Na Daud Magesa,
MWANZA WABUNGE wawili wa Chama cha Demokrasia n a M a e n d e l e o (CHADEMA) katika
Majimbo ya Ukerewe,Bw. Salvatory Naruyaga (Machemli) na Bw.Highness Kiwia wa Ilemela, Mwanza, wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM usiku wa kuamkia jana katika kata ya Kirumba jijini hapa.
Katika tukio hilo mbunge wa
Jimbo la Nyamagana, Bw. Ezekia
Wenje, alinusurika, ingawa baadhi
ya mawakala wa chama hicho
wamejeruhiwa akiwemo mtu mmoja
ambaye amepata jeraha katika
kiganja cha mkono wa kulia.
Waliojeruhiwa mbali na wabunge
hao ni pamoja na Bi.Judith Madaru,
ambaye amechomwa kisu upande
wa titi la kushoto, Bw.Haji
Mkwenda (21), amevunjika mguu
wa kulia, Bw.Ivor Mashimba, yeye
alijeruhiwa kichwani na mdomoni
huku Bw.Ahmed Waziri anayedaiwa
kuwa mfuasi wa CCM akikatwa
kiganja cha mkono wa kulia na
amelazwa Hospitali ya Bugando,
huku wengine wakilazwa Hospitali
ya Sekou Toure
Kwa mujibu wa habari kutoka
eneo la tukio zilizothibitishwa na
jeshi la polisi, sakata hilo lilitokea
saa 8:20 usiku wa kuamkia jana
katika Mtaa wa Bukoba, Kata ya
Kirumba Wilaya ya Ilemela jijini
hapa, ikiwa ni saa chache kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi mdogo
wa udiwani.
Habari zinaeleza kuwa wabunge
hao Bw. Kiwia wa Jimbo la Ilemela
na Machemli, Jimbo la Ukerewe
walifika eneo la mtaa huo baada
ya kupata tetesi kuwa kulikuwa na
wafuasi wa CCM wakitoa rushwa
ya fedha, chumvi na vitu vingine
kwa wananchi wa mtaa huo, ili
kuwashawishi wapige kura za
upendeleo kwa mgombea wa chama
chao.
K w amb a w a b u n g e h a o
walipofika eneo hilo, wakiwa na
gari la CHADEMA, walishtukia
wa k i z i n g i rwa n a wa f u a s i
wanaoaminika kuwa CCM na
baadhi ya vyama vingine na kuanza
kushambuliwa kwa silaha za jadi,
mapanga kiasi cha kuwajeruhi
vibaya.
Katika mashambulizi hayo
mbunge wa Jimbo la Ukerewe
alikatwakatwa mapanga kichwani
na baadhi ya sehemu za mwili
wake na huku Mbunge wa Jimbo
la Ilemela akikatwakatwa mapanga
kichwani na mgongoni ambapo
amejeruhiwa vibaya.
Al i s ema k uwa h a l i y a
Bw.Machemli inaendelea vizuri
baada ya kushonwa majeraha katika
hospitali ya BMC jijini Mwanza na
kuruhusiwa kurejea hotelini kwake
kuendelea kuuguzaa majeraha
aliyonayo.
Lakini Mbunge wa Jimbo la
Ilemela, Bw.Kiwia kutokana na hali
yake kutokuwa nzuri kwa sababu
ya kupata majeraha makubwa
kichwani katika tukio hilo (leo)
jana,alisafirishwa kuja jijini Dar es
Salaam kwa matibabu zaidi katika
hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katibu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA),
mkoani Mwanza, Bw.Willy
Mushumbusi, alisema kuwa Bw.
Kiwia amejeruhiwa vibaya kichwani
na mgongoni, ambapo katika tukio
hilo, yeye anadai kumwagiwa maji
machoni yanayosadikiwa kuwa na
kemikali ambapo macho yanawasha
na hali yake si nzuri.
“Kutokana hali yake kuwa
mbaya na kutokuwepo kwa
vifaa cha TC-Scan cha kubaini
madhara aliyoyapata kichwani
katika hospitali za Rufaa Bugando
amelazimika kusafirishwa kwa
ndege kupelekwa hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu.Lakini
Bw. Machemli amenipigia kuwa
ameruhusiwa kutoka hosptalini,”
alisema Bw.Mushumbusi.
Katibu huyo alilaumu jeshi la
polisi kwa kufumbia macho vitendo
invyofanywa na wafuasi wa chama
tawala na kudai wakati tukio hilo
likitokea usiku, polisi walikuwa
karibu na tukio lakini hawakutoa
msaada wowote wala kuchukua
hatua.
