09 October 2013

TANI 205 ZA MCHELE MBOVU ZAKAMATWA




Na Mwajuma Juma, Zanzibar
   Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, imekamata tani 205 za mchele mbovu na dawa zilizopitwa na muda kwa matumizi binadamu.

Hayo yamebainishwa na Mrajisi wa Bodi hiyo, Dkt. Burhan Simai, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mnazi Mmoja wilaya ya mjini Unguja. Alisema kati ya tani hizo 205 mchele mbovu, tani 130 zimeingizwa nchini na kampuni ya UTS RICE kutoka Pakistan na tani 75 zimeingizwa na kampuni ya Inter Link kutoka Kenya.
Dkt. Simai alisema kwamba bidhaa hizo zilifanikiwa k u k ama twa kutokana na operesheni maalumu iliyofanywa na Bodi hiyo hivi karibuni na kukamata tende tani 3.4 zilizotoka Dubai. Akizungumza na waandishi wa habari alisema bidhaa zote hizo zinafanyiwa utaratibu wa kuangamizwa na baadhi kurejeshwa zilizotoka kwa gharama za wamiliki wa bidhaa husika
   Sambamba na hilo alisema kuwa kumejitokeza tabia kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa hawahifadhi vyema bidhaa zao na matokeo yake kuharibika mapema.
  Kuhusu uingizwaji wa dawa feki hapa nchini Mrajisi huyo alisema kwamba wameweka mtandao maalumu wa kuweza kugundua dawa hizo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika. Alisema kuwa wakati wa kusimamia sheria umefika kwani wa fanyabiashara wengi wamekuwa wakifanya udanganyifu kwa masilahi yao binafsi bila ya kujali afya za watumiaji.

No comments:

Post a Comment