Na Joseph Mwambije, Songea
MKOA wa Ruvuma unakabiliwa na uhaba wa wakalimani wa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia 'viziwi' ambapo kati ya wakalimani watano waliopo, wawili kati yao ndiyo wamesajiliwa na Chama cha Wakalimani wa Lugha za Alama (CHAWALATA).
Mkalimani wa lugha za alama wa mkoani hapa ambaye amesajiliwa na chama hicho, Bw. Abdul Homera, aliyasema hayo mjini hapa jana wakati akizungumza na Majira katika mkutano Mkuu wa Chama cha Visiwi Tanzania (CHAVITA), tawi la Mkoa huo.
“Tunakabiliwa na changamoto nyingi ambapo wakalimani waliopo ni wachache na wanashindwa kujitolea, ruzuku inayotolewa na Serikali kwa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA)”
“Ruzuku inayotolewa na Serikali ni sh. milioni 10 kwa mwaka, kati ya hizo CHAVITA Taifa innapewa sh. milioni mbili ambazo zinaishia Makao Makuu kutokana na uchache wake hivyo hazitoshi kuendesha matawi yake 17 nchini,” alisema.
Aliongeza kuwa, viziwi wengi mkoani hapa wamepata ugonjwa huo baada ya kuugua uti wa mgongo ukubwani ambapo Mkoa huo una viziwi kati ya 400 na 500 ingawa sensa rasmi ya kuwatambua haijafanyika ambapo CHAVITA ina wanachama 45.
Kwa upande wake, Katibu wa CHAVITA mkoani hapa, Bi. Esha Abdalah, alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mwamko mdogo wa viziwi wilayani kutaka kufahamu lugha za alama hali inayowafanya wakwame katika mawasiliano.
No comments:
Post a Comment