03 April 2012

Mshindi kajulikana, sasa tuijenge Arumeru

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jana ilimtangaza Bw. Joshua Nassari (CHADEMA), kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
Katika uchaguzi huo, Bw. Nassari aliwashinda wagombea wenzake saba akiwemo mpinzani wake wa karibu Bw. Sioi Sumari (CCM).

Bw. Nassari alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 32,972 sawa na asilimia 54, wakati Bw. Sumari alipata kura 26,757 sawa na asilimia 44.

Vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo  na kura zao kwenye mabano ni DP (77), NRA (35), AFP (139), UPDP (18), TLP (18), na SAU (22). Jambo la kufurahisha, vyama vyote vimekubali matokeo yaliyotangazwa na kuipongeza CHADEMA kwa ushindi huo.

Mchuano mwingine kati ya CCM na CHADEMA ulikuwa katika nafasi za udiwani kwenye mikoa mbalimbali. Katika chaguzi hizo, baadhi ya wagombea wa CHADEMA waliibuka na ushindi.

Sisi tunasema kuwa, kiu ya wakazi wa Arumeru Mashariki ni kasi ya maendeleo ambayo waliahidiwa na mgombea wa chama kilichopata ushindi hivyo jambo la msingi ni kutekeleza ahadi kwa vitendo.

Wakazi wa jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa migogoro ya ardhi ambayo imedumu muda mrefu bila kupatiwa ufuimbuzi wa kudumu na kusababisha wananchi wakose maeneo ya kilimo ambacho ndio uti wa mgongo.

Ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi huo umetokana na imani ya wananchi juu ya sera zao na ahadi ambazo zilizotolewa na viongozi wa juu hivyo kama hazitatekelezwa ni rahisi wananchi kufanya mapinduzi ya kuchagua mwakilishi mwingine ambaye atasikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati.

Imani yetu ni kwamba, chama chochote cha siasa ili kiweze kukubalika na wananchi waliokichagua lazima kitekeleze ahadi zake kwa vitendo. Hali hiyo ndiyo itawafanya wananchi waendelee kukipenda, kukiheshimu na kukichagua katika chaguzi zote.

Tunaipongeza CHADEMA kwa ushindi wake, CCM na vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo kwa kukubali matokeo. Huu ni wakati mzuri wa kujipanga, kukijenga chama na kurudisha imani kwa wananchi ili uchaguzi ujao waweze kukichagua.




1 comment:

  1. USHAURI WA WAZI KWA MH. JOSHUA NASSARI (MBUNGE MTEULE WA ARUMERU MASHARIKI).

    KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE NAKUPA HONGERA SANA.

    KABLA HATA HAJAAPISHWA KUWA MBUNGE KAMILI NAOMBA UANZE MARA MOJA KUTAYARISHA MIKAKATI YA KUSHUGHULIKIA YAFUATAYO:
    1. KUCHAMBUA AHADI ZOTE WALIZOTOA VIONGOZI WATENDAJI WA SERIKALI WA CCM WAKATI WAKIFANYA KAMPENI ZA KUMNADI MGOMBEA WAO SIOI.
    CHAMBUA AHADI ZA MH. WASSIRA, NAIBU WAZIRI ARDHI (AKIWA MH.MBUNGE WA ARUMERU MAGH)KUFUATIA AHADI YAKE YA KUCHUKUA MASHAMBA AMBAYO HAYAJAENDELEZWA ILI WAPEWE WANANCHI WAKO PAMOJA NA AHADI NYINGINEZO. CHAMBUA AHADI ZA MH. DR. MARY NAGU AMBAYE ALISEMA HATASHIRIKIANA NA MBUNGE ATAKAYECHAGULIWA NJE YA CCM) PANGA MPANGO UMFUATE IKIWA ATAKUKATALIA KUTIMIZA MIPANGO ILIYOPITISHWA NA BAJETI YA MWAKA HUU KWA AJILI YA WANANCHI YA ARUMERU MASHARIKI. AKIKUTATALIA MCHONGEE KWA WANANCHI UNAOWAWAKILISHA TUONE KAMA ATAZUIA NGUVU HIYO YA UMMA.

