29 October 2013

M23 WAUA ASKARI WA JWTZJeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema askari wake Luteni Rajabu Mlima, ameuwawa mjini Goma, Congo (DRC), baada ya kupigwa risasi wakati akitekeleza jukumu lake la ulinzi wa amani nchini humo, anaripoti Darlin Said.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari, ilisema Luteni Mlima alipigwa risasi na kufa Agosti 27 mwaka huu, mjini Goma.
“Tukio hilo lilitokea wakati wa mapambano kati ya jeshi la Serikali ya Demokrasia ya Congo na waasi wa M23,” ilisema taarifa hiyo.
  Iliongeza kuwa, Luteni Mlima akiwa na kikundi cha JWTZ kilichopo mjini humo, kilikuwa kinakwenda kukinga raia wasidhurike na mapigano hayo katika eneo la Kiwanja, kwenye Milima ya Gavana, nchini humo.

No comments:

Post a Comment