09 October 2013

SIMBA KUANIKA 'SILAHA ZA KUIUA' PRISONS Nasra Kitana na Shufaa Lyimo
    Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni amesema leo anatarajia kuanika mikakati yake, ambayo ataitumia Jumamosi watakapocheza na Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari hizi jana kwa simu katika kambi hiyo iliyopo Bamba Beach, Dar es Salaam, Kibadeni alisema kiujumla timu inaendelea vizuri na mazoezi.

  "Tupo tumetulia tunaendelea vizuri na mazoezi kuhakikisha Jumamosi tunatoka na ushindi," alisema Kibadeni.Vile vile aliongeza kuwa timu yake imeanza mazoezi Jumatatu, ambapo kila mchezaji ana morali ya hali ya juu."Tulianza mazoezi Jumatatu kwa ajili ya mchezo huo, ambao naamini utakuwa na ushindani mkubwa," alisema.Alisema mikakati hiyo, ambayo ataianika ni kwa lengo la kuchukua ubingwa mapema kabla Ligi Kuu haijamalizika.Simba inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 15.

No comments:

Post a Comment