24 April 2012

Iran yatengeneza ndege kama ya Marekani

TEHRAN,Iran

SERIKALI ya  Iran imedai kwamba imepata maelezo ya undani kutoka ile ndege ya Kimarekani isiyokuwa na rubani ambayo ilianguka mwaka jana.

Kati ya  mambo ambayo Iran iliyagundua kutoka ndege hiyo ni kwamba ilitumiwa kumpeleleza,Bw. Osama Bin Laden wiki kadhaa kabla ya kuuawa.

 Iran ilisema imefanya mabadiliko ya kiuhandisi kwa ndege hiyo, na sasa inatengeneza aina ya ndege kama hiyo.

 Marekani ilisema ndege hiyo haijafanya kazi vilivyo, na imepuuza maelezo kwamba Iran huenda ikagundua mambo ya siri kutoka kwenye ndege hiyo.

Ndege hiyo ilianguka Mashariki mwa Iran  Desemba mwaka jana  na ilipatikana ikiwa haijaharibika.

Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo.

Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege hiyo isionekane na vyombo vya rada.

Ndege hiyo ya aina ya Sentinel isiyohitaji rubani, inatumiwa sana na Marekani kugundua maficho ya makundi ya wapiganaji nchini Afghanistan na Pakistan.(BBC)

No comments:

Post a Comment