Alisema mtu mmoja jina
halijafahamika, katika tukio hilo
alikatwa kiganja cha mkono
na mwenzake ambaye alikuwa
amedahamiria kumkata kwa panga
mbunge Machemli.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Mwanza, Bw. Clement Mabina,
alipoulizwa kwa simu kuhusiana na
tukio hilo linahusishwa na wafuasi
wa chama chake, alikana vikali
akisema hawahusiki kwa namna
yoyote ile.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mwanza (RPC), Kamishna Msaidizi
wa Polisi (ACP) Liberatus Barlow,
hakupatikana kuthibitisha tukio
hilo.
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai Mkoani Mwanza (RCO ),
ACP (Deusdedit Nsimeki alikiriki
kujeruhiwa kwa wabunge hao wa
CHADEMA.
Wakati huo huo, taarifa
iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu
wa Chadema, Bw. Zitto Kabwe,
kupitia mtandao wa Mabadiliko,
akiwa hospitalini Bugando alisema
kulikuwa na majeruhi mmoja
ambaye awali alijitambulisha ni
mwana -Chadema, lakini baadaye
iligundulika ni mtu wa UVCCM,
Bw. Ahmed Mkilindi.
Mtu huyo kwa mujibu wa Bw.
Zitto alikuwa anaongoza kikosi
kilichowavamia kina Kiwia. Alipata
jeraha mkononi.
Alisema hali ya Kiwia sio nzuri
sana. “Anatakiwa kufanyiwa CTscan
kuona athari aliyopata (maana
kapigwa na shoka na mapanga
kichwani). Bahati mbaya hapa
Bugando kifaa hicho hakifanyi
kazi,” alisema Bw. Zitto,” alisema
na kuongeza;
“Nimezungumza na Katibu wa
Bunge na ndani ya muda mfupi
ndg. Kiwia atasafirishwa kupelekwa
Muhimbili kwa uangalizi zaidi.”
Alisema Bw. Machemuli
anaendelea vizuri alitoka hospitali
jana (alipata huduma ya Kwanza
Sekou Toure).
Hiyo ccm inamabo ya kijinga sana tena sana hao wafuatiliwe na wakamatwe waliofanya mambo machafu hayo.Na utashangaa polisi hawatafanya kitu chochote.Tuombe Mungu nchi yetu hii hata askari hatuna imani nao.Viongozi wa chadema Mungu atawalinda na kuwaponya kwa damu ya Yesu Kristo.Tuko katika maombi kwa ajili ya viongozi hao wa chadema waliojeruhiwa na majambazi ya ccm. chama cha majambazi.
ReplyDeletePole sana Wabunge wa Wananchi ambao wamethubutu hata kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kuwatetea Watanzania,tuko pamoja nanyi,MUNGU awaponye hataka kwani DAMU zenu zinadai mbele za MUNGU,na haki itapatikana,Huu ni Wakati wa Wawatanzania kutetea haki zao wenyewe,kwa manaona jinsi majizi yalivyotayari kuumiza wanaotetea haki za Wanzania.
ReplyDeleteMwizi ni mwizi tu hata mbuzi mwenye tabia ya wizi hupiga pembe mbuzi wenzake ndivyo ccm wanavyofanya damu hii inayomwagika hakika haitapotea bure bali ni sadaka takatifu itolewayo katika muda huu wa mabadiliko ktk nchi yetu, hivyo watanzania tuzidi kuwaombea wapiganaji hawa MUNGU wa Mbinguni awaponye haraka warudi kwenye uwanja wa mapambano na zaidi sana watashinda kwa kuwa MUNGU yu pamoja nao!
ReplyDeleteHAWA MAJERUHI NI SAWA NA WAHANGA /MASHAHIDI WANAOPIGANIA DEMOKRASIA. DAMU YAO ILIYOMWAGIKA ITATUOKOA SISI WANYONGE WA TANZANIA.
DeleteNAWASIHI CHADEMA NA WANANCHI WA MWANZA NA NDUGU ZAO WASILIPE KISASI. MUNGU ATAWALIPA TU. WASAMEHENI KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO.
CHA KUSHUGULIKIA KWANZA NI AFYA ZENU NA KUHAKIKISHA WALIOWAFANYIA VITENDO HIVI WANAKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA. HAKI ITENDEKE KWA KUWA WATU WANAWEZA KUTUMIA MTINDO KAMA HUO KUUMIZA WENGINE. HAWA NI TERORISTS WASIHURUMIWE WALA KULINDWA KWA KUWA UMA WATANZANIA UTAWATAFUTA POPOTE WALIPO NA KUWAPELEKA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
hAKI IKIKOSEKANA HATA ITAFUTWE NCHI ZA NJE KAMA KUTAKUWA KULINDANA.
NAWASIHI CHADEMA MUENDELEE KUWA WATULIVU BILA KULETA VURUGU KAMA MNAVYOFANYA KWA SHIDA.
