05 April 2012

Watumishi wazorotesha mapato ya halmashauri

MA D I WA N I w a
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wamesema kupungua kwa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo ni dalili inayotokana na uvujaji wa fedha unaofanywa na baadhi ya
watumishi.Pia walidai hali hiyo imekuwa
ikichangia baadhi ya watumishi
kuvujisha na hata kughushi
stakabadhi za kukusanyia mapato.
Imeelezwa kuwa watumishi
hao wamekuwa wakiigeuza
halmashauri hiyo kama shamba la
bibi kwa kuchota fedha watakavyo
na hivyo kusababisha kushuka kwa
mapato kutoka sh. milioni 600
zilizokusanywa mwaka jana hadi
kufikia sh. milioni 300 mwaka huu.
Hayo yalisemwa juzi wakati wa
Kikao cha Baraza la Madiwani
kilichofanyika katika Ukumbi
wa John Mwankenja ambapo
walisema kama vitendo vya ufujaji
fedha vinavyofanywa na baadhi
ya watendaji vitaendelea itabidi
Mkurugenzi wa wilaya hiyo Bw.
Noel Mahyenga pamoja na Mweka
Hazina wa halmashauri Bw. John
Shirima wawajibike.
Akizungumza katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Masukulu, Bw.
Rephson Mwaisupule alisema,
miezi mitatu iliyopita katika
kipindi cha mwaka jana fedha
zilizokuwa zimekusanywa katika
vyanzo vya ndani vya mapato
zilikuwa sh. milioni 600 lakini
katika hali ya kushangaza mwaka
huu zilizokusanywa ni sh. milioni
300 tu.
Naye Diwani wa Kata ya Kawetele
Bw. Anyimike Mwasakilali alisema
tatizo la ufujaji wa fedha za
mapato katika halmasahauri hiyo
ni aibu hivyo inatakiwa watendaji
wote waliofanya ubadhirifu huo
kuchukuliwa hatua za kisheria
wakiwemo watendaji wa kata na
vijiji wanakusanya fedha katika
kata zao na vijiji.
Naye Diwani wa Kata ya
Lwangwa Bw. Robart Mwaibata
alisema baadhi ya watumishi
wamekuwa wakiandika ushuru
ma l i p o ma k u bwa ka t i k a
stakabadhi za malipo lakini fedha
zinazofikishwa halmashauri ni
kidogo hali ambayo imekuwa
ikisababisha halmashauri kujikuta
haina mapato ya kutosha.
Akizungumzia malalamiko
hayo ya madiwani Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya
ya Rungwe Bw. Meckison
Mwakipunga alisemna kuwa
halmashauri tayari imeanza
kuchukua hatua dhidi ya watendaji
wanaofuja fedha ambapo hadi sasa
watumishi 11 wa halmashauri hiyo
wamesimamishwa kazi.
Alisema kuwa, tayari watumishi
hao hawapo kazini baada ya
kubainika kufuja fedha hizo
na uchunguzi zaidi unaendelea
kuhusiana na ufujaji huo ili kujua
kama kuna watumishi wengine
waliofanya ubadhirifu huo nao
waweze kuchukuliwa hatua kama
walivyochukuliwa hawa wengine.
Tunachoomba ni ushirikiano kwa
nyie madiwani kwenye kamati ya
fedha ambayo tayari ipo, kazini
kushughulikia ubadhirifu huo,
tunajua tutawabaini wengine
ambao wamejificha kwani fedha
hizo zimefunjwa na wengi, alisema
Mwenyekiti huyo.

1 comment:

  1. Ndio hawa wafujaji fedha za Halmashauri ambao Mh. Mukama wa CCM ambaye anataka kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa iwafichie siri?

    ReplyDelete