17 April 2012

Operesheni ya kuzuia kelele za mabaa iendelee

NINAPENDA kumpongeza S u l e i m a n K o v a ,kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova kwa operesheni ya kuzisaka na kuzifunga kumbi zinazopiga kelele usiku na hata mchana iliyoendeshwa mwishoni mwa mwaka jana hapa jijini. (Majira, Oktoba 6, 2011).
Mimi nilikuwa nje ya nchi lakini
matokeo yake tuliyaona hata wakati
wa sikukuu ya Noeli. Lakini sasa
hali ni mbaya zaidi, sehemu mpya
pia zimezuka.
Athari ya kelele na mayowe kwa
binadamu inaeleweka.Masikio
yanawezakuhimili kelele kwa
kiwango fulani tu.Zaidi ya hapo
huwa ni kero. Kifupi kelele ikizidi
hufanya mtu achukie mazingita
yake. Hata wanyama hukumbia
makazi ya watu au barabara na
reli wakatokomea msituni, kelele
inawatisha.
Kelele ikizidi sana (zaidi ya
decible 30) hupasua viwango vya
masikio. Hatimaye mtu huwa
kiziwi. Wataalam wanasema, kelele
ikiendelea kwa muda mrefu mtu
huweza kupata kichaa.
Ni dhahiri wagonjwa, watoto
wajawazito , wanafunzi na hata sisi
tuliowazima tunaathirika sana na
kelele hapa jijini. Athari ni nyingi
lakini kubwa ni kukosa usingizi,
utulivu na amani katika maisha.
Inaharibu kabisa maisha ya wakazi
wengi. Mtu huwezi kuwa makini
na hivyo kurudisha nyuma kabisa
maendeleo yako na ya taifa zima.
Nchi nyingi duniani zina sheria
za kuzuia kelele. Hapa kwetu pia
tunazo lakini hatuzifuati. Nitaje
chache tu
*Mathalani, Sheria ya Usalama
na Afya Kazini (Occupational
Safety and Health Act.2003, Act
No. 5) Hii inalinda afya na usalama
wa mfanyakazi ikiwemo kumkinga
dhidi ya kelele nyingi kazini na
viwandani. Ikiwa hapana budi,
basi apewe vifaa maalumu vya
kumkinga asidhurike na kelele.
Aidha viwanda visiwe karibu na
makazi ya watu.
Sheria ya Vileo (The intoxicating
Liquor Act, Cap 77). Hii imeweka
aina ya leseni muuzaji wa pombe
awe nayo. AIdha inaelekeza saa
ya kufungua na kufunga mabaa
hayo. Uadilifu wa mwenye biashara
hiyo ni shartu mojawapo. Baa
ifungwe kabla ya saa 5 usiku.
Asiruhusu kero ya aina yoyote ile,
hasa makelele ya muziki.
Siyo kila nyumba inaruhusiwa
kuwa ya biashara, hususan ya baa
au night club hapa mjini.Sheria ya
mipango miji nchini (The Town
and Country Planning ACT, Cap
355) imetenga maeneo na viwanja
maalumu kwa shughuli za biashara
katika maeneo ya makazi ya watu.
Viongozi na wataalamu serikalini
na manispaa wanaielewa sana
sheria hii. Haifuatwi, ndiyo maana
kila nyumba ina biashara.
Kumbi na baa zinazoleta kelele
usiku hapa jijini zinafahamika.
kwani kuna malalamiko mengi
yanawafikia vyombo vya dola kila
kukicha na viongozi wa manispaa
zetu wanajua fika lakini hakuna
utekelezaji.
Kwenye maeneo hayo ambayo
hufahamika kwa kelele kumegeuzwa
'Night club'. Hupiga muziki kila
siku kuanzia saa tatu hadi saa 10
alfajiri/bila kujali madhara yake
kwa jamii inayozunguka. Viongozi
wanajua!.
Swali: Jeuri hii wanaipata
wapi?
Jibu : Ni jepesi, kutoka kwa
viongozi wa mamlaka husika yaani
manispaa, polisi na madiwani.
Aidha sisi wananchi ndio wa
kubeba kawama kubwa. Nani wa
kulaumiwa kwa kelele za harusi
(rusha roho na michiriko) mitaani.
Je wananchi wanaopiga miziki
ya redio mitaani na Tv nyumbani
mwao tunawafanya nini? Na hao
wenye maduka au mikokoteni ya
kanda za muziki, nani anawaruhusu
hawa?
Huu ni mtindo wa ubongo wa
jamii nzima. Ni saratani imeikumba
miji yetu.
Bahati mbaya operesheni ya
kamanda Kova imekuwa sana na
zingine nyingi zilizopita. Ni ya
' zima moto'. Aidha haikuwa ya
kitaalmu na ya lengi la kudumu
muda mrefu. Sasa kero imepamba
moto hapa jijini.
Nchi hii haiwezi ikaendelea kwa
kunywa pombe na kucheza muziki
usiku kucha na mchana kutwa.
Ni kwa kufanyakazi kwa jitihada,
umakini na maarifa. Sisemi watu
wasiburudike. lakini siyo masaa
ishirini na nne.
Nawaomba viongozi hususan
wa manispaa wasimamie swala hii.
Linatukera sana. Wenye mabaa na
kumbi hizo hawana nia njema.
Viongozi wa dini nao wasaidie.
Ni jamii ndiyo inayoteketea hususan
madili yanatoweka kabisa.
Sheria ya vileo inawapa raia
uwezo wa kupinga baa na kumbi
hizo zisianzishwe katika nyumba
au maeneo mnayofikiri hayafai au
yataleta athari kwa wakazi wake.
Aidha inawawezesha kupinga
leseni hizo zisitolewe tena iwapo
hamridhiki na kuwepo kwake.
Nakusihi sana kamanda Kova
uanzishe tena operesheni hiyo.
Mkishirikiana na mamlaka
zinazohusika nia na lengo lako
litatimia. Sisi wananchi tupate
amani na utulivu majumbani na
mitaani kwetu.
Nakutakia kazi njema.
Mungu Ibariki Tanzania
Daudi A Daudi
S.L.P 62018
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment