24 April 2012

Ufisadi wa kutisha waanikwa Maliasili

Na Benedict Kaguo, Dodoma


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, imeibua ufisadi mpya wa utoroshaji wanyama na ugawaji wa vitalu vya uwindaji unaodaiwa kufanywa na maofisa wa Wizara wa Maliasili na Utalii, kinyume na sheria.

JK aungana na vingozi wakuu kumzika Mutharika


Na Eckland Mwaffisi, Blantyre, Malawi

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliungana na viongozi mbalimbali wa Afrika na Jumuiya za Ulaya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Profesa Bingu wa Mutharika.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini hapa akiongozwa na Rais wa nchi hiyo, Bi. Joyce Banda.

Iran yatengeneza ndege kama ya Marekani

TEHRAN,Iran

SERIKALI ya  Iran imedai kwamba imepata maelezo ya undani kutoka ile ndege ya Kimarekani isiyokuwa na rubani ambayo ilianguka mwaka jana.

Kati ya  mambo ambayo Iran iliyagundua kutoka ndege hiyo ni kwamba ilitumiwa kumpeleleza,Bw. Osama Bin Laden wiki kadhaa kabla ya kuuawa.

Rais Sarkorzy ashindwa duru ya kwanza ya uchaguzi

PARIS,Ufaransa

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa,Bw. Francois Hollande, ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi nchini humo.

Huku idadi ya kura nyingi zikiwa zimehesabiwa Bw Hollande tayari amepata asilimia 28 ya kura akifuatiwa na Rais wa nchi hiyo, Bw. Nicolas Sarkozy anafuatia kwa a

Tenga: Ningekuwa mimi ningetoa adhabu kali Yanga

Na Zahoro Mlanzi

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kama angekuwa yeye ni kamati angetoa adhabu kali kwa wachezaji wa Yanga kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu walivyofanya wakati wa mechi yao dhidi ya Azam FC.

Yanga SC yamng'ang'ania Papic

Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kostadin Papic bado ni kocha wao halali kwa kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Jana Papic alikaririwa na vyombo vya habari akidai kwamba leo ndiyo mwisho wa mkataba wake wa kuinoa timu hiyo, ambapo pia aliwaaga mashabiki wa timu hiyo, mara baada ya timu yake na Polisi Dodoma kucheza katika mechi waliyoshinda mabao 3-1.

Simba yaendeleza wimbi la ushindi

:: Mechi ya Azam, Mtibwa Utata
Na Elizabeth Mayemba

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Simba jana waliendeleza kimbunga cha ushindi baada kuishindia Moro United mabao 3-0 katika ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Simba ambao wana pointi 59 wakifuatiwa na Azam sasa wanahitaji pointi ili waweze kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara.

Maskini Lulu, amwaga chozi mahakamani

Na Rehema Mohamed
MSANII maarufu wa filamu nchini Elizabert Michael 'Lulu' jana alimwaga chozi Mahakamani wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msanii huyo alimwaga chozi hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na msukumano kati ya askali magereza na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwa wakitaka kumpiga picha.

17 April 2012

Millya ahamia CHADEMA

*Adai CCM ni gari yenye pancha lukuki
*Nape: Alikuwa mzigo ndani ya chama
*Shigela: Amejivua gamba, bado wengine
                            
                  Bw.James Ole Millya
Na Pamela Mollel, Arusha
HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoani Arusha, Bw. James Ole Mallya, kutangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

CHADEMA wajitoa uchaguzi EALA

  • Wadaia mchakato huo umetawaliwa na rushwa
  • Wabunge wake wapinga marekebisho sheria

Nauli za daladala Dar kupanda tena, maombi 'yatinga' SUMATRA

Na Heri Shaaban
CHAMA cha Wamiliki wa Daladala MKoa wa Dar es SAlaam (DACOBOA)wamepeleka maombi yao Mamlaka ya Udhibiti Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa ajili ya kuongeza bei mpya ya nauli za daladala.

Uamuzi wa serikali kuipa meno SSRA wapongezwa

Na Rose Itono
BAADHI ya wadau wa masuala ya Hifadhi ya Jamii nchini, wameipongeza Serikali kwa kupitisha muswada wa marekebisho ya sheria za mifuko ili kuiwezesha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), kufanya kazi zake ipasavyo.

Wabunge CHADEMA tumieni busara, ushiriki wenu EALA ni muhimu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kilitangaza kujitoa katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambao unafanyika leo.

KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia), akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi, baada ya kuwasili katika Hoteli ya Tivoli, jijini Sao Paulo, nchini Brazil juzi tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kushoto kwake ni mkewe Mama Salma Kikwete. Picha na IKulu

Serikali ifanye kazi kwa uwazi

Na Pendo Mtibuche, Dodoma
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Samuel Sitta, amesema umefika wakati wa Serikali kufanya kazi kwa uwazi  katika mambo mbalimbali.

Dkt. Bilal atoa changamoto kwa Watanzania

Na Pamela Mollel, Arusha
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Ta n z a n i a Dkt. Mohamed Gharib Bilal amewataka wananchi, wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara jijini Arusha kutumia huduma za Benki ya ABC ili kuboresha maisha yao.

Wakulima wadogo wadogo kutoa tamko leo

Na Lilian Justice, Morogoro
MTANDAO wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania (MVIWATA) umeandaa kongamano la kitaifa ambalo pamoja na mambo mengine litajadili na kutoa tamko la kupinga mauaji ya wakulima wadogo nchini hasa wanaouawa katika harakati za kutetea ardhi yao.

Udanganyifu udahili wanafunzi wapata mwarobaini

TANZANIA ni moja ya nchi inayofanya kila jitihada kuinua kiwango cha elimu ili kuleta maendeleo lakini
pia serikali imeweka mkakati wa kuona kila Mtanzania anakuwa na elimu angalau ya kidato cha nne.

Operesheni ya kuzuia kelele za mabaa iendelee

NINAPENDA kumpongeza S u l e i m a n K o v a ,kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova kwa operesheni ya kuzisaka na kuzifunga kumbi zinazopiga kelele usiku na hata mchana iliyoendeshwa mwishoni mwa mwaka jana hapa jijini. (Majira, Oktoba 6, 2011).

Muleba wapitisha bajeti bilioni 41.1/-

BAADA ya majadiliano ya siku mbili ya bajeti ya halmashauri hatimaye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera limepitisha bajeti hiyo ya mwaka 2012/13 ambayo inakadiriwa kufikia zaidi ya sh. bilioni 41.1 zitakazokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali.

Bayern Munich uso kwa uso na Real Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (katikati) akizunguka uwanja na wachezaji wenzake katika mazoezi yaliyofanyika jana kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, dhidi ya Bayern Munich itakayofanyika leo katika Uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani. (AFP)

16 April 2012

Arumeru kwachafuka

*Kauli za wagombea zachochea uvamizi wa shamba
*Wananchi waharibu mali, nyumba za wawekezaji
*Wadai kuambiwa mashamba hayo ni mali yao

IBADA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein (kulia), akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Benjamin Mkapa, wakati wa ibada  maalumu ya kuwekwa wakfu Askofu Michael Henry Hafidh wa Dayosisi ya Zanzibar jana. (Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)

Wakalimani lugha ya alama waadimika

Na Joseph Mwambije, Songea 
MKOA wa Ruvuma unakabiliwa na uhaba wa wakalimani wa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia 'viziwi' ambapo kati ya wakalimani watano waliopo, wawili kati yao ndiyo wamesajiliwa na Chama cha Wakalimani wa Lugha za Alama (CHAWALATA).

