23 October 2013

KAMANDA JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA    

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), mstaafu James Kombe (pichani) amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam, anaripoti Frank Geofray-Jeshi la Polisi

   Akizungumzia kifo hicho, Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso alisema, Kombe alifariki hospitalini hapo jana ambapo taratibu za mazishi zinaendelea. Alisema marehemu alizaliwa mwaka 1950, Mwika mkoani Kilimanjaro, alijiunga na Jeshi la Polisi Machi 15,1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda, kupandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.
Baadhi ya vyeo alivyopitia na miaka aliyopata vyeo hivyo katika mabano ni Sajenti wa Polisi (1973), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977), Mkaguzi wa Polisi (1984) na Mrakibu Msaidizi (1986).Vingine ni Mrakibu wa Polisi (1991), Mrakibu Mwandamizi (1995), Kamishna Msaidizi wa Polisi (1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2002), hadi alipostaafu mwaka 2010.
Baadhi ya nafasi alizowahi kuzitumikia jeshini ni pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) katika Wilaya za Dodoma, Tarime, Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi Mkoa (RPC) katika mikoa ya Lindi, Arusha na Kigoma. Pia marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (FFU

No comments:

Post a Comment