NEW YORK,Marekani
MAMA wa mwanamuziki wa zamani, Whitney Houston amevunja ukimya kuhusu kifo cha mwanaye, baada ya kusema kwamba alifanya kila liwezekanalo ili kumnusuru mwanaye aondokane na matumizi ya dawa za kulevya.
Tangu kitokee kifo hicho, Cissy Houston, 78, amekuwa akikataa kuzungumza adharani kuhusu kifo cha mwanamuzi huyo ambaye alikutwa amekufa bafuni Februari, mwaka huu kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya,
Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la TheSun, akizungumza katika Kanisa la Hope Baptist lililopo eneo la Newark mjini New Jersey, ambapo mazishi ya Whitney yalifanyika, mwana mama huyo alisema kwamba alikuwa na matumani ya kwamba angemrejesha katika hali yake ya kawaida.
Akionekana mwenye majonzi Cissy alisema : "Hakuna kitu ambacho anaweza kukifanya juu ya jambo hilo na hakuna mtu yoyote anaweza kufanya chochote juu jambo hilo."
Mwanamama huyo ambaye ni muimbaji wa muziki wa Injili na ambaye alisema kwamba alikuwa akimshauri kufuata nyayo zake za kuimba nyimbo za dini, alisema kuwa anafahamu alifanya vizuri na hivyo hawezi kujilaumu.
"Alikuwa ni maalum sana kwangu. Nilikuwa na jeuri na binti yangu. Yeye ametimiza yote katika muda mfupi ambao amekuwa hapa, alikuwa mtu wa maajabu,"alisema.
Wachunguzi mjini Los Angeles, wanasema kwamba mwimbaji huyo alikuwa na matataizo ya moyo wakati alipobwia dawa hizo aina ya cocaine.
No comments:
Post a Comment