17 April 2012

Dkt. Bilal atoa changamoto kwa Watanzania

Na Pamela Mollel, Arusha
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Ta n z a n i a Dkt. Mohamed Gharib Bilal amewataka wananchi, wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara jijini Arusha kutumia huduma za Benki ya ABC ili kuboresha maisha yao.
Mwito huo aliutoa jana jijini
hapa wakati akifungua tawi
jipya la benki hiyo katika eneo
la Bondeni Mtaa wa Swahili
huku akisisitiza iwapo kila
mmoja atatumia furasa ya
benki hizo anaweza kupiga
hatua kiuchumi.
A l i s e m a k u w a ,
amefurahishwa kwa kuwepo
kwa huduma nyingi katika
benki hiyo ambapo alitaja
huduma hizo kuwa unapotaka
kufungua akaunti ya akiba
unahitaji kiwango cha sh.
5,000 tu jambo ambalo
litasaidia hata watu wa kipato
cha chini kufungua akaunti
katika benki hiyo.
Pamoja na huduma hiyo
pia Bw. Bilal alifurahishwa
na mtazamo wa benki hiyo
kuanza kutoa mikopo ya
nyumba ambapo alisema
itasaidia Mtanzania katika
kuboresha makazi yake.
Aidha aliwataka Watanzania
kwa ujumla kujenga utamaduni
wa kuzitumia benki zilizopo
nchini si tu kwa kuweka akiba
bali kutumia huduma zake
kama nyenzo ya kupata na
kukuza mitaji ya kujiendeleza
kibiashara.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa benki hiyo Tanzania Bw.
Borniface Nyoni alisema
ufunguzi wa Tawi la Arusha
ni hatua katika ukuaji kufikia
maeneo mengi hapa nchini
ambapo ushindani katika
sekta ya huduma za kifedha
ni mkubwa na unazidi kuwa
mkubwa kutokana na taasisi
nyingi za kifedha kuingia
kutokana na mazingira mazuri
ya soko na fursa tele zilizopo
nchini.
Wakati huo huo Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Bw.
Magesa Mulongo amesema
kuwa amefarijika sana kuona
Makamu wa Rais kuja kwenye
uzinduzi wa Benki hiyo huku
akitoa changamoto kwa benki
hiyo kuwa, Arusha kuna
ushindani mkubwa wa kibenki
ambapo hadi sasa kuna benki
19 kwa Mkoa wa Arusha.
Bw. Mulongo alisema
kuwa, Arusha kuna amani
ya kutosha hivyo watu
mbalimbali wasiogope kuja
kuwekeza katika jiji hilo kwa
kuwa tarehe 29 mwezi wa
5 hadi tarehe 2 mwezi wa 6
mwaka huu kutakuwepo na
mkutano mkubwa wa Benki
wa Maendeleo ya Afrika
ambapo Marais 10 wa nchi za
Afrika watahudhuria mkutano
huo.

No comments:

Post a Comment