NALIPONGEZA gazeti
lako kutupatia wananchi
nafasi ya kuelimishana
na kutoa maoni kwa
maendeleo ya nchi yetu.
Shamsi Vuai Nahodha, wewe
ndiye Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi. Sijawahi, lakini safari hii,
nimeamua nitumie njia hii kukupa
mang'amuzi yangu kwa sababu
najua nikisubiri tuonane ana kwa
ana, tutasubiri hadi nyoka aote
mabega.
Waziri wangu, wahenga
walisema, sikio halilali njaa! Hata
langu halilali njaa ndiyo maana
nimeyasikia haya. Japo ni kama
hayanihusu, nimekubali kuitwa
mmbea, lakini niyafikishe maana
mbona naona yanahusu nchi yangu
na usalama wangu pia? kwa nini
mtu aseme hayanihusu?
Ni kwamba, kuna watu wachache
ambao ni wajanja, wanataka
watumie ujuzi wa kuzungumza na
kurubuni, kukushawishi wewe na
watendaji wako ili “muingine
mkenge‚ kisha wao wafurahi,
wajitoe na kukaa pembeni.
Wakifanya hivyo, hapana shaka,
wataanza kuwasukuma hata vijana
na wale wasiojua hili wala lile,
waingie barabarani kukushinikiza
ujiuzulu ili wao wafurahi na hata
ndoto zako nyingine za kulitumikia
vyema taifa katika medani za
kisiasa, zife kifo cha mende. Ndiyo
maana nakuomba, usikubali ng
Waziri wangu, ukubali usikubali,
nimesikia kuna watu wachache
wanaokushinikiza upeleke
mchakamchaka wazo lao bungeni,
ili sheria itamke na kuitambua rasmi
sekta binafsi ya ulinzi na kuipa
mamlaka kamili wanayopendekeza
iitwe Private Security Industry
Authority.
Kwamba hili ukilifanikisha, sekta
hiyo iwe na mamlaka kamili kama
Jeshi, lijitegemee na lisimame na
kujiratibu kama si kujisimamia
na kufanya mambo yake yenyewe
kama wanavyotaka, itakuwa balaa,
hapatatosha kwa sababu hawa
hatatawalika wala kuongozwa.
Niliposikia hayo, nimejawa na
mawazo kwa muda mrefu sasa.
Sijafikiria kingine na kama wewe
unakijua tofauti na kwamba hawa
wanataka kuanzisha Jeshi jipya
nchini, uniambie, lakini kwa
uelewa wangu, wazo hilo linaenda
huko hata kama kwa sasa linaweza
kuwa limejificha ndani ya maneno
mengine yanayoweza kuonekana
matamu.
Hakika, huku ni kuanzisha
Jeshi lingine ndani ya nchi, au
basi mpango huo una malengo
mengine labda ya kisiasa tofauti
na unavyoweza kufikiriwa na
kuonekana.
Kinachoshangaza ni kwamba,
wameandikiwa na Wazungu
muswada wa sheria ambao ndio
huo wanaoupenyeza na kuzunguka
nao kwapani, ili kukushinikiza kwa
vitisho vya vurugu katika sekta
binafsi ya ulinzi, ili muswada huo
au mpango huo uupeleke bungeni
wakati hata wadau hawaujui.
Wanashindwa kujua kuwa kwa
kawaida, muswada wa sheria
lazima upite katika michakato
mingi inayowahusisha wadau na
utazamwe kisera, ndipo ufanywe
muswada na hatimaye, sheria na
sio idara, chama, kikundi au mtu
mmoja mwenye nguvu ya fedha
kujitungia sheria katika nchi kama
inavyoonekana katika jambo hili.
Nakuomba Waziri wangu, uwe
macho.
