Na Damiano Mkumbo, Singida
WAZIRI Mkuu, Bw.
M i z e n g o P i n d a
amewataka Watanzania
kujenga tabia ya kupanda miti kwa
wingi ili kuendeleza maisha yao
sabamba na kuyatunza mazingira.
Bw. Pinda alitoa mwito huo
wakati alipokuwa akizungumza
na wananchi katika maadhimisho
ya siku ya upandaji miti Kitaifa
yaliyofanyika katika Kijiji cha
Ilongero Halmashauri ya Wilaya
ya Singida juzi.
Alisema, ni lazima Watanzania
wakiwemo wakazi wa Mkoa
wa Singida walipe umuhimu
mkubwa suala la upandaji miti
na kuhakikisha kuwa inapona na
kukua, bila kungoja siku ya Taifa
ya kupanda miti.
Alisema, uhai wa binadamu na
wanyama unategemea miti, hivyo
wananchi wahamasike kupanda
miti na kuitunza iliyopo pamoja na
vyanzo vyake ili visikauke.
Pandeni miti kwa kutumia mbegu,
vikonyo na pingiri katika maeneo
maalum yaliyotengwa, vyanzo
vya maji, kuzunguka mashamba
na nyumba tunazoishi hata kama
ni za kupanga,” alisema Waziri
Mkuu.
Kuhusu mazingira alisisitiza
kuachwa tabia ya kukata misitu
kiholela na kuchoma moto
ovyo, kwa kuwa itamaliza miti
katika harakati za kupambana na
mabadiliko ya tabia nchi ambayo
yanaweza kuleta tishio kwa maisha
ya binadamu.
Pia aliwahimiza wakazi wa
Mkoa wa Singida kutumia fursa
ya misitu iliyopo katika kufuga
nyuki ili waweze kuvuna asali
na kuuza kwa ajili ya kuongeza
kipato chao.
Pandeni...pia miti ya matunda
kama miembe ya kisasa na mingine
kwa wingi kwa ajili ya kuboresha
lishe na kufanya biashara hiyo
itakuwa kichocheo kikubwa kwa
wakulima wadogo,” aliongeza.
Kuhusu mboga mboga Waziri
Mkuu alisema ni vema wakulima
wajipange katika bustani za aina
mbalimbali za mboga ili waweze
kufanya biashara na kuinua uchumi
wao.
Aliagiza kamati za ulinzi na
usalama za ngazi za vijiji hadi
mkoani ziongeze kipengele cha
kulinda misitu na kuondoa tatizo la
uvamizi wa maeneo hayo, ambalo
lazima zione kuwa ni jukumu lao.
Katika salamu zake kwenye
maadhimisho hayo Waziri wa
Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel
Maige alieleza kuwa wananchi
wameongeza hamasa ya kupanda
miti kutoka miche milioni 80
kabla ya mwaka 2001 na kufikia
miche 162.1 kati ya mwaka 2007
na 2011.
Bw. Maige alisema kuwa hata
hivyo bado kuna changamoto
nyingi, mojawapo ikiwa ni kuwa na
miti iliyopandwa bado haitoshelezi
mahitaji ya watumiaji, kwa kuwa
mazao ya misitu mahitaji yake
yameongezeka.
Katika maadhimisho hayo Waziri
Mkuu aliongoza operesheni ya
upandaji wa jumla ya miti 1,160
ya aina mbalimbali kwenye eneo la
chanzo kikuu cha maji katika Kijiji
cha Ilongero pamoja na kukagua
chanzo hicho cha maji.
Hata hivyo tafiti zinaonesha kuwa
mwananchi mzalendo huwa anatoa
kipaumbele katika kuyatunza
mazingira yanayomzunguka kwa
kuwa bila kuyatunza ni vigumu
kujipatia hewa safi ikiwemo
huduma ya maji.
Pia hali ya kukosekana kwa maji
katika sehemu ambazo hazina miti
ya kutosha ni kutokana na ongezeko
la ukame ambalo husababisha
kukauka kwa vyanzo hivyo siku
No comments:
Post a Comment