02 April 2012

Wajumbe wamkataa Katibu wa CCM

Na Patrick Mabula, Shinyanga
HALMASHAURI Kuu ya
Chama cha Mapinduzi
(CCM) Wi l a y a y a
K a h a m a m k o a n i
Shinyanga imemkataa Katibu wa
CCM wilayani humo Bi. Magreth
Chusi kwa kile walichodai anatumia
vibaya madaraka yake.

Kwa mujibu wa taarifa za
awali kutoka ndani ya kikao cha
halmashauri hiyo kilichoketi
mwishoni mwa wiki zilidai kuwa,
viongozi na wajumbe wake
walimkataa Katibu huyo na kutaka
aondolewe huku wakishinikiza
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga
aondoke naye.
Wakichangia hoja mbalimbali
baadhi ya wajumbe wa halmasahauri
hiyo ya Wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga iliyokuwa imehudhuriwa
na Katibu wa CCM Mkoa wa
Shinyanga Bw. Adamu Ngarawa
walimwambia hawamtaki Katibu
huyo kwa hiyo aondoke naye.
Bw. Paschal Ntale ambaye
alikuwa mmoja wa wajumbe hao
alikitaka Chama cha Mapinduzi
kumuondoa Bi. Chusi kwa madai
amekuwa akitumia madaraka yake
vibaya hasa kwa kutosikiliza kero
za wanachama wanapokuwa na
shida mbalimbali za kiuongozi.
Alisema, tangu aingie katika
nafasi hiyo wilayani humo (Katibu)
amekuwa na utaratibu mgumu ya
kumuona na kufanya viongozi na
wanachama wa CCM kujikuta
wanakuwa katika wakati mgumu
kwa nyadhifa zao za uongozi ndani
ya chama hasa walioko kwenye kata
na matawi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Umoja wa Wanawake wa chama
hicho (UWT) Wilaya ya Kahama Bi.
Aoko Nyangusu alisema hawamtaki
huyo Katibu.
“Hatumtaki huyu Katibu kwa
vile katika kutekeleza majukumu
yake, baadhi ya mambo amekuwa
akikiuka na tunapotaka kumuoya
amekuwa hataki na hatusikilizi,”
alidai.
Bi. Nyangusu alisema, amekuwa
akifukuza viongozi wa CCM wa
ngazi za chini katika kata na matawi
bila kufuata taratibu na kanuni
zilizomuwekwa katika madaraka
hayo kitendo ambacho kinaenda
kinyume na Katiba ya Chama cha
Mapinduzi.
Kufuatia kauli mbalimbali
za viongozi na wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya Wilaya ya
Kahama wajumbe hao walitaka
baada ya kikao Katibu huyo awe
ameondoka na Katibu wa CCM wa
Mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wake Katibu wa
CCM Mkoa wa Shinyanga Bw.
Adam Ngarawa alipoulizwa juu
ya kutokea kwa hali hiyo baada
ya kikao alikiri kukataliwa kwa
Katibu huyo na kusema uamuzi
ambao wajumbe hao waliutumia ni
kinyume cha utaratibu wa chama.
Bw. Ngarawa alisema wajumbe
hao walitakiwa tuhuma hizo
kuzipeleka katika Kamati ya Siasa
ya Wilaya ya Kahama zijadiliwe na
baadaye ndiyo ziwasilishwe kwenye
ngazi ya uongozi wa mkoa kwa
maamuzi na huo ndiyo utaratibu
wa CCM.
“Ni kweli Katibu wa CCM wa
Wilaya ya Kahama wamemkata,
wakimtuhumu tuhuma mbalimbali,
lakini wamekwenda kinyume
na taratibu za chama kwa hiyo
niliwakatalia kuondoka naye...
wanapaswa kufuata kanuni za
chama na kisha watuletee hayo
malalamiko sisi viongozi ngazi ya
mkoa kwa hatua zaidi,” alisema

1 comment: