- Nassari tishio matokeo ya awali
- Helikopta yatumika kurinda kura
- CHADEMA yasinda udiwani
111. kwenye Kituo cha Leganga
CCM ilipata kura 26 na Chadema
26, Makumira CCM 22 na Chadema
118, Kituo B CCM 42 na Chadema
100, kituo C, CCM kura 50 na
Chadema 62 na Kituo D, CCM kura
40 na Chadema 68.
Kwa upande wa matokeo ya
Kituo cha Akheri ambapo CCM
ilipata 60 na Chadema 192, CCM
56 na Chadema 169. Katika Kijiji
cha Nduruma CCM 88 na Chadema
94. Kituo cha Ushirika CCM 115,
Chadema 70, Akere Shule CCM
250 na Chadema 46, Kituo B
CCM 263, Chadema 33, Kituo cha
Mbole Sambo CCM 181, Chadema
63 na kituo cha pili CCM 150 na
Chadema 61.
Katika kituo cha Mbolesambo
CCM 181, Chadema 63, kituo
kingine CCM 150 na Chadema 61,
kingine CCM 183 na Chadema 72.
Kwenye kituo cha Ulisambaseni
CCM kura 58, Chadema 84, kingine
CCM 140, Chadema 163, Mtingisi
CCM 100 Chadema 88, kingine
CCM 42, Chadema 101 na Sinai
CCM 64, Chadema 30.
Katika kituo kingine CCM 100,
Chadema 144, kituo kingine CCM
CCM 102 na Chadema, Kituo
Mlibalo CCM 34, Chadema 123.
Katika kituo cha Ndalesambi
CCM 51, Chadama 119, Kata
ya Mkwakirika Kituo CCM 62,
Chadema 88, Ushirika Njari CCM
102, Chadema 164, Kisangari CCM
53, Chadema 113, Makumula CCM
8, Chadema 42, Makiba CCM 87,
23.
Chadema yatumia helikopta
kulinda kura
Kwa mara ya kwanza katika
historia ya uchaguzi nchini, jana
Chadema ilitumia helikopta yake
ikiwa ni sehemu ya kurahisisha
ulinzi wa kulinda kura kwa
kuzungukia maeneo yote ya jimbo
hilo.
Stahili hiyo ya Chadema kulinda
kura kwa helikopta ilikuwa kivutio
cha aina yake kama ilivyokuwa
wakati wa kampeni, huku baadhi ya
watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa
CCM wakipinga hatua hiyo.
Hata vivyo malalamiko hayo
yalipingwa na baadhi ya viongozi
wa Chadema, ambao walisema
kutumia helikopta ni jambo la
kawaida kwa kuwa huo ndio uwezo
wao, kama ilivyo kwa vyama
vingine vinavyotumia magari
kuzungukia maeneo mbalimbali.
“Sisi kutumia helikopta ndiyo
uwezo wetu kama wengine
wanavyotumia magari,” alisikika
akisema mmoja wa viongozi wa
Chadema. Wengine walisema
helikopta hiyo kukata anga wakati
zoezi la kupiga kura likiendelea
kungesababisha kubadili watu na
kuamua kuipigia kura CCM.
Kwa mujibu wa taratibu za
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kinachokatazwa wakati wa kupiga
kura ni watu au magari kuwa na
sare za vyama.
Kwa msingi huo mmoja wa
maofisa wa NEC alisema hata
kama helikopta hiyo inatambulika
kuwa ni ya Chadema, hilo si kosa.
“Helikopta ni sawa na usafiri
mwingine, kwa hiyo hakuna makosa
yaliyofanyika,” alisema.
Kwa mujibu wa matokeo hayo
katika Kituo cha Rigurusi CCM
128, Chadema 82, Menyelini CCM
105, Chadema 58, Kituo B CCM,
101, Chadema 57, Sinai CCM 94,
Chadema 30, Kananase Shule ya
Msingi CCM 188, Chadema 66,
Ofisi ya Kata Igurusi CCM 160,
Chadema 76, Ofisi ya Mlawango
A, CCM 72, Chadema 121, Kituo
B, CCM 63, Chadema 120, Kituo
C, CCM 80 Chadema 106.
