17 April 2012

Bayern Munich uso kwa uso na Real Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (katikati) akizunguka uwanja na wachezaji wenzake katika mazoezi yaliyofanyika jana kujiandaa na mechi ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, dhidi ya Bayern Munich itakayofanyika leo katika Uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani. (AFP)

MUNICH, Ujerumani
MICHUANO ya Klabu Bingwa Ulaya, inaendelea kutimua vumbi baadaye leo hii kwa kuikutanisha miamba miwili Bayern Munich itakayokuwa ikiikaribisha Real Madrid, kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika mechi ya kwanza ya hatua ya nusu fainali ya kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza Reuters, mabingwa hao wa Ujerumani watashuka uwanjani wakiwa na dhamira moja ya kuondoka na ushindi baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi za ligi ya nyumbani, baada ya kuambulia kipigo cha bao  1-0 kutoka kwa Borussia Dortmund.

Pia timu hiyo ilipata suluhu na timu ya Mainz ambapo imeshuhudiwa timu hiyo ikiongeza pengo la pointi nane, dhidi ya vinara wa ligi hiyo Dortmund katika michuano ya ligi ya Bundesliga.

Inaelezwa kwamba licha ya timu hiyo kuonekana kuimarika kila idara, lakini inaelezwa kuwa matokeo hayo yanaonekana kuwa mabaya kwa kikosi hicho cha Jupp Heynckes.

Ikiwa na wachezaji kama Mario Gomez, Franck Ribery ana Arjen Robben, kikosi hicho kinadaiwa huenda kikaisumbua ngome ya Real Madrid wakati mchezaji Bastian Schweinsteiger, akiendelea kujaribu kujiweka sawa baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na matatizo ya bega.

Huku mchezaji Jerome Boateng, akiongeza nguvu na kipa Manuel Neuer, akiwa mmoja wa  walinda mlango bora duninai kikosi hicho cha kocha  Heynckes kinadaiwa kuwa huenda kikachanganyikiwa baada ya kushuhudia kiungo wake David Alaba, akiikosa mechi hiyo baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi ya marudiano ya robo fainali dhidi ya timu ya  Marseille.

Vinara hao wa Ujerumani wanalezewa kuwa watashuka uwanjani kwa lengo la kuiangamiza  Real Madrid, ambayo hajawahi kufungwa tangu Januari 18 mwaka huu ilipofungwa na  Barcelona.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho, kinatarajia mashambulizi yake kuongozwa na Cristiano Ronaldo, ambaye ana uhakika atakuwa mwiba  kwa Wajerumani hao baada ya kufunga mabao 53 katika mashindano yote msimu huu.

Jumapili Real Madrid ilifikisha rekodi ya kufunga mabao 107 msimu mmoja katika michuano ya Ligi ya La Liga, ambayo ilikuwa  ikishikiliwa na mchezaji John Toshack tangu mwaka 1989/90 baada ya kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Sporting Gijon.

Katika kikosi hicho  Ronaldo amekuwa akisaidiwa na Mfaransa Karim Benzema na mshambuliaji mwingine raia wa Argentina, Gonzalo Higuain  anadaiwa kuwa mwiba mwingine ambaoa umekuwaukitumiwa na Real Madrid msimu huu kuwanyoosha wapinzani wao.


Mbali na wachezaji haoa nyota wa Brazil,  Kaka naye kwa sasa anafurahia kurejea kwenye kiuwango chake  na kikosi hicho cha  Mourinho kinadaiwa kitasafari kwenda Ujerumani kikiwa kifua mbele baada ya kiungo wake  Xabi Alonso  kurejea uwanjani  baada ya kumaliza kifungo chake.



Mtanange huo unadaiwa kuwa wa aina yake kwa  Heynckes, ambayoiliizuia Rea Madrid kutwaa ubingwawamichuano hiyo katika msimu wa 1997/98  kwakuichapa  Juventus 1-0  mjini  Amsterdam.

Michguano hiyo inatarajia kuendelea  kesho ambapo Chelsea itakuwa ikiumana na Barecelona kwenye uwanja wa Stamford Blidge.

No comments:

Post a Comment