30 May 2012

CHADEMA waishutumu CCM



Na Allan Ntana, Tabora

KATIBU Mwenezi wa CHADEMA Bw. Ali Mwakilima amewataka wananchi kutobweteka na ulaghai wa CCM pindi unapokuja uchaguzi kwa kuwahadaa kwa fulana, kofia na kanga.

Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kijiji cha Igunda Kata ya Ifucha, Manispaa ya Tabora ambako kulikuwa na
mkutano wa CHADEMA.


Bw. Mwakilima alisema inashangaza kuona wananchi wanafikia wanafikia hatua wanadanganyika na vitu hivyo na baada ya ghiliba hiyo wanatamka CCM imewalea.

”Mkitaka kujiridhisha na hilo kuwa watendaji na mabalozi nao hawaijui
Katiba...ni pale mtendaji anapohojiwa juu ya haki za msingi za raia na kuwa mkali. Hiyo ni kiashirio tosha kwamba nao Katiba ya nchi hawaijui,” aliongeza.

Aliwataka wananchi kuwa makini na michango isiyo ya lazima na kusema
kwamba michango inakuwa mingi, lakini huduma zinakuwa mbovu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA Bw. Saimon Lameck aliwaomba wananchi kwenye mkutano huo waichague CHADEMA kwani ni chama kitakachoweza kuleta mageuzi na huduma za kweli.

”Ukitaka kujua hali sasa ni tete na ngumu angalia kijana wa miaka 30 utadhani ana umri wa miaka 70, hiyo ni kutokana na gharama za maisha kupanda kila kukicha halafu ndugu zangu mnajitapa kuwa CCM imewalea, badilikeni,”  alisema.

No comments:

Post a Comment