Ukichunguza utabaini kuwa
mpango huu wa mapendekezo ya
muswada wa sheria ya sekta binafsi
ya ulinzi, unasukumwa na mtu
mmoja au wawili ambao ama ni
miongoni mwa viongozi wa chama
cha wamiliki wa makampuni binafsi
ya ulinzi, au ni mmiliki mmojawapo
wa kampuni binafsi ambayo kwa
mtazamo wake, anaona ina nguvu
labda kuliko zote au inazidiwa na
sasa anataka kuiponya kimaslahi.
Mapendekezo ya mpango huo
una sababu nyingi za kibinafsi
zilizojificha, ikiwamo maslahi
ya kuendesha mambo mengi
yatakayofanywa na sekta binafsi
ya ulinzi ikiwa ni pamoja na kupata
fedha toka kwa nchi marafiki au
wafadhili.
Swali ni kwamba, tangu
wameanza kutoa fedha na
misaada katika vyama hivyo
vinavyokushinikiza tumenufaika
nini kama nchi, kama sio kuishia
kuwaneemesha na kuwanenepesha
wahusika wachache?
Kwamba kwa msingi huo, katika
kufadhili vyama vya kitaaluma
katika sekta hiyo vinavyoweza
kuwa na majina kama Tanzania
Security misaada inayotolewa na
wafadhili, iwe inafikia kwao yaani
kampuni moja au mbili ili waitumie
watakavyo, badala ya kuwafikia
walengwa ambao ni wadau wote
wa sekta binafsi ya ulinzi.
Lakini usisahau kuna nchi
ambazo sekta hii ilianza kujitenga
na Jeshi la Polisi, kama hawa
wanavyotaka kufanya, katika nchi
hizo kwa sasa sekta hiyo ni vurugu
na wadau wake ni jeuri kwa Serikali
na hawatawaliki.
Pia ukiperuzi katika rejea na
mitandao utagundua kwamba katika
nchi nyingine, askari wa kampuni
binafsi za ulinzi wamekuwa ni
chanzo cha uasi katika majeshi na
mapinduzi ya Serikali halali.
Ndiyo sababu nashindwa
kuamini ama nashangaa kwa nini
Jeshi letu halijachukua hatua ya
kuchunguza mienendo ya wadau
hao na kudhibiti udanganyifu,
uchochezi na uongo unaosambazwa
ili kupotosha nia njema ya Serikali
ya kuanzishwa sekta binafsi ya
ulinzi hapa nchini.
Au nao wameingia katika mtego
na kushabikia mambo ambayo
hawajayapima urefu na upana
wake, kwa maslahi ya amani na
umoja wa nchi yetu?
Tafisri iliyojificha hapa, ni hasa
kutaka kuwaendeleza watu wa nje
ya nchi na kuwameza wazawa au
kuanzisha Jeshi jipya kwa malengo
gani, au ndio tuanze kufunga vilago
na kutafuta fursa za ukimbizi
kwa sababu wanasiasa wengine
wamekwishasema, 2015 kwa udi
na uvumba lazima wapate, la sivyo,
nchi hii haitatawalika.
Hayo yanaweza kuwa ni
maandalizi ya msingi ya nchi
kutotawalika wakati ukifika!
Waziri, ili ukiliachia mwanya,
litafungua milango na madirisha
kwa makampuni ya nje kuingia
hapa nchini yakiwa na mitaji,
rasilimali, teknojia na ujuzi mkubwa
na hivyo, yasitake ubia na kampuni
za wazawa kwa lengo la kuficha
mambo.
Hapo tutakuwa tunafanya nini?
Ndiyo maana nasema, hili linalenga
kuwameza wazawa au kuwatumia
wazawa walio tayari kuwameza
wazawa wenzao ili kufikia malengo
tarajiwa.
Kumbuka wanakuja na fedha
zao, mafunzo yao, teknolojia yao
na jeuri yao.
Wa k i p ewa n a f a s i h i y o ,
watashawishi kuunganisha kampuni
zile giant (kubwa) ili hizi ndogo za
wazawa zigeuzwe kuwa mawakala.
