17 October 2013

YANGA SC YAANZA MCHAKATO WA KAMPUNI



 Na Shaban Mbegu
  Klabu ya Yanga jana imetangaza kuwa ndiyo siku rasmi ya upigaji kura za maoni kwa ajili ya kuchagua timu hiyo iwe kampuni au kutokuwa kampuni.

Katika mkutano wa kawaida wa wanachama uliofanyika Januari 16 mwaka huu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji kwa niaba ya Kamati ya Utendaji alitoa mapendekezo kwa wanachama juu ya timu kuwa kampuni.
Katika mapendekezo hayo, Mwenyekiti huyo aliwaeleza wanachama juu ya umuhimu wa kampuni na kuwataka kutafakari kwa makini juu ya jambo hilo. Pia aliwaeleza kuhusu kuwepo kazi ya kupiga kura za maoni, ili kuweza kuona mawazo ya wanachama ambao ndiyo wenye klabu hiyo wanasemaje juu ya jambo hilo.
Kaimu Katibu Mkuu wa timu hiyo, Lawrence Mwalusako akizungumza katika mkutano wa waandishi uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo, alisema kuwa hiyo ndio siku rasmi kwa ajili ya kazi hiyo.Alisema kila mwanachama ambaye yupo hai ataruhusiwa kupiga kura, lakini atalazimika kufika na kadi yake ili kuepuka na wajanja watakaotaka kurudia mara mbili.
“Nachukua nafasi hii kuwaambia wanachama wa Yanga, kuanzia leo tarehe 16 mpaka Novemba 10 mwaka huu, kutakuwa na sanduku moja hapa klabuni kwa ajili ya kura za maoni,” alisema.Alisema kutakuwa na kura za aina mbili, za kukubali kuwa kampuni zitakuwa kwenye karatasi iliyoandikwa (NDIYO) au (HAPANA) kwa wale wasiotaka kuwa kampuni.
Katibu huyo alisema viongozi wameona watumie busara katika kufanikisha jambo hilo na ikumbukwe kuwa shughuli hiyo ni muhimu kwa ajili maendeleo ya Yanga.Ak i z u n g umz i a k u h u s u wanachama wa mikoani kama wa t awe z a j e k u p i g a k u r a , Mwalusako alisema itakuwa ni jambo gumu kwa wao kwenda kila mkoa.
Akifafanua kauli hiyo alisema kuwa watu wa mikoani si ‘watata’ kama ilivyo wa Dar es Salaam, pia viongozi na waasisi wa timu hiyo wapo jijini.“Unajua hapa ngoja niwe muwazi, Dar es Salaam ndiyo kuna watu watata ambao kama hujaenda nao sawa na kuwaelesha vizuri inaweza kuleta tatizo kubwa.
“Kuna kama hawa wazee wetu, wengi ndiyo wenye Yanga, wanaijua kiunaga ubaga kuanzia tangu ilipoanzishwa mpaka leo, sasa hawa ndiyo kila kitu kwa kweli,” aliongeza.Lakini Mwalusako alienda mbali na kudai kuwa watu wengi wa mikoani watapata fursa hiyo kupitia mchezo wao na Simba utakaopigwa Jumapili ijayo.
  “Tulisubiri mpaka kuelekea pambano la watani wa jadi, ndiyo zoezi hili (shughuli) lianze kwa kuwa tunaamini kuna wanachama wengi watakuja kuangalia mchezo huo na hiyo itakuwa fursa kwao kupiga kura za maoni,” alisema.Akizungumzia maandalizi ya mchezo wa Jumapili, Mwalusako alisema wao kama viongozi wamemaliza kila kitu kwa ajili ya mchezo huo.
  Mchezo huo wa mzunguko wa tisa utapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba yenyewe imejificha Bamba Beach Kigamboni nje kidogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mchezo huo wa kihistoria.
  Mwalusako ambaye ni beki wa zamani wa timu hiyo, alisema kilichobaki kwa sasa ni kazi ya benchi la ufundi la timu hiyo kumaliza kazi iliyobaki.“Sisi kama uongozi tumemaliza kazi yetu kwa asilimia kubwa, benchi la ufundi ndiyo limebaki na jukumu la mwisho kwa ajili ya kuandaa timu hiyo,” alisema.
  Aliongeza kuwa mchezo huo utakuwa ni mgumu japokuwa wana imani na kikosi chao kuibuka na ushindi katika mchezo huo kutokana na kuwa na wachezaji bora.“Tuna kikosi bora na kizuri, pia tumejiandaa vizuri, naamini utakuwa mchezo mgumu, japokuwa tuna imani ya kushinda, lakini chochote kinaweza kutokea kwa kuwa soka ni mchezo wa bahati,” alisisitiza.
  Wakati huo huo, Meneja wa Yanga, Hafidhi Salehe amesema timu yao ipo vizuri tangu walipotua Pemba kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na mchezo wa mahasimu zao Simba.Hafidhi alisema kwa sasa wanafanya mazoezi ya nguvu na jana walikwenda ufukwe wa Misali, ili kuwajenga wachezaji kuwa na nguvu pamoja na pumzi za kutosha.
  “Timu inaendelea vizuri na mazoezi leo jioni (jana), tunacheza na timu moja ya huku ikiwa ni sehemu ya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo, pia tunashukuru kwamba hatuna majeruhi katika kikosi chetu,” alisema.
Alisema wamefurahishwa na hali ya hewa ya Pemba kuwa ya utulivu, ambapo wachezaji wamekuwa na hamasa kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.
  S imb a n a Ya n g a z o t e zimeshacheza michezo nane, lakini wametofautiana kwa pointi tatu ambapo Wekundu wa Msimbazi ndiyo wanaongoza ligi kwa pointi 18, huku Yanga wakishika nafasi ya nne kwa pointi 15.

No comments:

Post a Comment