Na Anneth Kagenda
WATANZANIA wametakiwa kuondokana na fikra potofu kuwa mtu akitoa damu anapata matatizo ya kiafya, badala yake washiriki kikamilifu katika kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wajawazito wakati wa
kujifungua na ifike mahali vifo hivyo vipungue.
Hayo yalisemwa Dar es
Salaam juzi na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete,
wakati wa uzinduzi wa
Kampeini ya Uhamasishaji
Taifa wa kuchangia damu
salama ili kuokoa maisha
ya wajawazito maarufu
kama Saidia Mama Mjamzito
Ajifungue Salama.
K a m p e i n i h i y o
imeandaliwa na vijana
wa Taasisi ya Madaktari
Wahitimu wa Vyuo Vikuu
Tanzania (THPI) .
Mama Salma ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo
( WA M A ) , a l i s e m a
kumekuwepo na upotoshaji
mkubwa kwa Watanzania
wengi kuwa mtu anapoenda
kutoa damu anapata matatizo,
huku wengine wakitishwa
kuwa watagundulika na
magonjwa.
“Dunia ya leo Mtanzania
yeyote asiogope kukutwa
na ugonjwa dawa zipo
hospitalini mtapewa na
kuzitumia hivyo jitokezeni
kwa wingi mpime na mtoe
damu kwa ajili ya kuwasaidia
wajawazito na kujua afya
zenu, kwani bila mama
kiumbe hakiwewezi kuja
duniani,” alisema Mama
Salma.
Alisema jukumu la kutoa
damu si la akina mama
tu bali hata akina baba na
vijana wanatakiwa kushiriki
kikamilifu katika kuchangia
damu ili kuondokana na tatizo
la akina mama kufa kabla na
baada ya kujifungu.
Alisema takwimu za kitaifa
za vifo vya akina mama
wajawazito vilikuwa 529
kati ya 100,000 kwa mwaka
1999, 578 kwa 100,000 kwa
mwaka 2005. Kwa mujibu
wa Mama Salma vifo hivyo
vimepungua hadi 454 kati ya
100,000.
Alisema taifa lina uwezo
wa kukusanya chupa za damu
95,000 hadi 112,000 kwa
mwaka wakati mahitaji ni
350,000 hadi 400,000 kwa
kipindi hicho hicho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa THPI Dkt. Telesphory
Kyaruzi, alisema lengo kuu
la kuanzisha kampeini hiyo
ni kuhamasisha uboreshaji
huduma za afya nchini na
kushiriki kikamilifu katika
kutoa huduma bora za afya
kwa Watanzania pamoja na
kutatua matatizo ya afya ya
jamii ya wakati huu.
MAMA SALMA NAKUPA HONGERA KWA SHUGHULI ZAKO ZA KUSAIDIA JAMII LAKINI CHONDE CHONDE USIJE UKAWA KAMA MAMA MKAPA NA "FURSA SAWA" EQUAL OPPORTUNITY FOR ALL TRUST. JARIBU KUWA KARIBU NA YEYE UMUULIZE ALIAMBIE TAIFA MALI YAKIWAPO MAJENGO NA FEDHA ALIZO KUSANYA KAMA MSAADA ZIKO WAPI? WANACHAMA WAKE WAKO WAPI AU ALIWAACHA YATIMA BAADA YA MUME KUACHA AUONGOZI?
ReplyDelete