Na David John
WAANDISHI wa Afya
Radio ya Mwanza,
walioshinda Tuzo
za Umahiri Katika
Uandishi wa Habari Tanzania
(EJAT 2011) jana wametoboa siri
za ushindi wao.
Waandishi hao, Bw. Noel
Thomson na Bi.Cecilia Ndapigeze,
ambao wameshindi Tuzo ya EJAT-
2011, katika masuala ya Utalawa
Bora na Afya, walitoboa siri hiyo
katika mkutano wao na waandishi
wa habari jana Dar es Salaam.
Sherehe za utoaji a Tuzo za
EJAT-2011, zinazoratibiwa na
Baraza la Habari Tanzania (MCT),
zilifanyika Ijumaa iliyopita, ambapo
mgeni Rasmi alikuwa Rais Jakaya
Kikwete.
Kwa upande wake, Bw. Thomson
alisema kufanya kazi kwa bidii,
kudhamiria na uwajibikaji, ndio
vitu vilivyoinua kiwango chake
cha uandishi na hata kupata tuzo
ya EJAT katika masuala ya Utawala
Bora.
"Kwa kweli, nilifanya kazi,
hata kutengeneza kazi hii (radio
documentary), ambayo imekubaliwa
na waandishi wakongwe na
waliobobea katika uandishi wa
habari‚ mbali na kufanya kazi, pia
nilidhamiria kupata tuzo kama hii,"
alisema, Bw. Thomson, ambaye
zawadi yake ilikabidhiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania
Media Fund (TMF), Ernest
Sungura.
Aliongeza kuwa uwajibikaji
ni moja ni vitu vilivyomchochea
kutengeneza documentary, ambayo
itasaidia kuwakwamua Watanzania
kutoka katika matatizo mbalimbali
ya kijamii, kiuchumi, kiafya na
mengineyo.
“Na hili limenifanya kuamini
kuwa kama kila mtu (waandishi
wa habari, wafanyakazi wa afya,
madiwani, wabunge, wafanyakazi
wa Serikali) watawajibika ipasavyo,
nchi yetu itapiga hatua kubwa
huduma za afya zitaboreshwa,”
alisema.
Naye Bi. Ndapigeze, aliyenyakua
Tuzo ya EJAT-2011, katika masuala
ya Afya (radio), ametaja ubunifu
binafsi, uongozo mzuri wa Afya
Radio na ushirikiano kazini, kama
vigezo vya msingi vilivyomsaidia
kupata ushindi.
Bi. Ndapigeze alikabidhiwa
tuzo hiyo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali ya Taifa Muhimbuli
(MNH), Dtk. Marina Njelekela.
"Ni kweli ubunifu binafsi
umechangia, lakini mamenaja wa
Radio pia wamenisadia sana…ni
mameneja kweli wanaojua kuwatia
moyo na kuongoza walio chini yao,
“ alisema na kuongeza kuwa;
“Ushirikano tulionao katika
(Afya Radio) pia umenisaidia
kutengeneza documentary nzuri,
iliyonipatia ushindi."
No comments:
Post a Comment