17 October 2013

GHANA YAIADHIBU MISRI 6-1



KUMASI, Ghana
  Timu ya Ghana (Black Stars) juzi usiku iliiangamiza Misri, mabao 6-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda kucheza fainali hizo.

  Mshambuliaji Asamoah Gyan alianza kuifungia Ghana bao la kwanza dakika ya tano,huku mchezaji wa Misri, Wael Gomaa akijifunga
dakika ya 21 akiwa katika harakati za kuokoa.
  Mohamed Aboutrika aliipatia bao pekee la penalti Misri dakika ya 41, huku Majeed Waris akiifungia Ghana bao lingine dakika ya 44.
  Kipindi cha pili kilianza kwa Ghana kuliandama lango la Misri ambapo, Gyan akafunga bao la tatu dakika ya 51.Kama haitoshi, Sulley Muntari aliifungia Ghana bao lingine dakika ya 72 kwa mkwaju wa penalti.
  Christian Atsu alihitimisha karamu ya mabao baada ya kuifungia Ghana bao la sita na kuifanya timu hiyo kujijengea mazingira mazuri ya kwenda Brazil.Timu hizo zinatarajiwa kurudiana nchini Misri,lakini haijajulikana itakapofanyikia kutokana na vurugu zilizopo Misri.

No comments:

Post a Comment