Na Peter Mwenda
MEYA wa Bukoba, Bw. Aman
Anatory, amesema fani ya ununuzi
na ugavi ina jukumu kubwa katika
uchumi kwa vile inahusika moja
kwa moja katika kuinua uchumi.
Akizungumza katika mahafali ya tisa ya
Chuo cha Ununuzi na Ugavi (IPS), kilichopo
Chanika Dar es Salaam juzi, Meya Aman
alisema fani ya ugavi na ununuzi ndiyo
inasimamia matumizi mazuri ya fedha za
walipa kodi.
“Fani ya ununuzi na ugavi ni muhimu katika
kukuza uchumi wa nchi yoyote duniani,asilimia
kubwa ya fedha za walipa kodi hutumika katika
manunuzi ya mipango ya maendeleo ya nchi,”
alisema Meya Aman.
Alisema ni jukumu la wahitimu kudhihirishia
waajiri kuwa ujuzi waliopata katika kozi hizo
ni kwa ajili ya kuongeza ufanisi ili kunusuru
fedha za umma zisiingie mifukoni mwa
watu.
Awali Mkuu wa Chuo cha IPS, Bw. Leonard
Lyatuu, alisema chuo hicho tangu kianze mwaka
2002 kimekuwa kikitoa kozi mbalimbali za
ugavi na ununuzi nchini.
Alisema mwaka 2003, IPS walikubalika
na Chuo cha CIPS (UK) cha Uingereza
kinachosimamia mafunzo na mitihani ya
Shahada ya Juu ya Ununuzi,Shahada ya
Ununuzi na kinasubiri tamko la NACTE
kukamilisha mitaala ya Shahada ya Ununuzi na
Ugavi. Alisema mpaka sasa Chuo cha IPS kina
wanafunzi 354 wa kozi za ugavi na ununuzi.
No comments:
Post a Comment