Waziri! Mambo haya yanahitaji
mwono wa mbali na ndiyo maana
hawataki kukupa muda na nafasi ya
kuuona mwono huo.
Kila kukicha wanakutandika
na barua zenye vitisho lukuki,
ili ukurupuke. Chonde chonde,
nakuomba kwa aina ya bembeleza
ya mtoto wa mkulima, Waziri
Nahodha, usikurupuke wala
kukurupushwa. Tulia kama ilivyo
tabia yako, pelekea chombo taratibu
ili tufike salama.
Chama chochote makini, kiwe
cha kisiasa au katika sekta binafsi
ya ulinzi, kinapaswa kuwaonesha
wamiliki wa kampuni na wanachama
njia na mbinu za kuendeleza sekta
yao na sio kuwakandamiza.
Waziri naomba ukumbuke
kuwa hivi sasa sekta binafsi ya
ulinzi inabeba ajira ya Watanzania
takriban milioni mbili wengi wao
wakiwa ni vijana, hivyo kama una
mwelekeo wa kulibariki wazo la
mmiliki wa chama kimoja, basi
unataka Watanzania milioni mbili
wamilikiwe na kuamrishwa na
wageni katika suala hili nyeti?
Jambo hili nadhani linalenga pia
ama kuviwekea masharti magumu
vikampuni vya wazalendo,
au vifutwe ili wageni wapate.
Tunakwenda wapi?
Tukumbuke kuwa, uanzishaji
wa kampuni hizi una taratibu zake
ikiwa ni pamoja na waanzilishi
kuwa Watanzania waliokuwa
waajiriwa katika vyombo vya
ulinzi na usalama kama vile
JWTZ, Usalama wa Taifa, Jeshi
la Magereza, Jeshi la Polisi na
kadhalika.
Hili ni eneo lililokuwa limelenga
kuwawezesha watumishi hao
wanaostaafu wakiwa na nguvu,
watumike kwa hiyari yao kwa
manufaa ya taifa katika sekta
binafsi ya ulinzi wakijipatia kipato
halali na kuutumia vizuri ujuzi
wao.
Eti hao sasa kwa mpango
huo, waangushwe badala ya
kuwanyanyua. Au ndio hivyo
tuwarasimishe kwa Wazungu, ili
waamrishwe kuasi na kuwashawishi
wenzao waliowaacha katika majeshi
ya ulinzi na usalama kuwaunga
mkono?
Kimsingi ukiangalia kwa makini,
utabaini kuwa wanao ngangania
mpango huo, wanajitahidi sana
kuwashawishi watu wasiojua
historia na malengo ya kuanzishwa
sekta binafsi ya ulinzi, kwa
kuwatisha watu kwamba kuna
mgogoro ama vurugu, lakini ukweli
ni kwamba huo mgogoro wala
haupo. Uko wapi mgogoro?
Kinachodaiwa kuwa ni mgogoro
ambacho hujakijua, ni kwamba kwa
miaka kumi hivi, kumekuwa na
chama kiitwacho Tanzania Security
Industry Association (TSIA). Sasa,
wasioridhika na uendeshaji wa
chama hicho wamejiengua na
kuanzisha chama kiitwacho, Chama
cha Wamiliki wa Makampuni
Binafsi ya Ulinzi yenye Rasilimali
Watu.
Wa z i r i wa n g u , n a omb a
nitakufafanulia kidogo kwamba,
walinzi au kampuni binafsi tulizo
nazo nyingi ni zile zenye rasilimali
watu na ndizo zilizo nyingi yaani,
ulinzi wa kutumia rasilimali watu.
Huu ni ulinzi wa mtu akiwa na
silaha kama bunduki au kirungu
(man guard).
Hivyo, ujio wa chama chenye
malengo ya kujihusisha na rasilimali
watu, umechochea mwamko
wa kujitambua miongoni mwa
wadau.
