16 April 2012

Wateja wa M-Pesa kupata punguzo la kutoa fedha

Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu (katikati), akionesha nambari ya Mshindi wa Droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Bw. Revocatus Mkama, alishinda na kupata sh. milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid na Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma. (Na Mpigapicha Wetu)
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
KA M P U N I y a
Ma w a s i l i a n o y a
Vodacom Tanzania
imepunguza gharama
zake za kutoa fedha kwa kupitia
huduma yake ya M-Pesa hadi
asilimia 20 kwa mteja anapotoa
fedha kwa wakala yeyote wa
huduma hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom, Bw. Rene Meza alisema
gharama hizo zimepunguzwa
rasmi kuanzia leo kwa wateja wa
Vodacom sasa wanao uwezo wa
kutoa fedha kutoka kwa wakala
yeyote nchini na watatozwa kwa
hizi gharama mpya na nafuu
zitakazosaidia zaidi shughuli
za kiuchumi na kijamii za watu
waliosajiliwa na huduma ya
Vodacom M-Pesa.
"Tunaelewa hali ya uchumi
nchini na tunafahamu jinsi M-Pesa
ilivyokua huduma muhimu na
bora katika maisha ya kila siku
ya Watanzania, Hivyo tumeamua
kuifanya iwe nafuu zaidi na
rahisi kwa wateja wetu," alisema
Mkurugenzi huyo katika taarifa
iliyotolewa ya kutambulisha
gharama mpya za kutoa fedha.
Alisema upunguzaji huu
umekuja miezi michache baada ya
kampuni ya kupunguza gharama
za kutuma fedha na kuwa ndogo
kwa kiasi cha kuanzia sh. 50 kwa
muamala na kuzindua promosheni
ya siku 90 iitwayo 'Tuma na
Ushinde' ambapo sh. milioni 480
zitashindaniwa kwa kipindi chote
cha promosheni.
Alisema jukumu letu ni
kuhakikisha kwamba wateja wetu
wana furaha na wanajiwezesha
kupitia huduma ya M-Pesa.
Tutaendelea kuboresha bidhaa
na huduma zetu ambazo tunatoa
kwenye M-Pesa ili kuhakikisha
umuhimu kwa maisha ya kila siku
ya wateja

No comments:

Post a Comment