02 April 2012

'Vita madawa ya kulevya Zanzibar ni endelevu'

SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar imesema
kutokamilika kwa choo
cha kufichua madawa ya
kulevya katika Uwanja wa Ndege
wa Abeid Amani Karume si sababu
ambayo inaweza kuzorotesha shughuli
za mapambano dhidi ya dawa za
kulevya.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa
wiki na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia
Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Bi. Fatma
Abdulhabib Fereji wakati akijibu swali
la Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni
Bw. Mbarouk Wadi Mussa (CCM)
katika kikao cha Baraza la Wawakilishi
ambacho kiliketi mwishoni mwa wiki
mjini Zanzibar.
Bi. Fereji alisema kwamba, pamoja na
kutokamilika kwa ujenzi wa choo hicho
haimainishi kuzorotesha mapambano
hayo kwa vile kazi zote zinaendelezwa
kwa kutumia njia mbadala.
“Ni kweli kwamba choo hicho
kitakapoanza kutumika kitarahisisha
kazi za Jeshi la Polisi, katika kuwakamata
watuhumiwa lakini hata hivyo
kutokamilika kwake hakutozoroteshi
mapambano dhidi ya dawa hizo,”
alisema Bi.Fereji.
Aidha, alisema kwamba tayari choo
hicho kimeshafungwa katika uwanja
lakini bado kunahitajika vifaa vichache
ili ufungaji wake ukamilike.
Awali katika swali lake Mwakilishi
huyo alitaka kujua sababu zilizopelekea
kuchelewa kwa kufungwa na kutotumika

No comments:

Post a Comment