Sistone Shule ya Msingi Kituo
A, CCM 100, Chadema 59, B,
CCM 58, Chadema 55, C, CCM 76,
Chadema 44. Ofisi ya Kijiji Sistone
CCM 128, Chadema 82, Kata ua
Usa River Shule ya Msingi Msura
CCM 77, Chadema 79, Masura B,
CCM 74, Chadema 91, Moleve
Shule ya Msingi CCM 28, Chadema
176, Makumila CCM 50, Chadema
92, Shule ya Msingi Songa CCM
110, Chadema 86, Kijiji cha Ndulele
CCM 81, Chadema 94, Isanda A,
CCM 55, Chadema 118.
Kutoaminiana kwatawala
Kwa mujibu wa waandishi
wetu waliokuwa katika Jimbo la
Arumeru Mashariki kuna hali ya
kutoamini baina ya wafuasi wa
vyama vinavyoshiriki uchaguzi
huo, hasa vile vyenye upinzani
mkali vya CCM na Chadema.
Walisema hata pale gari lilipopita
eneo fulani kwa mwendo wa kasi,
kuliibuka hali ya hofu na mwingine
polisi kulazimika kufuatilia kwa
nyuma ili kujua kilichotokea.
Hata ulipofika wakati wa kula
chakula hali hiyo ya kutoaminiana
iliendelea, kwani wakati mwingine
wa s imami z i wa u c h a g u z i
walilazimika kufungua ‘hotpot’ ili
kuonesha kilichomo ndani ni nini.
Purukushani
Katika kituo kimoja kilichopo
katika Kata ya Majani ya Chai
zilitokea purukushani baada ya
kufika mwanamke mmoja na
kumwambia msimamizi wa kituo
hicho kuwa anataka kuzungumza na
wakala wa chama cha SAU.
Hata hivyo, alijibiwa kuwa
kwenye kituo hicho hakuna wakala
wa chama hicho, ndipo aliomba
aonane na wakala wa CCM na kisha
kuondoka.
Habari zieleza kuwa baadaye
alirudi na kundi la vijana waliovaa
kimasai na kuanza kuwarushia vijana
mawe waliokuwa wamesimama
umbali wa mita 100.
Kwa mujibu wa mashuhuda
vijana hao waliokuwa wamesimama
umbali wa mita 100 walianza kujibu
mapigo huku wakizidi kukusanyika
na kufanikiwa kuwazidi nguvu
vijana, hivyo kulazimika kupanda
gari na kukimbia. Hata hivyo
mwanamke aliyekuja nao alishindwa
kudandia gari, hivyo alikamatwa na
kuwekwa chini ya ulinzi.
Habari tulizopata wakati
tunaenda mitamboni zinaeleza
kuwa Chadema imeshinda udiwani
Kata ya Kirumba. Mgombea wa
Chadema Bw. Bahati Kauu alipata
kura zaidi ya 2,938 na yule wa
CCM Bw. Jack Robert (Masamaki
kura 2,121.
Imeandikwa na Willbroad
Mathias, David John, Dar, Queen
Lema na Pamela Mollel, Arumeru
na Daud Magesa, Mwanza.
Mi niliwambia kuwa Chadema itashinda tu maana chadema wanaomba Mungu aliye wa kweli,na wao wanatumia vyeo vyao na ufisadi.Na hii ni mwanzo tu napia ni dalili kuwa ccm kufikia 2015 hali itakuwa si shwari kutokana na watanzania kuchoshwa uongo wa chama tawala miaka 50 sasa.Si kwamba ccm na serikali haijafanya kitu wamefanya lakini mambo madogo madogo sana,mabo makubwa yanawashinda maana kila mtu ni mbinafsi.Akipewa uongozi anataka ale yeye ashibe,na anasahau wananchi.Sasa watanzania tumechoka na hali itakuwa mbaya zaidi ifikapo mwaka 2015,kama watabiri wa mabo ya siasa wasemavyo.Watanzania wa sasa si wa enzi zile watu wamechoshwa sana na serikali ya ccm.Rushwa kila kiongozi wa ccm,mahakama,polisi,uwanja wa ndege ofisi serikali za mitaa kata wilaya mikoa serikali kuu sasa tumwamini nani sisi raia.Bora tukubali mageuzi tuone hali itakuwaje.Ahsante watanzania kwa kuliona hilo na Mungu wetu ni mwema atasimamia raia wa tanzania na chama cha demokrasia-chadema.Mungu bariki Tanzania bariki chadema.
ReplyDeleteHelcopta, Helcopta. CHADEMA KUTUMIA HELKOPTA NI SOMO KWA SERIKALI YA TANZANIA NA NCHI NYINGINE ZA KIAFRIKA KATIKA KUFANYA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO NA ZA KIUCHUMI.
