16 October 2013

RIPOTI: UTENDAJI WA UMESHUKA  •  NI KUTOKA 90% hadi 70%, WATU 2,400 WATOA MAONI
  Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini nchini (REPOA), umebaini utendaji wa Rais Jakaya Kikwete, umepungua kutoka asilimia 90 mwaka 2008 hadi asilimia 71 mwaka 2012
.Idadi ya Watanzania wanaotaka Rais awajibike kwa Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, inazidi kuongezeka ambapo mwaka 2012, zaidi ya asilimia 55 walipendekeza awajibike.
Matokeo ya utafiti huo yaliyowasilishwa Dar es Salaam jana, yalikusanya maoni ya watu juu ya utendaji wa Rais, Bunge, Mahakama na kupewa jina la "Afro Barometer".
Akiwasilisha matokeo hayo, Mtafiti Msaidizi wa ripoti hiyo, Stephen Mwombela, alisema utafiti umebaini imani ya Watanzania dhidi ya utendaji wa Rais Kikwete, Baraza lake la Mawaziri na Bunge la Jamhuri ya Muungano, inazidi kudorora.
Alisema utafiti huo ulikusanya maoni ya watu 2,400 nchi nzima kipindi cha Mei hadi Juni 2012 ambapo watoa maoni ni watu wenye umri kuanzia miaka 18, wenye elimu tofauti na wasio na elimu.
"Pamoja na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, mhimili wa mahakama, bado imani yake kwa wananchi ni kubwa na imezidi kuongezeka ukilinganisha na Serikali, Bunge," alisema.
Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa ripoti hiyo asilimia 84 ya Wazanzibari bado wanaamini utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema watu wengi waliokosoa utendaji wa Rais ni wenye elimu kuanzia sekondari na kuendelea ambapo mwaka 2008, utendaji wa Rais uliungwa mkono wakati mwaka 2012, asilimia 60 tu, ndio waliounga mkono.
Ripoti hiyo pia imeonesha asilimia 70 ya Watanzania waishio mijini, wanaamini Rais anafanya kazi yake kwa ufasaha sawa na anguko la asilimia 19 ambapo mwaka 2008 ilikuwa asilimia 89.
Alisema wananchi waishio vijijini, mambo si mazuri kwani idadi ya wanaopinga utendaji wa Rais imeongezeka kutoka asilimia 8 mwaka 2008 hadi 26 mwaka 2012.
Upande wa Bunge, matokeo ya utafiti yanaonesha asilimia 61 ya Watanzania hasa wasio na elimu bado wanaamini Bunge linafanya kazi yake kwa umakini.
  Aliongeza kuwa, hali hiyo inaonesha imani dhidi ya utendaji wa Bunge, inazidi kushuka ambapo mwaka 2008, asilimia 65 ya Watanzania waliamini kwamba Bunge linawajibika ipasavyo.
  Mtokeo hayo yameonesha kwamba, mwaka 2012 asilimia 61 tu ya Watanzania waishio Bara wana imani na Bunge na Visiwani Zanzibar ni asilimia 64.
  Ak i z u n g umz a b a a d a y a kutangazwa kwa matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa PEROA, Profesa Samwel Wangwe, alisema matokeo hayo yana ujumbe kwa Serikali ili iweze kuwaelimisha wananchi matarajio ya kijamii na kiuchumi.
 "Watanzania wanatakiwa kuelezwa nini maana ya utendaji wa Rais na Bunge, naamini haya ni mawazo ya wananchi," alisema na kuongeza kuwa, viongozi wanatakiwa kuwajibika katika nafasi zao ili kurudisha imani kwa wananchi.
  Alisema utafiti wao utaendelea kuboreshwa kila mwaka kwa kufanyika nchi nzima ili kuhakikisha sauti za watu zinasikika; hivyo lazima kila kiongozi awajibike katika nafasi yake.
  Upande wa Mahakama, matokeo yanaonesha wanaopinga utendaji wake idadi yao imepungua kutoka asilimia 26 mwaka 2008, hadi 25 mwaka 2012.
Wananchi waishio vijijini ndio wanaongoza kwa kuwa na imani kubwa na makahama kwa asilimia 77, waishio mijini ni asilimia 70 tu.
 "Ni kawaida kuona kila Serikali mpya huwa na imani juu ya wananchi wake na muda unavyokwenda, mambo hubadilika," alisema Dkt. Jonas Kipokola, ambaye ni mtafiti na mtumishi mstaafu wakati akitoa maoni yake kuhusu ripoti hiyo.
 Aliongeza kuwa; "Kuongezeka au kupungua kwa imani ya watu kwa Serikali yao, inategemea ni namna gani Serikali inavyowasiliana na watu wake na kujenga mtazamo gani.
"Nadhani tungeyatumia matokeo ya tafiti hizi kuisukuma Serikali ifanye kazi yake vizuri ili kutimiza matakwa na imani ya wananchi," alisema. Naye Bw. Victor Kimesera, ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliukosoa utafiti huo na kudai kuwa, hauoneshi hali halisi ya mambo.
 "Tunajua uelewa wa watu dhidi ya utendaji wa mihimili ya nchi bado ni mdogo sana...ripoti haioneshi hali halisi ya mambo," alisema baada ya kuwasilishwa ripoti hiyo.
  Aliongeza kuwa, Watanzana wengi hawajui wajibu wa mbunge na kuitaka Serikali, ione umuhimu wa kuboresha elimu, kuhakikisha tafiti kama hizo zinatoa majibu halisi ya matatizo ya Watanzania.
 "Naamini kuanzia mwaka 2005, imani ya Watanzania juu ya Rais Kikwete ilikuwa kubwa ndiyo maana tafiti zilionesha imani kubwa juu yake imeanza kushuka," alisema.
  Naye Dkt. Abel Kiyondo, alisema Bunge lipo kwa ajili ya kutetea wananchi lakini kwa Bunge la Tanzania, halipo kwa ajili ya wananchi bali linawakilisha vyama vyao

No comments:

Post a Comment