05 April 2012

Polisi Dar wakamata dawa za kulevya za bilioni 1.4/-

Radhia Ramadhani na Joyce Kambota
WATU wanne raia wa Nigeria wamekamatwa na madawa ya kulevya aina ya HEROINE yenye thamani ya shilingi bilioni 1 .4 za kitanzania jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar e Salaam jana, Kamanda wa Polisi  kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam Bw. Suleiman Kova alisema watuhumiwa wa kesi hiyo sio watanzania ni  wanaigeria waishio maeneo ya Tabata kinyerezi kibaga.

" Tukio hilo limekuwa la ajabu sana kwani hatujawahi kukamata dawa za aina hiyo zilizokuja kwa dizaini ya pakti za chumvi tena zimekaushwa" alisema Kamanda Kova.

Watuhumiwa hao waliotambulika kama Bw.Ifeanyi     Oko(33),Bw.Uchendu Jerry(35),Bw.Ugwu Valentine(31) na Bi. Ani Lawretta(27)mbali na kukamatwa na paketi nne pia wamekutwa na kete 12 za madawa zilizokuwa tayari kwa kumezwa.

Kamanda Kova aliongeza kuwa hadi sasa nchini kumekuwa na mtandao wa madawa ya kulevya kutoka nchi za nje hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuwafichua watu ambao wana mashaka nao.

Wakati huohuo Kamanda Kova alisema walifanikiwa kuwakamata waalifu Sugu (84) kwa tuhuma mbalimbali kufuatia misako inayoendelea ili kuhakikisha hali ya jiji la Dar es Salaam ni tulivu.

"Miongoni mwa vitu ambavyo tunaweza kujivunia jeshi la polisi ni pamoja na juhudi zilizofanywa na kikosi maalum wakishirikiana na ulinzi shirikishi kwa kufanya dolia na kuwakamata waarifu hao"alisema Kova.

Baadhi ya watuhumiwa hao ni Bw.Rashid Seif(25),Bi.Habiba Juma(22),Bw.Ramadhan Suleiman(30),Bw.Shaban Adam(33),Bw.Salehe Omary(17)na wengine79.

No comments:

Post a Comment