09 October 2013

TFF 'YAITUNISHIA MSULI' YANGANa Fatuma Rashid
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepinga hatua ya Klabu ya Yanga kuzuia mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara kuoneshwa na kituo cha Televisheni ya Azam Media Group.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Yanga hawana uwezo wa kuzuia mechi yoyote isioneshwe kwani mechi za Ligi Kuu zote zipo chini ya TFF.

  Wambura alisema mechi zote kama zitachezwa nyumbani, au ugenini zitarushwa na televisheni hiyo kwani walishakubaliana nao, lakini kama Yanga watakuwa wameandaa mechi yao isiyohusiana na TFF, watakuwa na uwezo wa kuzuia televisheni hiyo isioneshe.
  Alisema klabu zote zina haki zao na kama mtu atatumia bidhaa za klabu mojawapo vibaya, wanahaki ya kumshtaki.Aliongeza kuwa klabu yoyote, ili icheze Ligi Kuu inajulikana inatakiwa ipitie wapi ili ipate hadhi.Alisema hizi ni haki za matangazo na si za timu hivyo, Yanga wanatakiwa waliachie suala hili kwani ligi ni bidhaa ya TFF.

No comments:

Post a Comment