Pamoja na kundi hilo, kibali
cha kuanzisha huduma ya ulinzi
kinapotolewa, kinazingatia mambo
yafuatayo; je kampuni inataka kutoa
huduma za ulinzi kwa kutumia
mitambo ikiwamo ya kuzuia wezi
na inayorekodi matukio na kuweka
kumbukumbu? Je, inataka kutoa
huduma ya ushauri wa kiusalama
na ulinzi? Au je, unataka kutoa
huduma za upelelezi binafsi?
Kama nilivyosema, ukichunguza
utagundua kwamba wengi
wanaangukia katika kundi la
kwanza la man guard na ndilo lenye
hao watu milioni mbili.
Kwa hiyo utabaini kwamba
uanzishaji wa chama chenye
kulenga rasilimali watu umeleta
ugomvi kwa vyama kongwe. Huu
ni ugomvi baina ya walio wengi‚
waliohama na kuanzisha chama
kipya na wachache waliobaki.
Waziri wangu Nahodha, ujue
ugomvi wa kugombea wanachama
sio jambo jipya, bali cha muhimu
ni kujua propaganda na mbinu
za ujenzi wa chama. Ijulikane
pia kwamba, siku zote ujenzi
wa vyama vya hiari ambavyo
watu hawashinikizwi na sheria
ama taratibu, njia inayotumika ni
kuhamasisha siyo kulazimisha watu
(wanachama).
Pata picha kwamba, katika
muktadha huo, chama kilichoachwa
kuona ukiwa uzeeni, lazima kelele
na mbinu chafu kama hizo zitokee,
tukubali tusikubali.
Kimsingi, Waziri na wataalamu
wako mnapaswa kuangalia kama
kuna athari zilizojitokeza kiutendaji
miongoni mwa kampuni moja moja
kwa kuanzishwa chama kipya
katika sekta ya ulinzi na kama
hakuna athari ya nini kujiingiza
katika marumbano yao.
Nasema hivyo nikijua kwamba
kibali cha kufanya huduma ya
ulinzi hutolewa kwa kila kampuni
na si kwa chama na kampuni ndiyo
inayowajibika kwa utendaji wake.
Wataalamu wako waangalie je, kuna
ulazima wa kutaka makampuni
zote ziwe katika chama kimoja
hata kama hawakitaki au hawaoni
sababu ya kuwa katika chama
hicho?
Kimsingi, jibu lake ni hapana,
hivyo ushauri ninakuomba uepuke
kujiingiza katika mgogoro huo,
kwa sababu hauna maslahi na
chama chochote kati ya hivyo
viwili, bali maslahi yako ni ya
umma.
Msema kweli,
Tanzania
Ninaungana na mawazo yaliyotolewa 100%. Wazo la hiyo private security authority ni ya kupinga kwa nguvu zote.
ReplyDeleteWaziri wetu Nahodha akae nalo mbali. Wabunge wetu wasisikie hata harufu yake. Huwezi kuchanganya mambo ya Private Securiy na mambo ya Serikali. Private na Serikali haziwezi kuchanganywa. Ndio maana vyombo vya Ulinzi (security) vinasimamiwa Na RAIS kama Amiri Jeshi Mkuu.
Mfano wa Wamarikani wa kutumia Private Security services huko Iraq na kwingineko ulileta matatizo mengi sana na wanajuta.
Serikali kusimamia watu au vyombo binafsi (Private business) ni kugumu sana. kawaida hawa watu binafsi hawataki kuingiliwa. Kwa hiyo na wao hawatakiwi kungilia shughuli za security zilizopangiwa Serikali duniani kote.
Mh. Waziri, nakuomba wazo hili usiliachie likavuka kizingiti cha mlango wako wa ofisi.
Hata hao wenye mpango huu wauache mara moja baada ya kusoma makala ya gazeti hili hapo juu.
Hatukatai ulinzi binafsi lakini uthibitiwe na na Serikali au mtatumaliza badala ya kutulinda.
Njooni na mbinu za kuboresha ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani na nyie kuhusu security (ulinzi shirikishi)