23 October 2013

LAAC: TUMEBAINI UBADHIRIFU URAMBO



   Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imebaini ufisadi mkubwa baada kupitia vitabu vya hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kwa mwaka 2011/2012 zinazoonesha sh. milioni 13.8, zililipwa mishahara kwa watumishi hewa, anaripoti Anneth Kagenda.

  Pia kamati hiyo imebaini halmashauri hiyo inadaiwa sh. milioni 138.3 na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF).Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajab Mbarouk Mohamed, aliyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hiyo, Dar es Salaam jana na kusisitiza kuwa, hali katika halmashauri ya Urambo si nzuri kwani fedha zimeliwa kwa kiwango cha juu.
  Alisema kamati yake pia imebaini sh. milioni 287 ambazo ni madai ya walimu na zaidi ya sh. bilioni moja ambazo zilitakiwa kupelekwa katika Mfuko wa Wanawake, Vijana na vijiji tangu kipindi hicho hazijapelekwa.
  Aliongeza kuwa, halmashauri hiyo ina miradi 26, ambayo kati ya hiyo, 11 ina dosari mbalimbali ambazo ni pamoja na kukosekana kwa stakabadhi zinazothibitisha mapokezi ya fedha husika.
“Tunaiagiza halmashauri hii pamoja na mambo mengine, iwachukulie hatua wote waliohusika na ufisadi wa fedha za mishahara hewa na kuhakikisha fedha zote ambazo hazijapelekwa kwenye mifuko husika, zinapelekwa haraka iwezekanavyo,” alisema

No comments:

Post a Comment