CHADEMA wakosoa utendaji wa polisi

*Wadai wakitumika kisiasa, amani iliyopo itapotea
Na Suleiman Abeid, Shinyanga

UCHAGUZI CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Bw. Gishuli Charles, ambaye  sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga juzi, wakati akitoa nasaha kwa wana CCM kutumia kura zao kuchagua viongozi waadilifu wakati wa uchaguzi wa chama hicho. (Picha na Suleiman Abeid)

Balozi Mwapachu awapa somo vijana

Na Willbroad Mathias
ALIEKUWA Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu, amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya sekta mbalimbali nchini na kuwataka waache dhana ya kujiona wao ni viongozi wa kesho.

Matumizi ya ardhi yashirikishe jamii

MIGOGORO ya ardhi imeendelea kuzikumba jamii nyingi katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kusababisha migogoro.

Shule za msingi, sekondari zakabiliwa tatizo la mimba

Na Pendo Mtibuche, Dodoma
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma, bado inakabiliwa na tatizo la mimba katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.

Wateja wa M-Pesa kupata punguzo la kutoa fedha

Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu (katikati), akionesha nambari ya Mshindi wa Droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Bw. Revocatus Mkama, alishinda na kupata sh. milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid na Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma. (Na Mpigapicha Wetu)
Na Mwandishi Wetu,

Mdee, Bulaya wataka kumtoa Lulu gerezani

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kawe Bi. Halima Mdee (CHADEMA) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Bi. Ester Bulaya (CCM) wameamua kujitokeza kumsaidia msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa mwigizaji marehemu Steven Kanumba.

Tutalinda uhuru wa dini zote-Dkt. Shein

Na Mwandishi Maalum,
Ikulu Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kulinda uhuru wa dini zote lakini haitavumilia vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa jina la dini huku ikisisitiza uadilifu kwa viongozi wa dini.

Serikali yasimamisha uchimbaji madini

Na Pamela Mollel, Manyara
 SHUGHULI za uchimbaji wa madini katika Kitalu D eneo la Mererani wilayani S ima n j i r o Mk o a wa
Manyara umesimamishwa kwa muda na Ofisi ya Madini Kanda ya Kaskazini baada ya kuibuka kutoelewana kwa wamiliki wa mgodi huo.

SOKA

Kiungo wa Manchester United, Michael Carrick (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyochezwa jana Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester. (AFP)

Simba yaendelea kujikita kileleni

Na Elizabeth Mayemba
VINARA wa Ligi Kuu Simba, jana waliendeleza ubabe katika mechi za ligi hiyo baada ya kuinyuka Maafande wa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

12 April 2012

'Lulu' yamkuta

*Apandishwa kortini Kisutu chini ya ulinzi mkali
*Asomewa shtaka la mauaji, arudishwa lumande 
*Mama yake Kanumba azungumza ya moyoni
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Dhana ya kujitegemea itachochea maendeleo

WAKATI Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere anajenga misingi ya Taifa hili baada ya uhuru, alitangaza siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Ulinzi shirikishi mwarobaini wa uhalifu

KUTOKANA na vitendo vya wananchi wengi kuwachukia askari polisi, wamekuwa mstari wa mbele
kuwalinda . Wamekuwa msaada na kuthubutu kuwaita wakombozi kutokana na ujasiri wao wa kulinda mali za watu, kuzuia ujambazi, kukabiliana na vibaka pamoja na kuwazuia wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Bajeti finyu yaikosesha raha Wizara ya Elimu

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema ufinyu wa bajeti unawafanya washindwe kuwatumia walimu kutoka kisiwani Pemba na maeneo ya mbali kusahihisha mitihani.

Nani wa kumnusuru mkulima wa pamba Shinyanga-2

KAMA tulivyoona katika toleo lililopita kwamba zao la pamba ni moja ya mazao makuu ya kibiashara hapa nchini ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa, lakini hata hivyo wakulima wa zao hilo wamekuwa wakilalamika kutosaidiwa na mamlaka zilizokabidhiwa jukumu hilo.