ReplyDeleteMIUONDO MBINU YA NCHI YETU YA TANZANIA NI MIBOVU NA SI YA KUAMINIKA KUTOKANA NA MAJANGA KAMA YA MAFURIKO, UBOVU WA BARABARA NA KUTOKUWAKO KWA BARABARA SEHEMU NYINGINE ZA NCHI, MAENEO YA NJAA N.K.
1)NI RAHISI MTENDAJI KURUKA KWA HELKOPTA ILI KWENDA KUFANYA KAZI ZA MAENDELEO AU UOKOAJI IKIWA DARAJA AU MITO IMEFURIKA AU MOTO UMELIPUKA MAHALI MAGARI HAYAWEZI KUTUMIKA.
2)NCHI YETU NI KUBWA SANA. KIONGOZI AKITUMIA GARI KWA MFANO KUTOKA DSM KWENDA TARIME KIKAZI, GHARAMA NI KUBWA ZAIDI KULIKO ANGETUMIA HELKOPTA. ANAWEZA KUFANYA KAZI KWENYE MAENEO MENGINE YA NJIA HIYO KAMA DODOMMA,SHINYANGA NK. ATAWEZA KUFIKA VIJIJINI KULIKO KUTUMIA GARI. AKIFIKA KWENYE MIJI MINGINE ANAWEZA KUTUMIA MAGARI YA MADC. MARC, N.K BADALA LA SHANGINGI LAKE KUTOKA DAR AMBALO HATA KWENDA VIJIJINI NI MBINDE. VIJIJINI NDIPO PENYE KAZI NA SIO MIJINI
3)ATAOKOA FEDHA ZA SERIKALI KWA UPANDE WA POSHO ZA MALAZI KWA KUWA ATATUMIA MUDA MFUPI WA SAFARI MUDA MFUPI KWA KUTUMIA HELKOPTA.
MPANGO HUU UTAWEZEKANA TU IKIWA KUNA SERIKALI INAYOONGOZWA NA CHAMA CHENYE HURUMA NA KUWAJALI WANANCHI WAKE. WANAOPIGANIA POSHO HAWAWEZI KUFIKIRIA KUTUMIA HELKOPTA. VIONGOZI WALIO WAVIVU NA WASIO WACHAPA KAZI HAWAWEZI KUBUNI KITU KAMA HIKI. WATABAKI WAKISEMA NI GHARAMA KUBWA NA MANENO MENGI YA KEJELI. BADALA YAKE WATUMIE KALAMU WALINGANISHE GHARAMA. VYUO VIKUU VINA WATAALAM WENGI TU WAPEWA KAZI WAPIGE HESABU. ISIWE NI KAZI YA KUWAPONDA HAWA WATAALAM WETU.
ANGALIENI MATUNDA YALIYOPATIKANA KUTOKANANA CDM KUTUMIA KOPTA ARUMERU.
NATAMANI CDM IINGIE MADARAKANI INUNUE KOPTA NYINGI TU BADALA YA KUNUNUA ZILE NDEGE ZA KINA MRAMBA AMBAZO TULIKULA MAJANI NA TUNAENDELEA KUYALA. UTAALAM NA BUSARA ZIKITUMIKA. MTINDO WA "OUTSOURCING" KAMA KWENYE KUKODI MAGARI, KOPTA HIZO ZITADUMU NA KUENDESHWA KWA UFANISI. MAGARI YA SERIKALI YATAENDELEA KUFA,WIZI WA SPEA NA MAFUTA UTAENDELEA N.K
MAFANKIO YA MPANGO HUU NI KUWA NA ZERO TOLERANCE YA UFISADI. KURA NDIZO ZITAKAZOTOKOMEZA UFISADI NA SIO MAMBO YA KUONDOA MAGAMBA. VYAMA, IKIWAMO CCM ITUMIE NGUVU ZA KURA ZA WANANCHI KUUONDOA UFISADI. WANANCHI WAHAMASISHWE WATUMIE KURA KAMA NJIA YA KUTOKOMEZA MAFISADI.
NGUVU YA KURA HIZI NDIO IMERUDISHA ARDHI AMBAYO ILIKUWA IMENYANGANYWA WANANCHI HUKO NDURUMA NA MOSHONO. KAMA SIO TISHIO LA KUNYIMWA KURA,ARDHI HII HAINGEPATIKANA. ARDHI HIYO NDIYO ITAKAYOLETA MAENDELEO KWA BAADHI YA WANAARUMERU.