Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JUMLA ya kaya 1,155
zenye kipato duni katika
Halmashauri ya Chamwino
mkoani Dodoma watapatiwa
matibabu bure.
Ha y o y a l i b a i n i s hwa n a
Mk u r u g e n z i Mt e n d a j i wa
halmashauri hiyo, Bw. Daud Mayeji
wakati akizungumza na gazeti hili
jana katika halmashauri hiyo.
Alisema, kaya hizo zinalazimika
kupewa huduma ya afya baada
ya kubainika kuwa hazina uwezo
wa kifedha hasa kujiunga katika
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF).
Mkurugenzi huyo alisema, kaya
hizo zitapewa vyeti ambavyo
vitakuwa vinawatambulisha
Wa n a k a y a h a o n a t a y a r i
kumefanyika uhakiki kwa ajili ya
kutambua kaya hizo.
Alisema, pamoja na kaya hizo
kupatiwa matibabu bure bado
halmashauri yake inaendelea kutoa
elimu kwa wananchi wa Chamwino
kwa ajili ya kujiunga katika mfuko
wa HIF.
Bw. Mayeji alisisitiza kuwa elimu
inatolewa kwa wananchi wengi
hususan wananchi waishio vijijini
ili waweze kutambua umuhimu
wa kujiunga katika mfuko huo
ambao una lengo la kuwarahisishia
wananchi kupata matibabu bila
usumufu wowote.
Aidha, alisema halmashauri
i n a f a n y a k i l a j u h u d i y a
kuboresha huduma ya matibabu
kwa wananchama wote ambao
wamejiunga na mfuko huo pamoja
na kuboresha mazingita ya matibabu
kwa wanachama.
Alisema, pamoja na kuwa wilaya
hiyo kuwa na sifa ya kufanya vizuri
katika utoaji wa huduma ya afya
kwa wananchama lakini bado kuna
changamoto mbalimbali amba
zo zinafanya wanachama wengine
kutojiunga na mfuko huo.
Mkurugenzi huyo alizitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja
na wananchi wengi wa Wilaya ya
Chamwino kuwa na kipato kidogo
jambo ambalo linasababisha wakazi
kutojiunga na mfuko.
Hata hivyo Halmashauri ya
Chamwino ni kati ya halmashauri
chache ambazo zilipatiwa tuzo
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Bw.
Mizengo Pinda kwa ajili ya
kusiamia na kutekeleza mpango
wa utoaji wa huduma ya afya kwa
wananchama vema.
No comments:
Post a Comment