UDONGO

Mfanyabiashara wa Soko la Buguruni Bw.Salum Mohamed, akipanga udongo 'maarufu Kigoma'  katika soko hilo, Dar es Salaam jana, baadhi ya watu hatafuna udongo huo ambao huuzwa Sh. 25, kwa kipande. (Picha na Peter Twite)

Wajane, yatima kupewa ruzuku

Na Livinus Feruzi, Kagera
SHIRIKA la Kuwezesha Watoto Yatima na Wajane katika Manispaa ya Bukoba la Matumaini Mapya linatarajia kutoa ruzuku ya zaidi ya sh. milioni 48.4 kwa wanawake wajane na walezi wa watoto yatima 200 lengo likiwa ni kuwapunguzia ugumu wa maisha unaowakabili.

CHADEMA waweka mkazo Serikali za majimbo

Na Raphael Okello, Bunda
CHAMA cha Demokrasia na Mae n d e l e o (CHADEMA) kimesisitiza kuwepo kwa serikali ya majimbo ambapo kimewaomba wananchi kuzingatia suala hilo watakapotoa maoni wakati wa mchakato wa uandikaji wa Katiba Mpya.

Mpiga drum wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta', James kibosho akifanya vitu vyake katika onesho la bendi hiyo lililofanyika juzi, Dar es Salaam. (Picha na Victor Mkumbo)

Yanga waenda Kanda ya Ziwa

*Sendeu alalamikia ratiba ya ligi
Na Elizabeth Mayemba

11 April 2012

Maskini Lulu, ombi lake latupwa

                                     Elizabeth Michael
Na Suleiman Mbuguni
MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' jana ameshindwa kutoa salamu za mwisho kwa msanii mwenzake katika tasnia hiyo, Steven Kanumba ambaye anadaiwa kabla ya kifo chake walikuwa pamoja nyumbani kwa marehemu Sinza Vatcan jijini Dar es Salaam.

05 April 2012

Mukama ang'aka


 *Awashukia wanaotakiwa kujivua gamba
*Adai wanatumika kumuhusisha na ufisadi
*Asema ndani ya CCM wote si Richmond


 Katibu Mkuu wa CCM Bw.Wilson Mukama.

Hukumu ya Lema kutikisa Arusha leo

*Polisi kuimarisha ulinzi maeneo mengi
Na Waandishi Wetu, Arusha

MLIPUKO FELI

Askari wa kikosi cha zimamoto na Uokoaji cha Halimashauri ya Jiji la Dar es salaam wakipambana kuzima moto uliolipuka na kuteketeza majiko ya soko la Samaki la kimataifa la feli jana chanzo cha moto huo ni mlipuko wa mafuta katika moja ya majiko ya kukaangia samaki.(Picha na Rajabu Mhamila)

Mzimu wa Arumeru wamgeukia Mrema

Na Bahati Mohamed
WANACHAMA wa Chama cha Tanzanian Labour Party (TLP), wamempa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Bw. Augustino Mrema muda wa siku 40 awe amejiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kuchangia chama hicho kishindwe katika uchaguzi wa mdogo wa ubunge Jimbo Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.

Utamaduni wa kutoa rushwa sasa tuukatae

TATIZO la rushwa nchini lipo katika sekta mbalimbali lakini hali hiyo haina maana kuwa inakubalika katika jamii.

Wakulima washauriwa kuongeza thamani ya korosho

Na Godwin Msalichuma, Kilwa
WAKULIMA wa korosho wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, wamekitaka chama
kikuu cha ushirika mkoani humo, Ilulu kutenga korosho kwa ajili ya
kubangulia  ili kuziongezea thamani ya zao hilo na zingine kuzitafutia soko nje ya nchi.

Majambazi yavamia viongozi wa kanisa

Na Said Hauni, Lindi
WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya viongozi wa dini ya Kikristo Parokia ya Nyangao Wilaya na Mkoa wa Lindi huku wakipora fedha taslimu sh. milioni tano.

