16 April 2012

Tutalinda uhuru wa dini zote-Dkt. Shein

Na Mwandishi Maalum,
Ikulu Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kulinda uhuru wa dini zote lakini haitavumilia vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa jina la dini huku ikisisitiza uadilifu kwa viongozi wa dini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein aliyasema hayo
jana katika hotuba yake aliyoitoa
katika hafla ya kumweka wakfu
Askofu wa 10 wa Dayosisi ya
Zanzibar Michael Henry Hafidh.
Alisema, ustawi wa dini
mbalimbali Zanzibar unahusika
na Sera ya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar ya uhuru wa kuachia
kanisa kuendesha seminari zao
na makongamano yao bila ya
kuingiliwa.
Alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa
shughuli hizo za kidini zimekuwa
zikiendeshwa kwa amani ambapo
kwa bahati mbaya pamoja na hayo
kumekuwepo nyakati ambapo
kutofahamiana kumejitokeza katika
baadhi ya makongamano.
"Serikali imeweka utaratibu
maalum wa utoaji ruhusa wa
makongamano hayo, taratibu hizo
ni pamoja na utunzaji wa amani na
kutobughudhiana kidini‚ tuelewe
sote kwamba viongozi wa dini
ni walimu na walezi wa jamii na
wanadhamana kubwa mbele ya
Mwenyezi Mungu," alisema Dkt.
Shein.
Aidha, alisema kuwa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea
kufanya kila linalowezekana kulinda
haki za Watanzania katika kufuata
dini na kuabudu dini waitakayo na
kuishi bila ya kubaguliwa kutokana
na sababu ya dini, kabila au rangi.
Alisema, hakuna budi wananchi
wote kwa pamoja kujivunia na
kuiendeleza hali ya amani na
utulivu iliyopo hapa nchini ambapo
ziko nchi mbalimbali wamekuwa
wakikosa hali hiyo kwa sababu ya
migogoro inayotokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kidini,
kisiasa na kikabila,
Pamoja na hayo Dkt. Shein
alisema kuwa licha ya kuwa
Tanzania haina dini ya serikali kama
ilivyokuwa ikisisitizwa na Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere na viongozi wa amamu
zilizofuata lakini Watanzania wengi
ni wafuasi na waumini wa dini
zenye madhehebu tofauti.
Kutokana na hilo Dkt. Shein
alisisitiza jukumu la kulinda
heshima baina wananchi na
usalama wa nchi linategemea sana
mafunzo yanayofundishwa na
yanayohutubiwa na viongozi katika
nyumba za ibada.
Pia, alisisitiza viongozi wa
dini mbalimbali wana wajibu
wa kuhakikisha sehemu za ibada
zinatumika kwa ibada tu bila ya
kuingiza mambo mengine na kutoa
mwito kwa Jumuiya zote za kidini na
wananchi kuendelea kuheshimiana
na kuishi bila ya kubaguana.
"Sote tuwe na lengo moja la
kuiletea maendeleo nchi yetu kwa
manufaa ya watu wake wote,”
alisema Rais.
Pia Dkt. Shein aliwaeleza
waumini hao kuwa mambo yao
waliyomueleza ameyasikia na
atayafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment