29 October 2013

WANAOMPINGA JK WAKAMATWA



  •  WALIKUWA NA BUNDUKI TATU, MAPANGA 18 NA VISU
  • WAKUTWA MSITUNI, WAPO WATUMISHI WA SERIKALI

 Na Yusuph Mussa, Handeni
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, amesema watu waliomuua askari mgambo Salum Mgonje na kumpiga risasi Mkuu wa Kituo cha Polisi Songe, wilayani Kilindi Edward Lusekolo ni kikundi kilichokuwa kinaishi msituni.

MWIGAMBA AZIDI KUIBUA MAZITO

  • AMTOLEA UVIVUMBOWE,ASISITIZA MABADILIKO


 Pamela Mollel na Goodluck Hongo
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha, Bw. Samson Mwigamba, amesema kutokana na uadilifu wake na mapenzi mema aliyonayo katika chama, ameamua kuachia madaraka kwa muda ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

M23 WAUA ASKARI WA JWTZ



Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema askari wake Luteni Rajabu Mlima, ameuwawa mjini Goma, Congo (DRC), baada ya kupigwa risasi wakati akitekeleza jukumu lake la ulinzi wa amani nchini humo, anaripoti Darlin Said.

ALIYEMPIGA MTAWA JELA MIEZI SITA



  Mahakama ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imemhukumu mfanyabiashara maarufu mjini humo, Bw. Dola Jamal, kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kumshambulia Mtawa wa Kanisa la Katoliki, anaripoti Raphael Okello, Musoma

24 October 2013

MPASUKO MPYA SEKTA YA ELIMU



  • MAWAZIRI ZANZIBAR,BARA SASA KUKUTANA
  • KUJADILI MITAALA MASOMO YA DINI,MUZIKI
Na Faki Mjaka-(MAELEZO) Zanzibar
  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema masomo ya dini na mengine, yataendelea kufundishwa pamoja na kufanyiwa mitihani katika ngazi zote.

RIPOTI : UHALIFU WAONGEZEKA TANZANIA



 Na Grace Ndossa
  Hali ya ulinzi na usalama nchini, imeendelea kudorora kutokana na ongezeko la matukio ya uhalifu yanayoendelea kufanywa na baadhi ya watu. Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Kupunguza Umaskini nchini (REPOA), Dkt. Abel Kinyondo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akiwasilisha taarifa ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Afrobarometa, kuhusu matukio ya uhalifu nchini.

BAN KI-MOON AIMWAGIA SIFA APRM AFRIKA



 Na Hassan Abbas
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw. Ban-Ki Moon amesema Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) ni nguzo muhimu ya kukuza utawala bora barani humo.

MALINZI AAHIDI NEEMA AKIWA RAIS TFF



Na Mwandishi Wetu
  Mgombea Urais katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema endapo atachaguliwa katika nafasi hiyo, anaahidi kuenzi mafanikio ya awamu inayomaliza muda wake.

HAMIS KIIZA AWAPA FARAJA YANGA SC


  • SIMBA SC YABANWA MKWAKWANI
Na Waandishi Wetu
  Mshambuliaji, Hamis Kiiza wa Yanga jana aliwapa faraja mashabiki wa timu hiyo baada ya kuifungia mabao mawili kati ya matatu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora.

VODACOM YAWAPAMBA WAHARIRI



 Na Goodluck Hongo
  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, jana imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya wahariri wa vyombo vya habari na timu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 3.5.

23 October 2013

KIKWETE: NI AIBU SERIKALI KUDAIWA



  • AKIRI WAKULIMA KUDAI BILIONI 17/- ZA MAHINDI
  • KUTOA MELI ZIWA NYASA , VICTORIA, TANGANYIKA

 Na Mwandishi Wetu, Ludewa
Rais Jakaya Kikwete, amesema ni aibu Serikali kudaiwa na wakulima wa Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe ambao wameiuzia mahindi yao. Kutokana na hali hiyo , aliwahakikishia wakulima hao kulipwa fedha zao haraka iwezekanavyo.