Polisi Dar wakamata dawa za kulevya za bilioni 1.4/-

Radhia Ramadhani na Joyce Kambota
WATU wanne raia wa Nigeria wamekamatwa na madawa ya kulevya aina ya HEROINE yenye thamani ya shilingi bilioni 1 .4 za kitanzania jijini Dar es Salaam.

Watumishi wazorotesha mapato ya halmashauri

MA D I WA N I w a
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamesema kupungua kwa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo ni dalili inayotokana na uvujaji wa fedha unaofanywa na baadhi ya

MAZUNGUMZO


Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ajuwa na mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kamuni ya Unilever Global, Bw. Paul Polman, Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu)

Babati yapewa siku 14 kuwasilisha mchanganuo

Anneth Kagenda na Flora Amon
HALMASHAURI y a Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imepewa siku 14 kuwa imepeleka mchanganuo mpya ambao pamoja na mambo mengine uwe unaainisha vizuri matumizi ya sh. milioni 77 ambazo inadaiwa kuwalipa wafanyakazi hewa. Agizo hili lilitolewa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Bw. Idd Azzan.

HATARI

Watoto wakicheza kwa kuning'inia katika gari lilokuwa Mtaa wa Braziri eneo la Kinondoni,Dar es salaam jana.bila kujua kuwa wanahatarisha usalama wao.(Picha na Peter Twite)

Adha ya umeme yawakumba wabunge

Anneth Kagenda na Frola Amon
ADHA y a k u k a t i k a
umeme mara kwa mara
imewawakumba wabunge
waliokuwa wakihudhuria
vikao vya kamati za bunge
kwenye Ofisi Ndogo ya
Bunge, hatua iliyowalazimu
kuahirisha vikao hivyo.

Kandoro awashukia mafisadi wa dawa

Na Charles Mwakipesile, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro, amesema mafisadi wanaoiba dawa za Serikali, kuzipeleka kwenye maduka ya watu binafsi na kusababisha uhaba mkubwa wa dawa katika Bohari Kuu (MSD), hawawezi kuvumiliwa.

Adhabu za Yanga zaitoa 'kamasi' TFF

Na Zahoro Mlanzi
KIKAO cha Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kimeshindwa kumalizika juzi kama ilivyotarajiwa kutokana na wajumbe waliohudhuria kikao hicho, baada ya kutokea mvutano katika kufikia muafaka wa rufani zilizowasilishwa na Klabu ya Yanga.

04 April 2012

Madaktari waliogoma sasa wakaliwa kooni

*Tume ya Haki za Binadamu yashauri washtakiwe
*Yaeleza sababu ya kukaa kimya wakati wa mgomo
*Yasisitiza madaktari walivunja matakwa ya katiba

Mashahidi kesi ya ubunge Segerea wakiri makosa

Na Anneth Kagenda
MASHAHIDI wa utetezi upande wa Jamuhuri wamekiri mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufanya kosa la kisheria kwa kutosaini fomu za matokeo katika vituo vyao.

Majibu kipimo cha mbunge wa CHADEMA hadharani

*Watano washikiliwa kuhusika na vurugu
Na Zourha Malisa

Uwezeshaji wajasiriamali kielimu usiwe na kikomo

SERIKALI kupitia Kituo chake cha Uwekezaji nchini (TIC), imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kutoa elimu ya maarifa kwa wajasiriamali wadogo na wale wa kati ili waweze kukuza mitaji yao, kujiendeleza kibiashara na kufikia malengo.

NGUO

Baadhi ya wauzaji nguo za mtumba (kushoto) wakiwaonesha wateja wanguo hizo kama walivyokutwa mtaa wa Agrey ,Dar es salaam jana nguo hizo zimekuwa na soko nchini kutokana na ubora wake.(Picha na Rajabu Mhamila)

TLP yamteua mgombea ubunge A.Mashariki Na Rehema Maigala

SEKRETARIETI ya Tanzania Labour Party (TLP) imemchagua Bw. Micah Mrindoko, kuwa mgombea ubunge wa Afrika Masharika .