    KUNA MLOLONGO WA AHADI ZILIZOTOLEWA NA NA VIONGOZI WENGINE KAMA RAIS MSTAAFU, MBUNGE WA MONDULI MH. LOWASSA, MBUNGE WA MTERA MH. LUSINDE. UKIMULIZA KWA NINI ALIWATUKANA WANANCHI WAKO KATIKA KAMPENI(MCHONGEE KWA WAPIGA KURA WAKE AU NEC YA CCM KWA KUWA NDIO WALIMTUMA. HAWA VIONGOZI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIWATAJA MAWAZIRI NA WATENDAJI WENGINE SERIKALINI KUWA WANGALITIMIZA AHADI HIZO KAMA ZA ARDHI, MAJI , UMEME, BARABARA,N.K.

    AHADI ZOTE ZIMEREKODIWA NA ZIMEZAMBAZWA KWA WATANZANIA WOTE KUPITIA VYOMBO VYA MAWASILIANO. TUNAIMANI KUWA WALIYOYAZUNGUMZA SI YA UONGO WALA YA KUKEJELI WATU. TANAAMINI WANANCHI WALIOAHIDIWA NI WALE WALE WALIOKUPIGIA KURA KPITIA CHADEMA NA WALE AMBAO HAWAKUKUPIGIA WAKIWAKO WANACHAMA WA CHADEMA, CCM NA VYAMA VILIVYOSHIRIKI.

    KWENYE KUGAWA MAENDELEO HAKUNA KUCHAGUA WALE WALIOPIGIA KURA CCM NA WALE WALIOKIPIGIA CHADEMA. HII NI KULINGANA NA DHANA YA DEMOKRASIA KAMILI

    KWA MANTIKI HII, HAKIKISHA KUKAMILISHA ORODHA HII YA AHADI UJE UIPELEKE KUNAKOHUSIKA ILI ZISHUGHULIKIWE. UKIKWAMA, RUDI KWA WANANCHI WAKO NA WATAFAHAMU LA KUFANYA. (UWAAMBIE KUWA WALIKUWA WAMEDANGANYWA HIVYO WASIKUBALI TENA KUFANIWA HIVYO KWA CHAGUZI ZIJAZO. IKIBIDI UCHAPISHE NA KUSAMBAZA AHADI HIZI KWENYE VYOMBO MBALI MBALI. WAKIKANA KUZITOA, TUMIA USHAHIDI WA AINA MBALIMBALI. HAWAWEZI KUKANA SAUTI ZAO.

    HUU NDIO UJASIRI WA UKOMBOZI WA WATU WALIOKUCHAGUA NA WASIOKUCHAGUA. WATANZANIA WOTE WATAIGA MTINDO HUU WA KUORODHESHA AHADI WAKATI WA KAMPENI.

    KWENYE KAMPENI SI MAHALI PA KWENDA KUWAGHILIBU, KUWAHADAA NA KUWADANGANYA WANANCHI. KAMA HAWA VIONGOZI WALISEMA UONGO BASI WARUDI KWA WANANCHI WAWAMBIE KUWA WALIKUWA WANAWADANGANYA ILI WAWAPE KURA ZAO.

    HII ITAWAKOMESHA VIONGOZI WASIWE WAKISIMAMA MAJUKWAANI NA KUTEMA MANENO YA UONGO NA AHADI HEWA. HII ITAWAZUIA WASIDANGANYE KWENYE KAMPENI NYINGINE. WASIIPONZE SERIKALI KWA KUWALUNDIKIA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA.

    WATANZANIA WASIENDELEE KUDHARAULIWA. WAMESOMA SANA KULIKO HAPO NYUMA. WALIOMALIZA DARASA LA SABA, SEKONDARI,VYOU VIKUU NA TAASISI NYINGINE NI WENGI. WASTAAFU NI WENGI VIJINI. WANAUWEZO MKUBWA WA KUCHAMBUA MAMBO.

    2)USISAHAU KUORODHESHA AHADI ZAKO ULIZOTOA NA KUZIFUATILIA WANANCHI WASIJE KUKUMBUA. UKIKWAMISHWA WAJULISHE WANANCHI.

    UKICHANGANYA AHADI ZAKO NA HIZO ZA WAHESHIMIWA WAZIRI NA VIONGOZI WA SERIKALI UTAKUWA NA MTAJI MKUBWA WA KUENDELEZA MAENDELEO YA WANANCHI WA ARUMERU MASHARIKI. KUMBUKA VIONGOZI HAWA NI WA SERIKALI INAYOTUMIA SERA ZA CCM NA NDIO WENYE KUTOA MAFUNGU. UZURI WAMEKWISHA KUWAAHIDI WANAARUMERU.

    ReplyDelete