12 April 2012

Ulinzi shirikishi mwarobaini wa uhalifu

KUTOKANA na vitendo vya wananchi wengi kuwachukia askari polisi, wamekuwa mstari wa mbele
kuwalinda . Wamekuwa msaada na kuthubutu kuwaita wakombozi kutokana na ujasiri wao wa kulinda mali za watu, kuzuia ujambazi, kukabiliana na vibaka pamoja na kuwazuia wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Kati ya mambo ambayo polisi
wamekuwa wakitupiwa lawama
moja kwa moja na wananchi ni
kujihusisha na kupokea rushwa,
kutofika kwa wakati katika eneo la
tukio na kuwaachia wahalifu.
Pamoja na lawama hizo,
wamekuwa hawakati tamaa na
kuwa wavumilivu, watendaji na
wawajibikaji kwa kuzingatia sheria,
taratibu na kanuni zao na kuendelea
kuwajibika kikamilifu.
Mkoani Iringa polisi wamekuwa
mstari wa mbele katika kukabiliana
na kila aina ya uhalifu baada ya
kauli mbiu yao ya ulinzi shirikishi
ambapo sasa raia walikuwa karibu
zaidi na wakitoa taarifa hazivuji
ila zinaendelea kubakia siri kati ya
jeshi la polisi na mtoaji wa taarifa.
Polisi wamekuwa wakizifanyia
kazi kwa umakini zaidi taarifa
wanazopatiwa na raia wema ambao
wanatoa ushirikiano endapo
ukweli wa taarifa hizo utabainika
kuwa sahihi, huzawadiwa na
endapo zikawa siyo sahihi pia
mtoaji huelimishwa namna ya
kufuatilia matukio ya uhalifu ili
siku nyingine asaidie zaidi kupata
taarifa kamili.
Katika matukio ya uhalifu
yakiwemo ya ujambazi, jeshi
la polisi wamekuwa mstari wa
mbele katika kushirikiana na raia
kuhakikisha watu na mali zao
wanakuwa salama kwa kupokea
taarifa na kuzifanyia kazi mara
moja na wahalifu kutiwa hatiani
na wananchi kuendelea kuishi
katika mazingira yenye matumaini
zaidi.
Kwa mfano uhalifu wa
ujambazi, uvamizi wa magari,
wizi wa mifugo, uvunjaji wa
maduka, vibaka kuwavamia watu
wanapotoka katika biashara ama
kazi zao, wanawake kubakwa,
kujihusisha na dawa za kulevya
zikiwemo bangi kwa sasa mkoani
Iringa imekuwa historia baada ya
jeshi la polisi kushirikiana kwa
karibu zaidi na wananchi katika
dhana yake ya ulinzi shirikishi.
Maeneo ambayo awali yalikuwa
yanakumbwa na matukio ya
magari kuvamiwa ni milima ya
Nyang’oro, Kitonga, Nyololo,
Ihemi ambako magari ya mizigo
yalikuwa yanatekwa na mizigo
kupakuliwa yakisababisha hasara
kubwa kwa wamiliki magari
hayo.
Wa n a n c h i w a l i w e z a
kushirikiana na polisi kwa
kuwapatia taarifa sahihi baada
ya uaminifu kati ya Kamanda
wa Polisi wa Mkoa, Bw. Evarist
Mangalla na watendaji wake
ambapo wamezifanyia kazi
taarifa walizopata na matokeo
yake uhalifu sasa umekomeshwa
kabisa na wananchi wanaishi
kwa usalama na mali zao zipo
salama.
Ni kawaida kwa sasa kuwaona
OCD Semunye akirandaranda
katika mitaa ya Frelimo,
Mwangata, Ipogolo, Kihesa, Ilala,
Mkwawa, Kihodombi pamoja
na maeneo mengine yote katika
nyakati za usiku na mchana
akikagua askari waliopangwa
toka vituo vya mabasi wasafiri
wasiibiwe mizigo yao, mitaa
wananchi wasibomolewe
nyumbani nyakati wanapokuwa
katika biashara zao za uzalishaji
na usalama kuwa mkubwa zaidi.
Toka ujio wa kamanda mpya,
wamekuwa ni msaada mkubwa
kutokana na utendaji wao
kushirikisha zaidi wananchi,
kuwa karibu na askari wao na
kuwa wafuatiliaji wa karibu, hali
hiyo imepunguza sana ambapo
tunaweza kusema imemaliza
kero za watu kuvamiwa, kupigwa
nondo, kuibiwa na hatimaye
mali na maisha yao kuwa katika
usalama mkubwa.
Kitu kinapofanywa vizuri kwa
jamii tunatakiwa tuwapongeze.
Kwa hili ambalo linafanywa
na polisi wa mkoa wa Iringa
wanastahili pongezi na siyo kila
wakati kuwatupia lawama na
kuwashutumu.
N a w a o m b a w a n a n c h i
tushirikiane na polisi kwa kuwa
kwa hakika ni walinzi wa raia na
mali zao na ndilo jukumu lao.
Utendaji yakinifu wa polisi,
mkoani Iringa kwa sasa upo juu
na wahalifu wameingiwa na hofu
kufanya matukio waliyokuwa
wakiyafanya baada ya kudhibitiwa
kikamilifu na kusababisha sasa
kila mtu kujishughulisha kwa kazi
sahihi kwa kuhofu kuchukuliwa
hatua akikamatwa mtaani.
Miaka ya nyuma kulikuwa na
matukio ya kiuhalifu ambapo kwa
sasa ni tofauti yamepungua.
Wa n a n c h i mn a t a k i w a
kushirikiana nao kwa kuwa
kazi wanayoifanya ni kubwa ya
kuwalinda raia, mali na usalama
wa nchi nzima hata kama vitendea
kazi walivyo navyo ni dhaifu na
wanafanyakazi katika mazingira
magumu wanazingatia uzalendo

No comments:

Post a Comment