17 April 2012

Muleba wapitisha bajeti bilioni 41.1/-

BAADA ya majadiliano ya siku mbili ya bajeti ya halmashauri hatimaye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera limepitisha bajeti hiyo ya mwaka 2012/13 ambayo inakadiriwa kufikia zaidi ya sh. bilioni 41.1 zitakazokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa juzi na
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Bw. George
Katomero iliridhiwa na baraza baada ya
kujadiliwa kwa siku mbili na hivyo kutoa
nafasi ya kuifanyia marekebisho katika
masuala kadhaa ikiwemo matumizi ya mapato
yanayotokana na vyanzo vya ndani.
Awali akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo
Bw. Katomero alisema kati ya fedha hizo
zinazotarajiwa kukusanywa zaidi ya bilioni 3.2
zinatokana na vyanzo vya ndani huku nyingine
zikitarajiwa kupatikana kupitia ruzuku ya
Serikali Kuu na wahisani.
Hata hivyo madiwani hao wamekubaliana
kwamba kiasi cha shilingi bilioni moja zitumike
katika miradi ya maendeleo badala ya milioni
527.1 zilizotengwa awali kwa miradi lengo
likiwa kuboresha maisha wa wakazi wa wilaya
hiyo.
Mmoja wa madiwani hao Bw.Justus Magongo
wa kata ya Muhutwe alisema hakuna sababu ya
halmashauri kutegemea kwa kiasi kikubwa
fedha za ruzuku zinazotewa na serikali kuu kwa
madai kuwa sio za uhakika katika upatikanaji
wake, na kuwa wakati mwingine uletwa kwa
kuchelewa.
Aidha madiwani hao waliitaka halmashauri
kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato
ili kufikia lengo hasa kutokana na bajeti ya
mwaka huu kuwa na ongezeko la takribani
shilingi bilioni 15 kutoka bilioni 26.24 kwa
mwaka 2011/12 hadi kufikia bilioni 41.12
mwaka 2012/13.

No comments:

Post a Comment