17 April 2012

CHADEMA wajitoa uchaguzi EALA

  • Wadaia mchakato huo umetawaliwa na rushwa
  • Wabunge wake wapinga marekebisho sheria
 Na Benedict Kaguo, Dodoma
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameitaka Serikali kuondoa mfumo wa usimamizi mbovu wa sheria ili kupunguza madhara yanayoendelea kujitokeza kwa Taifa kama warazifanyia marekebisho sheria hizo kila wakati.

Walisema sheria zilizopo sasa, bado hazijaweza kusimamiwa kikamilifu hivyo kusababisha madhara kwa wananchi yakiwemo vifo, ulemavu na magonjwa ya akili.

Mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika (CHADEMA), aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo ya Usalama barabarani.

Alisema liliopo nchini kwa sasa sio kutungwa sheria mpya kwani matukio mengi ya ajali yanachangiwa na usimamizi mdogo wa sheria zilizopo na kufafanua kuwa, asilimia 74 ya ajali za barabarani zinasababishwa na uzembe wakati asilimia 14 ni kasoro zilizopo katika sheria husika.

Bw. Myika alisema, kama mfumo wa utawala hautaweza kusimamia sheria hizo ni wazi kuwa matukio ya ajali za barabarani yataendelea kutokea na kuleta madhara kwa wananchi kwa kuongeza idadi ya vifo na ulemavu wa kudumu.

“Tabia ya askari wa Usalama Barabarani kuchukua rushwa, vinachangia kuliangamiza Taifa letu, Serikali ielekeze nguvu kwenye mfumo wa utendaji na usimamizi wa sheria zilizopo badala ya kutunga sheria mpya ambazo mwisho wa siku, zinakaa katika  makabati bila kuzifanyia kazi,” alisema Bw. Mnyika.

Akizungumzia Marekebisho ya Sheria za kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Myika aliitaka Serikali ieleze kwanini kiwango cha dawa zinazokamatwa kinaongezeka siku hadi siku wakati idadi ya watuhumiwa ikiendelea kupungua mwaka hadi mwaka.

Alisema kutunga sheria za kukabiliana na dawa za kulevya, hakusaidii kama hakuna rekodi ya watu wangapi wamefungwa kwa kuhusika na biashara hiyo hivyo aliitaka Serikali ishughulikie kiini cha tatizo badala ya kuendelea kutunga sheria.

Kwa upande wake, Mbunge wa Rombo, Bw. Joseph Selasini (CHADEMA), alisema kama Serikali itaendelea kutunga sheria mpya ni wazi haitasaidia kupunguza tatizo la ajali bali ikakuwa imetengeneza mtandao mpana kwa askari wa Usalama Barabarani kupokea rushwa.

Wakati huo huo, mbunge wa Masasi, Bi. Mariam Kasembe (CCM),  amekataa kuunga mkono hoja wala kuchangia chochote Katika miswada inayoendelea bungeni ya marekebisho ya sheria mbalimbali hadi Serikali itakapopeleka bungeni Sheria ya Korosho ambayo imekuwa ikiahidiwa kwa muda mrefu sasa.

Bi. Kasembe alionesha msimamo huo bungeni mjini Dodoma jana na kudai kuwa, kwa muda mrefu Serikali imeahidi kupeleka bungeni muswada huo ili kutungwa sheria ambayo itasimamia kikamilifu zao la korosho badala yake suala hilo limekuwa likipigwa danadana.

Alisema kwa muda mrefu, wakulima wa korosho hawatendewi haki kutokana na ukosefu wa sheria madhubuti ya korosho badala yake wanashindwa kunufaika na fursa zinazotolewa kwenye zao hilo.

“Fedha nyingi zimekuwa zikiishia Bodi ya Korosho na kunufaisha wajanja wachache huku wakulima wa zao hilo wakiendelea na matatizo yao pamoja na ukosefu wa pembejeo za kilimo.

“Leo sitaunga mkono hoja yoyote wala kuchangia chochote hadi Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakapoleta sheria ya korosho bungeni, kwanini inapigwa danadana kila siku,” alihoji.

Aliilaumu Bodi ya Korosho nchini na kudai imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wakulima badala yake fedha zinazotolewa kwa ajili ya wakulima zinaishia katika bodi hiyo.

2 comments:

  1. HONGERA CHADEMA KWA KUONYESHA UKOMAVU. HUU SIO WAKATI WA KULA NA KUHUSUDU VITU HARAMU. hARAMU IITWE HARAMU.

    ReplyDelete
  2. Na mzinzi aitwe mzinzi.

    ReplyDelete