21 October 2013

BILAL ATOASOMO KWA WABUNGE SADC



 Jane Edward, Arusha
   Makamu  wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amelitaka Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kujadili suala zima la demokrasia kwenye chaguzi mbalimbali

  Alisema asilimia kubwa ya wananchi katika jumuiya hiyo, bado hawajui umuhimu wa kushiriki katika chaguzi hivyo kushindwa kutumia fursa ya demokrasia. 
  Dkt. Bilal aliyasema hayo jijini Arusha jana wakati akifungua Mkutano wa 34 wa Mabunge ya Nchi wanachama wa SADC, unaoendelea mjini humo na kuongeza kuwa, jumuiya hiyo inapaswa kuliangalia jambo hilo ili kuziepusha nchi zao katika majanga mbalimbali kama uvunjifu wa amani unaotokea katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu.
  Aliongeza kuwa, jumuiya hiyo ina nafasi kubwa ya kurudisha amani ya nchi ambayo wakati mwingine inapotea kwa kuwa wananchi hawajui umuhimu wa kupiga kura na kubuni mbinu mpya za kuwaelimisha wananchi .
  "Wananchi wanapaswa kujua umuhimu wa demokrasia hasa kwenye upigaji kura hivyo lazima waelimishwe, msikubali amani ya nchi zenu ipotee," alisema Dkt. Bilal.
  Alilitaka jukwaa hilo kuhakikisha linakuwa na hadhi ya Bunge kamili kama yalivyo mabunge mengine kwani kama litapata hadhi hiyo, litachangia ongezeko la wingi wa wanawake bungeni na kusaidia mambo yanayoihusu nchi husika.
  Awali Spika wa Bunge la Tanzania, Bi. Anne Makinda, alisema Tanzania bado ina uhitaji wa wabunge kutoka Viti Maalumu ili uwiano wa wabunge wanaume, wanawake uwe sawa hali ambayo itasaidia mabadiliko ya kiutendaji bungeni.
  "Changamoto iliyopo kwa wanawake nchini Tanzania bado hawajaweza kujitokeza kwa wingi na kushiriki chaguzi mbalimbali kwani bado wana dhana iliyojengeka kuwa wanawake ni viumbe dhaifu na waoga hivyo kusababisha wengi wao kubaki nyuma na kuwaona wanaume kuwa ndiyo wanaoweza pekee," alisema

No comments:

Post a Comment