BILAL AONGOZA KUAGWA NYAISANGA


  • PADRI ATAKA WAANDISHI WA HABARI WAHESHIMIWE

  Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mtangazaji mkongwe na Meneja wa Kituo cha Abood Media, marehemu Julias Nyaisanga, aliyefariki dunia Oktoba 20 mwaka huu, mkoani Morogoro, baada ya kusumbuliwa na kisukari. Marehemu Nyaisanga aliagwa jana katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni Dar es Salaam
 Na Rehema Maigala

  Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana ameongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji mkongwe na Meneja wa Kituo cha Abood Media, marehemu Julias Nyaisanga, aliyefariki dunia Oktoba 20 mwaka huu, mkoani Morogoro.

KAMANDA JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA



    

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), mstaafu James Kombe (pichani) amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam, anaripoti Frank Geofray-Jeshi la Polisi

PAC YATAKA WIZARA YA ELIMU IKAGULIWE



  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi wa mahesabu haraka iwezekanavyo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kuondoa sintofahamu ya mahesabu yake, anaripoti Anneth Kagenda.

KESI YA PINDA YAKWAMA



   Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ilishindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kikatiba aliyofunguliwa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), anaripoti Rehema Mohamed. Hali hiyo ilitokana na kiongozi wa jopo la mawakili wa Serikali, Naibu AG, George Mwasaju kutokuwepo mahakamani hapo

LAAC: TUMEBAINI UBADHIRIFU URAMBO



   Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imebaini ufisadi mkubwa baada kupitia vitabu vya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kwa mwaka 2011/2012 zinazoonesha sh. milioni 13.8, zililipwa mishahara kwa watumishi hewa, anaripoti Anneth Kagenda.

UHABA WA WATAALAMU KUTAWALA MKUTANO MKUU NAIROBI KENYA



Na Anne Kiruku, EANA
  Mkutano wa siku tatu unaojumuisha wataalamu wa vyuo vikuu vya umma vya Afrika Mashariki na watendaji wakuu wa sekta binafsi, unatarajiwa kujikita zaidi kuhusu uhaba wa wataalamu na mahitaji ya soko la ajira.

TTCL KUPAMBANA NA UHALIFU WA MITANDAO




Na Mwandishi Wetu
  Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imejidhatiti kupambana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu kupitia mitandao ili kuwahakikishia wateja wake huduma bora.

KIVUMBI CHA LIGI KUU KUENDELEA LEO



  •   YANGA HUKU SIMBA KULE

Na Neema Ndugulile
  Ligi Kuu ya Vodacom, inatarajia kutimua vumbi tena leo katika viwanja vitatu tofauti, ambapo Yanga itaikaribisha Rhino Rangers katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

KABURU AMWAGA SERA WAJUMBE WAMCHAGUE



Na Mwandishi Wetu
  Mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Shirikisho la Mpira w a Miguu Tanzania(TFF), Geofrey Nyange 'Kaburu' kupitia Kanda nam ba 11 ya Morogoro na Pwani, amewataka wapiga kura katika Uchagu zi Mkuu utakaofanyika Jumapili hii, kumchagua ili awez e kushirikiana na viongozi wenzake kuleta mabadiliko kat ika taasisi hiyo.

MALINZI KUANIKA MIKAKATI YAKE LEO


Na Mwandishi Wetu
  Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), mgombea wa nafasi ya urais, Jamal Malinzi leo anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari kuzindua rasmi kampeni zake, huku akitoa mpango endelevu wa kuendeleza soka nchini ndani ya kipindi chake.

SERENGETI BOYS YAALIKWA OLIMPIKI



 Na Fatuma Rashid
  Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Serengeti Boys), imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika itakayofanyika Mei mwakani.

22 October 2013

DKT. SHEIN AVUNJA UKIMYA WA KATIBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pianiMakamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, akifungua semina ya sikunneya watendaji na viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya na mikoa Mjini Dodoma jana

  • ASEMA CCM HAINA NIA YA KUHODHI MCHAKATO
  • ATOA AGIZO ZITO KWA MAKATIBU WILAYA, MIKOA
Na Elizabeth Joseph,Dodoma
  Chama Cha Mapinduzi ( C C M ) , k i m e s e m a hakijahodhi wala hakina nia ya kuhodhi mchakato wa Mabadiliko ya Katiba unaoendelea kama inavyosemwa na baadhi ya vikundi.

