30 May 2012
Albino wana uwezo wa kufanya kazi zote'
Na David John, Aliyekuwa Mwanza
IMEELEZWA kuwa jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Albino wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa ili kuhaakisha maendeleo.
Hayo yalielezwa hivi karibuni mkoani Mwanza na Bi.Vicky Ntetema ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Same Sun hapa nchini, baada ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kujionea changamoto zinazowakabili watu hao.
Alisema, kuna haja kupinga mawazo ama fikra potofu ambazo zimejengeka katika vichwa vya Watanzania kwamba watu wenye ulemvu wa ngozi hawana uwezo wa kufanya kazi na kupelekea kunyimwa fursa katika maeneo mbalimbali wanayokwenda kuomba kazi.
"Kuna changamoto kubwa, kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuweza kukubalika katika jamii na hasa pindi wanapokwenda kuomba kazi katika maeneo tofauti ambapo wanakutana na vikwazo vingi hasa kuonekana kama hawana uwezo mbali na elimu waliyokuwa nayo," alisema.
Alisema, moja ya changamoto zinazowakabili walemavu wa ngozi ni kutokukubalika vema na kuonekana kama wao ni watu watofauti ambao hawawezi kufanya lolote katika jamii kitu ambacho kinawakosesha amani na kuonekana wanatengwa katika nchi yao.
Kwa upande wa elimu darasani alisema, walimu wanapaswa kuwa karibu na watu hao ikiwa pamoja na kuonesha upendo wa hali ya juu pia kuepuka kutoa adhabu ambayo inatokana na kufanya vibaya kwa mwanafunzi mlemavu darasani.
"Najua kuna taasisi nyingi hapa nchini na zinasaidia katika maeneo mengi, lakini binafsi naomba tujikite zaidi katika kuwasaidia watu hawa," alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment