05 April 2012

Adha ya umeme yawakumba wabunge

Anneth Kagenda na Frola Amon
ADHA y a k u k a t i k a
umeme mara kwa mara
imewawakumba wabunge
waliokuwa wakihudhuria
vikao vya kamati za bunge
kwenye Ofisi Ndogo ya
Bunge, hatua iliyowalazimu
kuahirisha vikao hivyo.
Akizungumza na wajumbe
wa Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC) Mwenyekiti
wake, Bw. John Cheyo,
alisema kutokana na adha
hiyo, jana walilazimika
kusitisha vikao vyao baada
ya kusubiri umeme urudi bila
mafanikio.
"Waheshimiwa wajumbe
naahirisha kamati hadi
(kesho) kwani leo, hatuwezi
kuendelea bila umeme,"
alisema Bw. Cheyo.
Wakati akiahirisha kikao
hicho tayari watendaji wa
Idara ya Mwasibu Mkuu wa
Serikali walikuwa wamefika
ofisi za bunge kuwasilisha
taarifa za matumizi ya fedha.
Kwa upande wak e
Mwenyekiti wa Kamati ya
Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC) Bw. Augustino
Mrema, yeye alisitisha
kusikiliza mchanganuo wa
ripoti ya mkoa wa Singida
kutokana na matatizo hayo
ya umeme.
Wa k i z u n g u m z a n a
waandishi wa habari baadhi
ya wabunge walisema
kukatika kwa umeme
kunaathiri shughuli nyingi
nchini.
Mbunge wa Mufindi
Kusini Bw. Mendrad Kigola
alisema "Kukatika kwa
umeme kumetuadhiri kwani
mambo mengi yameshindwa

1 comment:

  1. Acheni kulalamika. Kachukueni Jenereta lililo nyumbani kwa Mkurugenzi wa TANESCO.

    ReplyDelete