Na Stephano Samo, Manyara
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vurugu kubwa zimezuka kwenye mashamba ya ngano baina ya wafugaji wa Kijiji cha Gidagamuoda Kata ya Mogitu Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na wakulima wakubwa.Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wafugaji wa Kata ya Mogitu jana walidai kuwa vurugu hizo zilianza juzi baada ya wakulima hao kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji unaofanywa na wakulima wakubwa.
Walisema, wakulima hao walikuta
mtoto wa wafugaji hao akichunga
mifugo kandokando ya mashamba
na kumkamata kisha kumfungia
dani ya nyumba zao ndipo wafugaji
hao wakapata taarifa ya tukio hilo
na kuamua kuchukua hatua.
Walisema kuwa katika vurugu
hizo silaha za jadi zilitumika
ikiwemo mikuki, sime na mapanga
ambapo wafugaji hao walimkata
na mapanga mmoja wa wakulima
hao na kumjeruhi vibaya na
kumsababishia maumivu makali
hivyo kupelekwa Hospitali ya
Tumaini wilayani humo kwa ajili
ya matibabu.
Walidai kuwa wakulima hao
wakubwa ambao ni Watanzania
wenye asili ya kiasia eneo hilo lenye
zaidi ya hekari 40,000 wamekuwa
wakiyatumia mashamba hayo kwa
ajili ya kuzalishia zao la ngano.
Akizungumzia hali hiyo
Mbunge wa Jimbo la Hanang,
Dkt. Mary Nagu alisema hawezi
kuvumilia tena kuona wawekezaji
wakijichukulia sheria mikononi
kwa kuwa kuna njia za kufuata ili
kuepusha migogoro kama hiyo.
" H a w a W a h i n d i
wanatunyanyasa...sana, kwa
kutumia fedha zao wanatufanya
tuwe watumwa kwenye ardhi yetu,
yaani mifugo yetu haina thamani
kabisa hawataki iwepo wakati
ndiyo tegemeo letu," walisema.
Alisema kuwa, wakulima
h a o wa k u bwa wame k uwa
wakiwanyanyasa wafugaji hao
kwa kukamata mifugo yao kila
wakati na pia kuwafikisha Kituo
cha Polisi Katesh hasa vijana pindi
mifugo ikiwa inakamatwa inalishwa
pembeni ya mashamba hayo.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya
hiyo, Kapteni Mstaafu Winfrid
Ligubi akizungumza na mwandishi
wa habari hizi kwa njia ya simu jana
alidai kuwa magazeti yamekuwa
yakiandika habari za vurugu badala
ya kuandika maendeleo.
Ninyi kazi yenu ni kusubiri
vurugu zitokee na kuandika habari
mbona mambo mengi ya maendeleo
yakifanyika huwa hamuandiki,
mnasubiri wahuni wawapigie simu
na kuwajulisha vurugu zimetokea
ndipo mnaandika, alisema Ligubi
na kuongeza;
Kwa nini hampendi kuandika
mambo ya msingi mnabaki
kuandika mambo ya vurugu tu kila
mara vurugu tu, mnapenda haya
nendeni wenyewe mkaangalie
hayo mashamba mimi sisemi
chochote,alidai.
Hata hivyo Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoani Manyara, Eurelia
Msindai alidai kuwa bado hajapata
taarifa yeyote kuhusiana na tukio
hilo la vurugu kwenye Kijiji cha
Gidagamuoda Kata ya Mogitu.
Aidha, wakulima hao wa
Kampuni ya Ngano kutoka nchini
Kenya kwa sasa wanadaiwa
kuyakimbia makazi yao ambayo
yalikuwa karibu na mashamba
hayo na kuhamia karibu na mji wa
Katesh ili kuepuka kushambuliwa
na wafugaji.
No comments:
Post a Comment