09 October 2013

MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA Na Gladness Theonest
   Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.

  "Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena maombi," alisema.
Alisema kilio chao amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.
  "Kama Bunge litaamua kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri sana kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi," alisema.
Alitaja sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa wataalamu.
  Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
  Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata

No comments:

Post a Comment