17 April 2012

Nauli za daladala Dar kupanda tena, maombi 'yatinga' SUMATRA

Na Heri Shaaban
CHAMA cha Wamiliki wa Daladala MKoa wa Dar es SAlaam (DACOBOA)wamepeleka maombi yao Mamlaka ya Udhibiti Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kwa ajili ya kuongeza bei mpya ya nauli za daladala.
Maombi hayo ya kuongeza bei ya nauli mpya yametokana na madai ya wamiliki wa daladala Dar es Salaam kwamba  gharama za uendeshaji zimepanda.

Akizungumza Dar es Salaam jana,Mwenyekiti wa DACOBOA Bw.Sabri Mabrok alisema kuwa wamepeleka maombi hayo SUMATRA ili yaweze kufanyiwa kazi.

"Mapendekezo ya bei mpya tumeshakabidhi kwa SUMATRA tunasubiria hatua za utekelezaji kwa sababu na bei za vifaa pamoja  na gharama zingine za uendeshaji zipo juu sana kwa sasa."alisema Bw.Mabrok.

Alielezea bei za uendeshaji zilivyokuwa kwa  mwaka 1995 ambapo ziko tofauti na za sasa.

Alisema  bei ya mafuta lita moja ilikuwa ikiuzwa sh.385 na bei ya nauli ya daladala sh. 150 na kwa upande wa dola moja ilikuwa sh.1600, lakini sasa hivi bei ya lita moja sh. 2200 wakati dola moja inauzwa kwa sh.1900.

Kwa upande wa bei ya  taili moja shilingi 400,000 na bei ya betri la gari 150,000 ambapo mwaka 1995 betri la gari lilikuwa likiuzwa kwa sh.70,000.

Alisema kuwa sababu kuu za kuomba kupandisha gharama za nauli  ni kutokana na mbiundombinu kuwa mibovu na sababu hizo hapo juu,pamoja na  kuharibika kwa magari yao ambapo asilimia 100 ya daladala  na vituo vyote vibovu pia.

"Tumeshindwa kupandisha bei kiholela ya daladala kutokana na  daladala azipo katika biashara huria ndio maana tumefuata sheria kupitia ngazi husika atuna mamlaka ya kupandisha bei tofauti biashara nyingine za mmiliki kuamka asubuhi na kutoa bei ya bidhaa yake.

5 comments:

  1. Wwe Bw.Mabrok hiyo dola 1 inyouzwa Tshs.1900/= iko wapi? Tunaomba utuonyeshe ilo duka la kubadili fedha. kwa sasa dola moja ya kimarekani huzwa kati ya Tshs. 1570/= hadi 1630/= Bw.Mabrok, hebu acha upumbavu wa kufikili watanzania ni miaka ya sabini.

    Uhsaur: Fanya mambo yako kwaufasaha, na kama upo ulazima utafanikisha tu azima yako.

    ReplyDelete
  2. Ifike mahali Mamlaka zilizopewa majukumu ya kusimami bei halali za huduma nchini ziwe ni za haki na zinazingatia hali ya kipato cha chini. Watu kuendelea kuona gharama mbalimbali zikiongezeka bila kipato chao kutiliwa maanani kama vile umeme, maji na usafiri kwa kutaja huduma chache tu ni kutowatendea raia wa kipato cha chini si haki.
    Katika kufanya biashara lazima kuzingatia kuna FAIDA na HASARA. Kama mtu anaona hapati faida kwa kufanya biashara yoyote ile kama ya usafirishaji wa abiria aamue kujiondoa kwenye biashara hiyo.
    Serikali inarakishe utaratibu wa kutumia njia mbadala ya kusafirisha abiria mijini na vijijini kama ilivyo katika nchi nyingineao wana usafiri wa reli, majini, anga na mabasi makubwa na si mabasi madogo kama ilivyo hapa kwetu yanayomilikiwa na watu binafsi wenye lengo la kupata faida kwenye migongo ya wananchi wasio na uwezo.
    Ni wakati muafaka kuwa na chombo cha kutetea haki/maslahi ya wananchi ambao vipato vyao vimedidimia na kusababisha waishi maisha ya kubabaisha na mateso mkubwa mno.

    ReplyDelete
  3. Bwana Mabrouk, hizo tairi unanunua kila siku pamoja na battery? Usilale na kuamka then ufikiri kupandisha bei, hiyo dola inayouzwa 1900 umeiona wapi na duka gani? Mabrouk eee, acha usanii bwana. SUMATRA kuweni makini na huyu jamaa

    ReplyDelete
  4. SUMATRA, Mmsiwe wavivu wa kutenda kazi. Mkiambiwa chochote na akina Mabrok, fanyeni utafiti. Mnaweza kutumia daladala yenu kujua kama wamiliki wa daladala wanapata faida ama hapana. Mnaweza hata kutumia baadhi ya madereva kuwapa data za marejesho ya kila siku kwa mabosi wao.

    Naona sisi wasafiri wanyonge mtuonee huruma. Hata siku moja mwajiri wetu hajatumia kigezo cha dola au ongezeko la bei ya vyakula kutkuamua kutuongezea mishahara. Labda mtuombee kwa Serikali ili tuongezewe mishahara.

    Kama wenye magari wanavyonunua tairi au petroli, na sisi wananchi tunanunua sukari, maziwa,mahindi n.k ambavyo vyote hivi vinapanda bei kila kukicha.

    Wengine hatuna ajira tunatumia magari haya haya kutafuta kazi.

    Tutaua watoto kwa njaa kutokana na nia yenu ya kutaka kupandisha nauli.

    Wewe Mabrok sio BROKE kwa hiyo tuonee huruma.

    ReplyDelete
  5. Maoni,
    Tunaomba Serikali yetu itufikirie sisi watanzania wa hali ya chini.
    pia tunaomba iwapunguzie kodi wamiliki wa mabasi ya dalala pia waharakishe usafiri wetu wa mabasi ya mwendo kasi.
    Maisha yamepanda sana ila mshahara bado ni Ule ule.

    ReplyDelete