Haroun Mahundi; IGP wa mwisho wa Nyerere aliyetuachia mafunzo mengi

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kiwete akimpa pole IGP wa zamani, Bw. Haroun Mahundi alipofiwa na mkewe, Bi. Clara Francis Mahundi mwaka 2010.

Twiga Stars yapata msaada wa jezi

Na Amina Athumani
TIMU ya taifa ya soka ya wanawake (Twiga Stars), imepewa msaada wa jezi na Kampuni ya Galileo by Travelport kwa ajili ya kuisaidia katika maandalizi yake ya kukata tiketi ya  kucheza Fainali za Nane za Kombe la Afrika  kwa Wanawake (AWC), zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

03 April 2012

Mshindi kajulikana, sasa tuijenge Arumeru

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jana ilimtangaza Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.

TIC yatoa changamoto kwa wajasiriamali kuhusu elimu

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimetoa changamoto kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini kusaka maarifa na elimu kama njia ya kujiendeleza kibiashara na kufikia mafanikio.

AFYA KWANZA

Wateja wakinunua samaki waliokaangwa eneo la jikoa samaki Feri Dar es salaam jana,bila kujali ubora na usafi wa eneo hilo hali inayoweza kuhatarisha afya zao.(picha na Peter Twite)

Msitumie kampuni zinazowanyonya wakulima-Dkt Mahenge

Na Rashid Mkwinda, Makete
MWENYEKITI wa Bodi ya Pareto Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji wa wilaya hiyo mkoani Njombe kutotumiwa na baadhi ya kampuni ambazo zina  nia ya kuwanyonya wakulima wa zao la pareto kwa kununua kwa bei ya chini.

Mizengo Pinda aagiza wananchi kupanda miti

Na Damiano Mkumbo, Singida
WAZIRI Mkuu, Bw.
M i z e n g o P i n d a
amewataka Watanzania
kujenga tabia ya kupanda miti kwa
wingi ili kuendeleza maisha yao
sabamba na kuyatunza mazingira.

KITOWEO

Mchuuzi wa samaki akimsaidia mteja wake (kushoto) kufunga mzigo wa samaki kwenye pikipiki namba T 742 BYC, mara baada ya kumuuzia kama walivyokutwa Soko la Kimataifa la Samaki Feri, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha na Charles Lucas)

Waziri Nahodha usidanganyike wala kukurupuka

NALIPONGEZA gazeti
lako kutupatia wananchi
nafasi ya kuelimishana
na kutoa maoni kwa
maendeleo ya nchi yetu.

Chamwino kupewa matibabu bure-DED

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JUMLA ya kaya 1,155
zenye kipato duni katika
Halmashauri ya Chamwino
mkoani Dodoma watapatiwa
matibabu bure.

MNADA WA SAMAKI


Dalali wa soko la kimataifa la Samaki feri(aliyeketi juu) akinadi samaki waliokuwa kwenye gari hilo kama alivyokutwa, Dar es salaam jana(picha na Charles Lucas)

Wafugaji watunishiana misuli na wawekezaji

Na Stephano Samo, Manyara
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vurugu kubwa zimezuka kwenye mashamba ya ngano baina ya wafugaji wa Kijiji cha Gidagamuoda Kata ya Mogitu Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na wakulima wakubwa.Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wafugaji wa Kata ya Mogitu jana walidai kuwa vurugu hizo zilianza juzi baada ya wakulima hao kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji unaofanywa na wakulima wakubwa.

Poulsen kumrudisha Bocco Taifa Stars

Na Zahoro Mlanzi
SIKU chache baada ya mshambuliaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) na Azam FC, kuandika barua ya kustaafu kucheza timu ya taifa, Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeibuka na kusema hatma yake ipo mikononi mwa kocha wake, Jan Poulsen.

