16 April 2012

Serikali yasimamisha uchimbaji madini

Na Pamela Mollel, Manyara
 SHUGHULI za uchimbaji wa madini katika Kitalu D eneo la Mererani wilayani S ima n j i r o Mk o a wa
Manyara umesimamishwa kwa muda na Ofisi ya Madini Kanda ya Kaskazini baada ya kuibuka kutoelewana kwa wamiliki wa mgodi huo.
Mg o d i u l i o s imami s hwa
unamilikiwa na wakazi wawili
wa mkoani Arusha ambao ni
Bw.Kitinda Kimaro pamoja na
Anthony Ngoo ambapo ulipewa
leseni ya uchimbaji yenye namba
PML No.0003601 miaka iliyopita.
Kwa mujibu wa vyanzo vya
habari vilivyolifikia gazeti hili kwa
masharti ya kutokutaka majina
yao yaandikwe magazetini vilidai
kwamba ofisi hiyo imesimamisha
kwa muda wa mwezi mmoja
shughuli za uchimbaji katika mgodi
kuanzia Machi 26 mwaka huu hadi
Mei 3, mwaka huu.
Vyanzo hivyo vya habari vilieleza
kuwa lengo la kusimamishwa kwa
shughuli hizo za uchimbaji katika
eneo hilo, lililenga kutoa muda kwa
pande mbili zinazovutana kutafuta
suluhu ya namna ya kufanya kazi
kwa maelewano.
Hata hivyo, Majira ilifanikiwa
kupata nakala ya barua ya
kusimamisha shughuli za uchimbaji
katika mgodi huo yenye Kumb.Na
DA 74|503|VOL II|160 ya Machi
26 mwaka huu iliyoandikwa na
kusainiwa na Ofisa Madini Mkazi
wa Mererani mkoani Manyara
Injinia L .P Mayala.
Katika barua hiyo ambayo nakala
imepelekwa moja kwa moja kwa
Kamishna Msaidizi wa Madini
Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa
Kituo cha Polisi Machimboni
pamoja na kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Usuluhishi na Usalama
ilitaka pande mbili kuwasilisha
mapendekezo wa kufanya kazi
kwa maelewano mnamo Aprili 3,
mwaka huu.
Ha t a h i v y o , g a z e t i h i l i
lilipowasiliana na Kamishna wa
Madini Kanda ya Kaskazini,
Bw.Benjamin Mchwapaka alikiri
ofisi yake kusimamisha kwa muda
shughuli za uchimbaji katika mgodi
huo huku akisema kuwa wanasubiri
maagizo waliyoyatoa kwa pande
zote mbili yatekelezwe hadi pale
watakapokutana tena.
Alisema kwamba, pande mbili
zinazovutana katika mgodi huo
endapo zisipoweza kukubaliana ofisi
yake itachukua maamuzi magumu
kwa kuzingatia maslahi ya pande
zote huku akikataa kuzungumzia
maamuzi yatakayochukuliwa.

No comments:

Post a Comment