakuu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Bw. Makali anasema matokeo rasmi yanaonesha kuwa shule ya Tusiime iliyopo Tabata ndiyo imekuwa ya kwanza kimkoa kwa  kufaulisha
wanafunzi wote wa shule ya msingi kwenye mitihani ya kumaliza darasa
la saba mwaka 2011.

Katika matokeo ya Wilaya ya Ilala Tusiime pia imekuwa ya kwanza
ikifuatiwa na shule za St Joseph, St Theresoflisieux, African, Agens
Michael, Mkoani, Boma, Christ The King, Al Madrasa-Tus Asaifiya na New Ambasador.

Akifafanua kuhusu taarifa ambazo zimekuwa zikiwachanganya Watanzania
kuhusu baadhi ya shule jijini Dar es Salaam kujitangaza kwamba
zimekuwa za kwanza kiwilaya na kimkoa wakati sio kweli, anasema; "Nitazichunguza shule hizo na kuchukua hatua."

Bw. Makali alionesha kuchukizwa na tabia ya shule hizo na aliahidi
kufuatilia taarifa hizo na itakapobainika kwamba ni kweli, hatua kali
zitachukuliwa kwa shule husika ili iwe fundisho.

“Mimi sitambui matokeo mengine zaidi ya haya yanayoonesha kuwa
Tusiime ndiyo imeongoza kimkoa na kiwilaya, hao wanaojitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wamekuwa wa kwanza hayo matokeo wameyatoa wapi? Huu ni uongo wa hali ya juu na itabidi nifanyie kazi tabia hii ili Watanzania wasiendelee kupotoshwa,” alisema.

Katika matokeo rasmi ya Wilaya ya Kinondoni shule 10 bora
ni Filbert Bayi ambayo ndiyo imekuwa ya kwanza ikifuatiwa na Drive Inn, Ali Hassan Mwinyi Elite, Sunray, Msisiri ‘B’, Sunrise, Sahara,
Mirambo, Bethel Mission na Anininduni.

Temeke shule ya kwanza ni Montfort, Hollycross, Al-Hikma,
Fraylouisamigo, Shalom, Chang’ombe, Minazini, St Marys International,
Kurasini na Mivinjeni.

Kutokana na kufanya vizuri zaidi, Manispaa ya Ilala jijini Dar es
Salaam, iliiipa tuzo maalum shule ya Tusiime kwa kufanikiwa kufaulisha wanafunzi.

Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni na manispaa hiyo kwa mkuu wa shule
hiyo, kama ishara ya kutambua mchango wa shule hiyo katika kukuza elimu nchini.

Bw. Makali, alisema shule ya Tusiime inastahili kupewa tuzo hiyo maalum kutokana na kufaulisha wanafunzi wote na kwa kuwa ya kwanza kimkoa miaka miwili mfululizo.

“Wamekuwa wa kwanza kimkoa kwa miaka miwili mfululizo na tuzo
waliyopata ni kutokana na kufaulisha wanafunzi wote kwa asilimia 100,
haya ni mafanikio makubwa kielimu nawapongeza,” alisema.

Mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Bw. Philibert Simon, anasema wanafunzi 19 walichaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum.

Alitaja baadhi ya shule za vipaji maalum walizochaguliwa wanafunzi hao kujiunga nazo kuwa ni Ilboru, Kibaha, Tabora Boys, Mzumbe, Ifunda Ufundi na Iyunga Ufundi.

Aliongeza kuwa si mara ya kwanza kwa shule hiyo kupewa tuzo ya aina hiyo, kwani Julai 2010 ilipewa tuzo ya aina hiyo na manispaa hiyo hiyo kwa kufaulisha wanafunzi kwa daraja A mwaka 2009.

“Siri ya mafanikio ni uongozi wa shule kutoa  ushirikiano wa kutosha
kwa walimu, wazazi kwa upande wao wamekuwa wakitimiza wajibu wao na
haya ndiyo  yametufikisha hapa tulipo,” anasema.

Anasema mazingira mazuri ya shule nayo yamekuwa na mchango mkubwa
katika kuhakikisha wanafunzi wanapata muda wa kutosha wa kusoma na
kushiriki michezo mbalimbali.

"Tunaamini kwamba matokeo haya hayakuja kwa bahati mbaya, bali
kumetokana na moyo wa kujituma kwa wanafunzi na walimu wao.
Kufaulisha wanafunzi wote si jambo la bahati kwani tumeshuhudia shule
nyingi zikifelisha nusu ya wanafunzi katika mitihani ya mwisho," anasema.

Hakuna shaka kwamba ufaulu huo mkubwa umetokana na jitihada za walimu
kufuatilia wanafunzi kuhakikisha wanafuata misingi ya masomo na
kujisomea ili waweze kufanya vyema.

Anasisitiza kuwa walimu wa shule zingine nao wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kufundisha kwa ari na moyo wa kujituma ili kuboresha elimu nchini.

Anaongeza kuwa pamoja na mazingira magumu ya baadhi ya walimu kwenye shule mbalimbali hasa za serikali wajitaidi kusahau ugumu huo na kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuinua kiwango cha taaluma.

Hata hivyo anakiri kuwa mazingira ya shule nayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha ufaulu kwa shule za binafsi na za Serikali
zinapaswa kuiga mfano huo.

Anasema vifaa vya kujifunzia kama maabara navyo vina nafsi yake, kwani mwanafunzi kujifunza bila vitendo haiwezi kumsaidia siku za usoni.

Mwanafunzi akiambiwa kuhusu kifaa sayansi ili aweze kukielewa
vyema ni muhimu zikawepo maabara za shule hiyo ili kuhakikisha
wanapata ufahamu wa hali ya juu.

7 comments:

  1. Naona hapo hamjawa makini kwa wilaya ya Kinondoni shule kumi zinazoongoza hazimo kwenye kumi bora za mkoa na kumi bora za mkoa hazipo kenye kumi bora za wilaya ya kinondoni. Nadhani waandishi mnahitaji kuwa makini zaidi. Na sidhani kama kuna shule inaitwa Azanaki ila kuna Zanaki au Anazaki. Check that!

    ReplyDelete
  2. mie sijui kama mwanafunzi aliye kwenye hizo shule au mwalimu wanaowafundisha wanatofautiana vipi katika shule zingine nchini???? labda niseme tu kuwa the way those teachers are being treated, inawapa moyo wa kufanya kazi with a willing heart.

    ReplyDelete
  3. HIYO TAKWIMU YENU MMEKOSEA KUNA MIKOA IMEINGIA 10 BORA LAKINI HATUIIONI! KAMA MKOA WA KAGERA MBONA HAIKO KWENYE ORODHA YENU?

    ReplyDelete
  4. 7, 8, HIZO NAFASI ZIMETOKA MKOA WA KAGERA KWAIYO HIZO SHULE ZIPO KWENYE 10 BORA!

    ReplyDelete
  5. kama kweli hao Tusiime ni washindi wa kwanza Mkoa wa Dar es Salaam, mbona kwenye interview za kujiunga na shule bora za form one walikuwa wanafanya vibaya hivyo. Siamini kuwa walitumia akili zao. There is something.

    ReplyDelete
  6. ndugu Anazak ipo huku kwetu Mbezi Temboni. hata google kwanza basi!

    ReplyDelete