02 April 2012

CCM yakabwa koo Arumeru

  • Nassari tishio matokeo ya awali
  • Helikopta yatumika kurinda kura
  • CHADEMA yasinda udiwani

Wabunge CHADEMA wacharangwa mapanga

Na Daud Magesa,
 MWANZA WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia n a M a e n d e l e o (CHADEMA) katika
Majimbo ya Ukerewe,Bw. Salvatory Naruyaga (Machemli) na Bw.Highness Kiwia wa Ilemela, Mwanza, wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM usiku wa kuamkia jana katika kata ya Kirumba jijini hapa.

Mama Salma ahamasisha uchangiaji wa damu

           Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi

Na Anneth Kagenda
WATANZANIA wametakiwa kuondokana na fikra potofu kuwa mtu akitoa damu anapata matatizo ya kiafya, badala yake washiriki kikamilifu katika kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wajawazito wakati wa
kujifungua na ifike mahali vifo hivyo vipungue.

Waandishi waeleza siri ya ushindi tuzo za EIAT

Na David John
WAANDISHI wa Afya
Radio ya Mwanza,
walioshinda Tuzo
za Umahiri Katika
Uandishi wa Habari Tanzania
(EJAT 2011) jana wametoboa siri
za ushindi wao.

Wataalam wa ununuzi, ugavi watakiwa kukuza uchumi

Na Peter Mwenda
MEYA wa Bukoba, Bw. Aman
Anatory, amesema fani ya ununuzi
na ugavi ina jukumu kubwa katika
uchumi kwa vile inahusika moja
kwa moja katika kuinua uchumi.

Post titleWanawake wakidhamiria kuleta mageuzi ya elimu inawezekana

UTASHI wa kusaidia
ama kujitolea katika
shughuli za kijamii
hasa zinazolenga
kuharakisha maendeleo tafiti
zinabainisha kuwa ni moja
wapo ya hatua madhubuti katika
kuendeleza uchumi endelevu.

'Udhaifu wa watendaji chanzo cha migogoro vyama vya siasa nchini'

UPO msemo wa Kiswahili
ulizoeleka kuwa 'lisemwalo lipo
na kama halipo linakuja'.

Ofisa Elimu: Walioshindwa kuwapeleka wanafunzi shule kushtakiwa mahakamani

Na Said Hauni, Lindi
WANAFUNZI wapatao 326 sawa
na asilimia 22 kati ya 1,605,
waliochaguliwa kujiunga na
masomo ya sekondari mwaka
huu katika Halmashauri ya Lindi mkoani
Lindi bado hawajaripoti kwenye shule
walizopangiwa.

'Vita madawa ya kulevya Zanzibar ni endelevu'

SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar imesema
kutokamilika kwa choo
cha kufichua madawa ya
kulevya katika Uwanja wa Ndege
wa Abeid Amani Karume si sababu
ambayo inaweza kuzorotesha shughuli
za mapambano dhidi ya dawa za
kulevya.

Wajumbe wamkataa Katibu wa CCM

Na Patrick Mabula, Shinyanga
HALMASHAURI Kuu ya
Chama cha Mapinduzi
(CCM) Wi l a y a y a
K a h a m a m k o a n i
Shinyanga imemkataa Katibu wa
CCM wilayani humo Bi. Magreth
Chusi kwa kile walichodai anatumia
vibaya madaraka yake.

Mama mzazi wa Whitney avunja ukimya

NEW YORK,Marekani
MAMA wa mwanamuziki wa zamani, Whitney Houston amevunja ukimya kuhusu kifo cha mwanaye, baada ya kusema kwamba alifanya kila liwezekanalo ili kumnusuru mwanaye aondokane na matumizi ya dawa za kulevya.

Mkwassa ataka Twiga Stars iweke kambi mapema

Na Amina Athumani
KOCHA Mkuu wa timu ya soka la Wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuiweka kambini mapema timu hiyo mara kambi hiyo itakapovunjwa keshokutwa kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya raundi ya pili.