24 May 2012

Heineken yawapa burudani mashabiki UEFA



Na Mwandishi wetu

SHAMRASHAMRA  za kusherekea ubingwa wa timu ya Chelsea katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya,zimeendelea kufana katika mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania,baada ya Heineken Champions Planet  kuwaandalia pati mashabiki wa timu hiyo.

Timu ya Chelsea ilitwaa ubingwa huo Jumamosi iliyopita baada ya kuilaza Bayern Munich ya Ujerumani katika mechi ya fainali ya michuano hiyo iliyopigwa mjini Munich nchini Ujerumani.

Katika mchezo huo mshambuliaji Didier Drogba ndiye aliyeibuka shujaa,baada ya kuisawazishia bao Chelsea dakika za majeruhi na kisha akakwamisha kimiani mkwaju wa mwisho wa  penalti  ulioifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa mabao 4-3

Kufuatia ushindi huo  ukumbi wa  Heineken Champions Planet uliopo  Masaki,jijini Dar  es Salaam ambao kwa kipindi chote cha  miezi mitatu tangu hatua ya makundi ambapo mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakishuhudia michuano hiyo katika ukumbi huo walipata fursa ya kujimwaya mwaya baada ya ushindi huo.

Sherehe hizo ziliwakutanisha mashabiki wapatao  250  wakiwemo watu mashuhuri wa burudani na serikalini ambao walishuhudia pambano hilo katika luninga ndogo ambayo ilionekana kama uwanja kabla ya kuoneshwa katika luninga kubwa.


"Kila mshiriki tangu Februari wamekuwa wakiingojea siku hii  kubwa , ni usiku wa usiku wa wageni wote  kwa ajili ya tukio hili ni mabingwa katika haki zao wenyewe na kuwa na muda mrefu wa kudumu kumbukumbu ya matukio yote  yaliyojitokeza kwa ajili ya usiku, "alisema mmoja wa mashabiki watimu hiyo  Heri Tungaraza.

Shamrashamra hizo ambazo zilianza tangu saa mbili usiku zilianza kwa kuoneshwa mechi zilizopita, na magoli  huku luninga ya Heineken TVC,ilikuwa ikionesha michezo hiyo kupitia luninga zote zilizomo katika jumba hilo huku wageni wakiburudishwa na muziki laini.

No comments:

Post a Comment