ENDELEENI KUTUMIA KURA ZA WANANCHI KAMA SILAHA KUU YA DEMOKRASIA. LINDENI HAKI HII YA DEMOKRASIA KUFA NA KUPONA BILA KUTISHIKA ILI HAKI HII ISIPORWE NA MAJAMBAZI YA KISIASA.
KURA NDIZO PEKEE ZITAKAZOWAANGAMIZA MAFISADI NA KULETA MAENDELEO YA KWELI KWA WATANZANIA WOTE.
MSIWE WEPESI WAKUHUKUMU BILA KUJUA CHANZO , MNAAMINI MANENO YAKUAMBIWA NA KUYAKUBALI BILA KUTAFAKARI, HAO WANAODAI WAMEUMIZWA MBONA HAWASEMI WAO NDO WALIANZA KUJERUHI WATU? NAPINGA SANA VITENDO HIVIVYAKINYAMA LAKINI UKWELI USIFICHWE, SAA SABA ZA USIKU UNAFANYA NINI KTK ENEO LISILOLAKO NAWE SI MPIGA KURA WA ENEO HILO? KUNA MTU KAVUNJWA MGUU, MMOJA KACHOMWA KISU KWENYE TITI MWINGINE KAKATWA KIGANJA JE HAWA NAO WAMEKATWA NA NANI NA INASEMEKANA SI WANACHADEMA, MBONA MNAPENDA KUSEMA UONGO NA KUFICHA UKWELI, MBELE YA MUNGU HAKUNA LITAKALO FICHIKA. NAWAPA POLE WOTE WALIOPATWA NA MKASA HUO MWENYEZI MUNGU AWAPE AFYA NJEMA MAPEMA. NDUGU ZANGU TUONDOKANE NA CHUKI ZISIZO NA MSINGI TANZANIA YENYE NEEMA ITAJENGWA NASI SOTE TUMRUDIE MUNGU KATIKA KUTENDA MATENDO MEMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteWewe hapo juu, hakuna aliyehukumu. Mchangiaji alisema "wahusika wakamatwe na wapelekwe mahakamani" ambapo ukweli utapatikana.
DeleteNikuulize, wewe ukitembea usiku hata wa manane ukipigwa utasema ni sawa? Waliowapiga nao walitoka wapi saa hizo? Je, eneo hilo lilikuwa na amri ya kutotembea usiku? Ukishakuwa Mbunge usitembee usiku hata kama ni kwenda hospitali au kutoka kwenye sherehe au kilio? Hii Tanzania yetu ni huru na yenye amani na kila mtu ana haki ya kutembea popote na saa yoyote mradi asivunje sheria isipokuwa kama kuna amri rasmi ya serikali ya kutotembea eneo fulani kwa wakati fulani.
Waliowapiga hawa walikuwa wengi zaidi yao. Kwa nini hawakuwapeleka kwenye vyombo vya sheria? Ita unyama unyama. Ujambazi ni ujambazi. Kumuumiza binadamu mwenzio sio sawa. Jifanye kama ni wewe ungalisikiaje? Kuwa na huruma na ukemee mabo maovu kama haya na si kuyakuza kwa kuwa yanaweza kukupata wewe au ndugu zako.
VYOMBO VYA DORA VIFANYE KAZI YAKE BILA WOGA, HAYA MATENDO MAOVU YASIPOZIBITIWA MAPEMA TUNAKOELEKEA HALI ITAKUWA MBAYA ZAIDI,POLENI WOTE MLIOPATWA NA MKASA HUO MUNGU AWAPE MOYO MKUU WA KUWEZA KUSAMEHE WALIOWAKOSEA ZAIDI SANA TUJIFUNZE KUVUMILIANA BILA KUUMIZANA. FUNDISHO KWETU SOTE TUJIEPUSHA NA SIASA ZA CHUKI TANZANIA TUNAYOTAKA KUIJENGA NI MOJA KWANINI TUPIGANE WENYEWE KWA WENYEWE? TUKIONDOA UBABE MAMBO YATAKWENDA SHWARI
ReplyDeleteVYOMBO VYA DORA VIFANYE KAZI YAKE BILA WOGA, HAYA MATENDO MAOVU YASIPOZIBITIWA MAPEMA TUNAKOELEKEA HALI ITAKUWA MBAYA ZAIDI,POLENI WOTE MLIOPATWA NA MKASA HUO MUNGU AWAPE MOYO MKUU WA KUWEZA KUSAMEHE WALIOWAKOSEA ZAIDI SANA TUJIFUNZE KUVUMILIANA BILA KUUMIZANA. FUNDISHO KWETU SOTE TUJIEPUSHA NA SIASA ZA CHUKI TANZANIA TUNAYOTAKA KUIJENGA NI MOJA KWANINI TUPIGANE WENYEWE KWA WENYEWE? TUKIONDOA UBABE MAMBO YATAKWENDA SHWARI
ReplyDelete