05 April 2012

Babati yapewa siku 14 kuwasilisha mchanganuo

Anneth Kagenda na Flora Amon
HALMASHAURI y a Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imepewa siku 14 kuwa imepeleka mchanganuo mpya ambao pamoja na mambo mengine uwe unaainisha vizuri matumizi ya sh. milioni 77 ambazo inadaiwa kuwalipa wafanyakazi hewa. Agizo hili lilitolewa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Bw. Idd Azzan.
Alisema
halmashauri hiyo imetumia fedha
hizo kuwalipa wafanyakazi hewa
na watu waliostaafu, jambo ambalo
ni kinyume cha sheria.
Alisema watu waliolipwa fedha
hizo watatakiwa kuzirudisha na
ikiwa watakaidi sheria itachukua
mkondo wake. Alisema kuwa
halmashauri hiyo inatakiwa
kuwabana ili wazirudishe pamoja
na kutoa mchanganuo unaoeleweka
juu ya fedha sh. milioni 119 ambazo
zilikuwa ni za ujenzi wa zahanati.
"Tunaomba maagizo yote
tuliyotoa yatekelezwe kwa muda
muafaka, lakini pia ikumbukwe
kwamba kamati imesikitishwa
kuona hoja zingine zimeshindwa
kupatiwa majibu yanayoeleweka,"
alisema.
Mwenyekiti huyo aliitaka
halmashauri hiyo kuwa makini
mara tu zinapotakiwa kuwasilisha
michanganuo inayoonesha utendaji
wao, kutoa ushirikiano kati ya
halmashauri ya Babati Mjini na
Vijijini.
Naye Mwenyekiti wa LAAT Bw.
Augustino Mrema, alitoa onyo kali
kwa halmashauri hiyo na kusema;
"Lazima makosa yao yatafutiwe
adhabu ya onyo la mdomo ili kuleta
tija" alisema.
Wakati huo huo,Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii imetakiwa
kupunguza matumizi ya fedha
kwenye semina, maonsho.
Hayo yalibainisha Dar es Salaam
jana na Makamu Mwenyekiti wa
Hesabu za Serikali Bi.Zainabu
Vullu,wakati wakupitia hesabu za
wizara hiyo.
Bi.Vullu alisema, sh. Bilion 1.9
zimetumika kinyume na bajeti
ikiwemo sh. milion 729 kutumika
kwenye sherehe za nane nane mjini
Dodoma. Alisema mbali na fedha
hizo pia Wizara ilichangisha kwa
Taasis mabalimbali sh. miloni
86.kwa ajili ya sherehe ya nane

2 comments:

  1. Aksante sana Mh. Azzan. Toboa siri ili sisi wananchi tuwapatieni data za jinsi fedha zinavyotafunwa na halmashauri yetu. Sisi wananchi ndio tulikutuma kupitia bunge letu.

    Kama ataudhkerwa mtu aende mahakamani au arudi kwetu wananchi tumsafishe kama atakuwa amechafuliwa jina.

    Usiwasikilize watu kama akina Mukama wa CCM wanaobeza Kamati yenu. Hakuna siri kwenye mambo yanayohusiana na wizi wa mali ya UMMA. chapa kazi utuzwe na UMMA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naungana nawe Wananchi wana haki ya kujulishwa mambo yao. (The Right to know) kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

      Delete