22 October 2013

‘VIPODOZI VINACHANGIA UKOMA’



  Wanawake na wanaume wanaopenda kujichubua, wapo hatarini kupata ugonjwa wa ukoma kutokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, anaripoti Elizabeth Joseph, Dodoma

  Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma mkoani Dodoma, Dkt. Martin Massimba, aliyasema hayo mjini humo jana wakati akizungumza na Majira juu ya athari zitokanazo na matumizi ya vipodozi kwa wanawake na wanaume wanaopenda kujichubua.
  Alisema baadhi ya wanawake na wanaume wana tabia ya kutumia vipodozi vikali kwa kuvichanganya na kemikali nyingine ili waweze kujichubua.
  “Wote wanaofanya hivi wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa ukoma, vipodozi vingi wanavyotumia kuvichanganya vina kemikali nyingi zinazoweza kuharibu ngozi yao,” alisema.
  Aliongeza kuwa, watumiaji vipodozi wanapotokewa mabaka katika ngozi zao, hudhani y ame t o k a n a n a v i p o d o z i walivyotumia jambo ambalo si kweli, bali wengi wao waliopima, vipimo vimeonesha kuwa na ugonjwa wa ukoma.
  Dkt. Massimba alitoa wito kwa watu wote wanaopenda kutumia vipodozi vyenye kemikali kali, kuacha mara moja pia kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua kama wana maambukizi ya ugonjwa huo ambao huchukua muda mrefu hadi kujulikana

No comments:

Post a Comment