WAFUASI WA PONDA WAACHIWA

  • MAHAKAMA KUU YABAINI KASORO ZA KISHERIA

 Na Grace Ndossa

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewaachia huru wafuasi 52 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, waliokuwa wakikabiliwa mashtaka matatu.

MAWAKILI: PINDA ANA KINGA YA BUNGE



 Mawakili katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), dhidi ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, jana waliendelea kuvutana mahakamani, anaripoti Grace Ndossa.

AANGUKA, AFA AKITOA USHAHIDI KORTINI



  Mkazi wa Kijiji cha Bitale, Wilaya ya Kigoma Vijijini, amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitoa ushahidi kwenye Mahakama ya Mwanzo, iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma, anaripoti Mwajabu Kigaza, Kigoma.

‘VIPODOZI VINACHANGIA UKOMA’



  Wanawake na wanaume wanaopenda kujichubua, wapo hatarini kupata ugonjwa wa ukoma kutokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, anaripoti Elizabeth Joseph, Dodoma

TANZANIA YAPAA KIUCHUMI EAC



 Na Penina Malundo
  Imeelezwa kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika Mashariki ukilinganisha na Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi

TAMWA IUNGWE MKONO KUPIGANIA USAWA WA KIJINSIA



Alexander Joseph
"Tofauti hii inatokana na ukweli kuwa, hicho ni kipindi cha ongezeko la talaka na kasi ya watoto kubaki wakilelewa na mama wa kambo.
  Tofauti na ilivyo ada kwa jamii nyingi za Kitanzania kwamba wakati wa mavuno jamii nzima katika familia tangu watoto, wanawake na wanaume huwa na kipindi cha furaha, hali ni tofauti katika wilaya ya Newala kwani hicho ni kipindi cha majuto na maumivu kwa wanawake na watoto.

UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAKWAMISHA MAENDELEO NCHINI



Na Ramadhan Libenanga
Kasi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea inaweza kurudi nyuma miaka mitano ijayo, iwapo hatua thabiti hazitachukuliwa kupunguza kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

SIMBA, YANGA ZAINGIZA MIL.500/-



Na Fatuma Rashid

  Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3, imeingiza sh.milioni 500,727,000.

TFF WAPANGUA RATIBA LIGI KUU



Na Fatuma Rashid
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.

JK AMLILIA NYAISANGA, KUAGWA LEO LEADERS’ CLUB



  Rais Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi katika kuomboleza kifo cha mtangazaji mkongwe nchini aliyekuwa Meneja wa Kituo cha Abood Media, Julius Nyaisanga kwa jina maarufu Uncle J, anaripoti Mwandishi Wetu.

21 October 2013

CUF YAMTEGA ZITTO KABWE



  •  WAIPINGA PAC,WAJIPANGA KUCHUKUA HATUA
  • WATISHA KUSUSIA KIKAO CHAKE OKTOBA 25

Rachel Balama na Anneth Kagenda
  Chama cha Wananchi (CUF), kinatafakari hatua za kuchukua pamoja na kumuandikia barua Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda aweze kuzifunda Kamati za Bunge ili zitambue wajibu wake.Tamko la CUF linatokana na Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Zitto Kabwe, kuvitangazia kiama vyama tisa vya siasa vinavyopata ruzuku lakini vimeshindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa fedha.

JULIUS NYAISANGA AFARIKI DUNIA



Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
  Mtangazaji mkongwe na aliyekuwa Meneja wa Kituo cha Abood Media, mkoani Morogoro, Julius Nyaisanga kwa jina maarufu (Uncle J), amefariki dunia jana saa moja asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro

CHADEMA WAMLIPUA SITTA

  • WADAI AMESHINDWA KUJENGA BARABARA URAMBO


Na Goodluck Hongo, Urambo
 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kama kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015, watabadilisha matumizi ya Ofisi ya Spika iliyojengwa na mbunge wa Urambo Mashariki, Bw. Samuel Sitta.

BILAL ATOASOMO KWA WABUNGE SADC



 Jane Edward, Arusha
   Makamu  wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amelitaka Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kujadili suala zima la demokrasia kwenye chaguzi mbalimbali

CHINA KULETA WATALII 10,000 KILA MWAKA



Na Mwandishi Maalumu, SHENZEN, China
    China imeahidi kuleta watalii 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwakani.
Ahadi hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Wakala wa kutoa Huduma za Usafiri wa China na Hong Kong (China Travel Services Hong Kong Limited-CTS), Bw. Zhang Xuewu baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, jijini Shenzen, nchini China.

MUNGAI ATAKA VIBALI WALIMU WA NJE VIPUNGUZWE GHARAMA



 Na Rachel Balama
  Serikali imeshauriwa kufuta malipo ya vibali vya kazi kwa walimu wanaotoka nje ya nchi ili kuzisaidia shule hizo kutoa elimu bora na kutoathiri mapato na matumizi ya shule husika. Mwito huo ulitolewa Dar es Salam, mwishoni mwa wiki na aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai, katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ghomme ya Jijini.

WANANCHI WAONYWA UUZAJI HOLELA WA ARDHI



 Na Mwandishi Wetu, Korogwe
  Wananchi wa vijiji vya Kwagunda na Mnyuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, wameaswa kuwa makini na kutolaghaiwa kuuza ardhi yao mara baada ya kazi ya kupanga matumizi bora ya ardhi, kupimwa na kugawiwa hatimiliki katika maeneo yao kukamilika

MZEE KAWAWA ‘SIMBA WA VITA’ ALISIMAMIA KUANZISHWA JKT



Na Juma Kiyenze
.
  Mzee Rashid Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ ni mwanasiasa mkongwe alisimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu ya Serikali aliyokabidhiwa kwa nidhamu, uadilifu na bila woga hapa nchini.Hakika alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wazalendo, jasiri na mhimili mkubwa wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa harakati ya kupigania uhuru wa Tanganyika dhidi ya Wakoloni wa Uingereza.

RUSHWA IMETUPOFUSHA MACHO, TUNASUBIRI KUTUMBUKIA SHIMONI



Daniel Samson
"Dawa ya rushwa sio kulaumiana au kunyoosheana vidole na wengine kujiona watakatifu na rushwa haiwaathiri, lakini mapambano ha yanahitaji utashi na dhamira ya dhati kwa kila raia
"RUSHWA adui wa haki" ni msemo uliotumika sana na mwasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere katika harakati zake za kupinga utoaji na upokeaji rushwa ambayo ililenga kupotosha haki na usawa miongoni mwa wananchi.

VIJANA MTAJI WA SIASA KUELEKEA UCHAGUZI 2015



Adolf Mkono
‘‘ CCM wanaona jinsi wapinzani wao wanavyozidi kuimarika siku hadi siku na kujua matokeo halisi ya idadi za kura walizopata wao dhidi ya mpinzani wao na kuzifanyia kazi

  Harakati za kinyang'anyiro cha kiti cha urais mwaka 2015 kimekuwa kikivitesa vyama vya siasa na baadhi ya wanasiasa huku wananchi wakiendelea kutaabika kwa ukali wa maisha.Baadhi ya wanasiasa wamediriki kutamka wazi kuwa watagombea katika kiti hicho na kuzua malumbano kwa wananchi wao badala ya kusimamia shughuli za maendeleo kuwakomboa wananchi wao.

SIMBA, YANGA' NGOMA NZITO'



Na Elizabeth Mayemba

 Wakongwe wa soka nchini, Simba na Yanga jana zimetoka sare ya mabao 3-3 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

17 October 2013

VYAMA VYA SIASA VYAMSHUKIA ZITTO


  •  KILA CHAMA CHAMVAA KWA STAILI YA AINA YAKE
  • VYAMTAKA AACHE KULAZIMISHA KUTAFUTA UMAARUFU
Na Darlin Said

  Vyama vya siasa vya CCM, CUF na NCCR-Mageuzi vimemshukia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, kutokana na kauli yake ya kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi, kusitisha ruzuku kwa vyama hivyo kutokana na kushindwa kuwasilisha hesabu za fedha tangu mwaka 2009.

BAKWATA YAKUNWA KIKWETE KUKUTANA NA WAPINZANI IKULU

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu muda mfupi baada ya  kushiriki swala ya Idi iliyofanyika katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam jana asubuhi.


 Na Rachel Balama
  Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limempongeza Rais Jakaya Kikwete, kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni na kujadili maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya kwa amani na utulivu.

TMA YATOA TAHADHARI YA MAFURIKO NCHINI



 Na Penina Malundo
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imezitaka mamlaka husika kuchukua tahadhari kukabiliana na mafuriko yanayoweza kutokea msimu wa mvua ili kukabiliana na madhara ambayo yanaweza kusababishwa na mafuriko yakiwemo magonjwa ya mlipuko.

DAWA ZA KULEVYA CHANGAMOTO KWA TANZANIA, CHINA-BALOZI



Na Mwandishi Maalum, China
  Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhusiano na China, ambapo vijana wa Kitanzania 175 wapo katika magereza ya nchini humo, kutokana na makosa ya uhalifu yakiwemo ya kusafirisha dawa za kulevya.
Kauli hiyo ilitolewa na Balozi wa Tanzania nchini China , Abdulrahman Shimbo, wakati akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyewasili nchini humo jana kwa ziara ya kikazi.

HOSPITALI YA UPASUAJI WA MOYO KUJENGWA NCHINI



 Na Rachel Balama
  Hospitali ya Kimataifa ya upasuaji wa moyo inatarajiwa kujengwa nchini na Hospitali ya PARAS iliyopo nchini India baada ya kuvutiwa na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini Tanzania.

RAIS KIKWETE YUPO SAHIHI KUSAINI MSWADA WA KATIBA



Hamisi Kigwangalla

  Kama ningemshauri Rais Jakaya Kikwete hata kidogo tu kwenye hili la Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, ningemshauri aisaini sheria hiyo.

YANGA SC YAANZA MCHAKATO WA KAMPUNI



 Na Shaban Mbegu
  Klabu ya Yanga jana imetangaza kuwa ndiyo siku rasmi ya upigaji kura za maoni kwa ajili ya kuchagua timu hiyo iwe kampuni au kutokuwa kampuni.

KUZIONA SIMBA, YANGA ‘BUKU TANO’



Na Mwandishi Wetu
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mechi ya Simba na Yanga Ligi Kuu ya Vodacom itakayopigwa Jumapili Uwanja wa Taifa ambapo cha chini kitakuwa sh. 5,000.Kiingilio cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.

GHANA YAIADHIBU MISRI 6-1



KUMASI, Ghana
  Timu ya Ghana (Black Stars) juzi usiku iliiangamiza Misri, mabao 6-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda kucheza fainali hizo.

16 October 2013

RIPOTI: UTENDAJI WA UMESHUKA



  •  NI KUTOKA 90% hadi 70%, WATU 2,400 WATOA MAONI
  Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini nchini (REPOA), umebaini utendaji wa Rais Jakaya Kikwete, umepungua kutoka asilimia 90 mwaka 2008 hadi asilimia 71 mwaka 2012

UPINZANI WATINGA IKULU


 
Rais Jakaya Kikwete(kulia), akisalimiana na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Bw. Tundu Lissu baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mbunge wa Kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR- Mageuzi, Bw.James Mbatia. Viongozi wa vyama hivyo na CUF, walikwenda Ikulu kufanya mazungumzo na Rais Kikwete juu ya mchakato wa Katiba Mpya.  
  •  WAMUANGUKIA RAIS KIKWETE ASISAINI MUSWADA WA KATIBA

 Na Eckland Mwaffisi
   Rais Jakaya Kikwete, jana alikutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni ili kujadili maendeleo ya mchakato wa Katiba Mpya nchini.

WATU SITA KUNYONGWA HADI KUFA



 Na Suleiman Abeid, Shinyanga

  Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, imewahukumu washtakiwa sita adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kuwatia hatiani katika makosa ya kuua kwa kukusudia.

PAC YAZUIA RUZUKU VYAMA VYA SIASA




. David John na Frank Monyo

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji mstaafu Francis Mutungi, kusitisha utoaji wa ruzuku kwa baadhi ya vyama vya siasa kwa kushindwa kuwasilisha hesabu za ukaguzi wa fedha tangu mwaka 2009.

HAZINA YATUHUMIWA KUHUSIKA NA UFISADI



 Na Anneth Kagenda
  Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imesema katika utafiti wake kwenye halmashauri mbalimbali nchini, imebaini kuna mchezo mchafu unaofanywa ambapo vitendo vya ufisadi mkubwa vinaanzia Hazina.

MADAKTARI WATAKA UFOO SARO AACHWE APUMZIKE



 Leah Daudi na Fatuma Mshamu
  Maendeleo ya afya ya mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro, yameendelea kuwa siri yake na madaktari wanaomtibu hadi siku tatu zijazo ambapo ataruhusiwa kuonana na watu wanaotaka kumjulia hali.Hata hivyo habari zinaeleza kuwa hali ya mwandishi huyo imezidi kuimarika.

SIMBA SC, YANGA PRESHA INAPANDA, PRESHA INASHUKA


Na Mwandishi Wetu
  Wakati zikiwa zimebaki siku tatu watani wa jadi, Simba na Yanga washuke dimbani wachezaji na mashabiki wa timu hizo mioyo imekuwa ikidunda kutokana na presha ya mchezo huo.

LIGI KUU KUENDELEA TENA LEO



 Na Fatuma Rashid
  Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inaanza raundi ya tisa leo kwa timu ya Tanzania Prisons kushuka dimbani dhidi ya Ashanti United Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

TFF YATISHIA KUISHUSHA DARAJA YANGA



 Na Fatuma Rashid
  Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. milioni 5, baada ya baadhi ya viongozi wake kuzuia kituo cha Azam Televisheni kuonesha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar..

11 October 2013

MGOMO WASAFIRISHAJI :PINDA: MALORI, MABASI RUKSA

  •  AMTAKA MAGUFULI,WADAU KUFIKIA MWAFAKA
  • ARUDISHA MSAMAHA WA ASILIMIA TANO MIZANI
Na Darlin Said
 Waziri Mkuu , Bw. Mizengo Pinda , amesitisha utekelezwaji wa agizo la Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli la kuondoa msamaha wa tozo kwa uzito wa magari uliozidi ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubalika kisheria.

STK YANASWA KATIKA UTAPELI





 Gari yenye namba STK 3665 likiwa ndani ya kiwanda kimoja kilichopo Mbagala, Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) ambapo dereva wake alikamatwa akidaiwa kutaka kumtapeli mmiliki wa kiwanda hicho ambaye ni mteja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) juzi jioni.
 Na Mwandishi Wetu
   Jeshi la Polisi mkoani Temeke, linamshikilia dereva wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliyefahamika kwa jina la Bw. Samwel Mulagalazi, ambaye anadaiwa kushirikiana na watu wawili waliotaka kumtapeli mteja wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), sh. milioni 60

SUMAYE 'AWALIPUA' UPINZANI



 Na Andrew Ignas
  Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, amesema baadhi ya wabunge wa upinzani, wameugeuza ukumbi wa Bunge kama sehemu ya malumbano, matusi badala ya kujenga hoja ambazo zitachochea maendeleo kwa wananchi.

MAADHIMISHO YA MTOTO WA KIKE KUFANYIKA LEO



 Na Mwandishi Wetu
  Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe , leo anatarajiwa kuwa miongoni mwa washiriki wa mjadala mpana kuhusu njia za kumaliza tatizo la ndoa za utotoni , ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani.

10 October 2013

USALAMA ‘FEKI’ ANASWA MTEGONI




 Bw. Kennedy Magige, anayedaiwa kuwa Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ‘feki’ akiwa hoi baada ya kunaswa na kupata kipigo kutoka kwa wananchi. 


Kitambulisho cha Usalama wa Taifa, alichokuwa akitumia, Bw. Magige, kwenye majukumu aliyokuwa akijipangia


  Gari aina ya Land Cruiser Prado, alilokuwa akitumia wakati wa shughuli zake za kila siku.

  Bw. Magige na mtuhumiwa mwenzake wakiwa kwenye gari la Polisi tayari kupelekwa kituoni



 Na Mwandishi Wetu


 Watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli , huku mmoja akitumia kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.

WAKAMATWA NA ATM 243 ZA BENKI YA NMB



  Na Faida Muyomba, Geita

 Jeshi la Polisi mkoani Geita,limefanikiwa kuwakamata watu wawili wakiwa na kadi 243 za watu mbalimbali wilayani Chato, zinazotumika kutolea fedha kwenye ATM za Benki ya NMB kinyume cha sheria.

NGUVU ZA CHADEMA ZAMTISHA MANGULA


Na Mariam Mziwanda
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania (Bara), Philip Mangula ameshangazwa na chama hicho kuwa na ‘jeshi’ kubwa la wanachama, lakini linazidiwa nguvu na jeshi dogo la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hatua ambayo imemfanya aamke na kusoma alama za nyakati kwa kuwarudia wananchi.

WADAU WA HABARI WAMFUNGIA DKT. MUKANGARA, MWAMBENE


Na Rachel Balama
  Wadau wa habari hapa nchini wameazimia kusitisha kuandika , kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fennella Mukangara na Msemaji wa Serikali Assah Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

VIONGOZI WAWE MAKINI KUTOA KAULI,MAAMUZI YAO



Na  Alex Marwa


  Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wamekaririwa wakitoa kauli zenye mkanganyiko na maamuzi mbalimbali ambayo yameacha sintofahamu kwa wananchi.Kiongozi mzuri ni yule anayeheshimu utawala wa sheria na hivyo kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa ambazo yeye ana wajibu wa kuzisimamia wakati wa kutoa maamuzi mbalimbali, hususan yanayowagusa wananchi moja kwa moja.

09 October 2013

JK ATULIZA WAPINZANI



Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba (katika), akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, Dar es Salaam jana, kuhusu vyama hivyo kusitisha maandamano ya kupinga rais kusaini rasimu ya Muswada wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
  •  WASITISHA MAANDAMANO,WAKUBALI MEZA YA MAZUNGUMZO
  • JUKWAA LA KATIBA LAWAPA WOSIA,LATAKA WAWE NGANGARI

 Na Mariam Mziwanda
   Vyama vitatu vya siasa vinavyoshirikiana katika muungano wa kushinikiza k utokusaini wa kwa Muswaada wa Katiba vimeridhia kukutana na Rais Jakaya Kikwete, pamoja na kusitisha maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kesho.

TANI 205 ZA MCHELE MBOVU ZAKAMATWA




Na Mwajuma Juma, Zanzibar
   Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, imekamata tani 205 za mchele mbovu na dawa zilizopitwa na muda kwa matumizi binadamu.

MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA



 Na Gladness Theonest
   Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.

MOAT YATOA TAMKO KUFUNGIWA MAGAZETI



 Na Godfrey Ismaely

  Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT) kimemtaka Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara kuondoa adhabu kwa magazeti yaliyofungiwa yakiwemo Mwananchi, Mtanzania na Mwanahalisi bila masharti

MABASI YAGOMA KWA SAA SITA



Penina Malundo na Revina John
  Madereva wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani katika Kituo cha Ubungo, jijini Dar es Salaam jana yamegoma kwa takriban saa sita wakishinikiza Serikali kutowatoza faini ya asilimia tano ya uzito unaozidi kwenye magari yao yanapopimwa kwenye mizani.

NBC YAZINDUA PROMOSHENI YA 'WEKA UPEWE' NCHINI



Na Mwandishi Wetu
   Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi promosheni ya muda wa miezi mitatu ya kuweka akiba iitwayo 'Weka Upewe' itakayogharimu zaidi ya sh. milioni 300.Promosheni hiyo ina lengo la kuhamasisha wateja wake nchi nzima kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ikiwa ni moja ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC

TFF 'YAITUNISHIA MSULI' YANGA



Na Fatuma Rashid
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepinga hatua ya Klabu ya Yanga kuzuia mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara kuoneshwa na kituo cha Televisheni ya Azam Media Group.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Yanga hawana uwezo wa kuzuia mechi yoyote isioneshwe kwani mechi za Ligi Kuu zote zipo chini ya TFF.

SIMBA KUANIKA 'SILAHA ZA KUIUA' PRISONS



 Nasra Kitana na Shufaa Lyimo
    Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema leo anatarajia kuanika mikakati yake, ambayo ataitumia Jumamosi watakapocheza na Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari hizi jana kwa simu katika kambi hiyo iliyopo Bamba Beach, Dar es Salaam, Kibadeni alisema kiujumla timu inaendelea vizuri na mazoezi.