22 October 2013

AANGUKA, AFA AKITOA USHAHIDI KORTINI  Mkazi wa Kijiji cha Bitale, Wilaya ya Kigoma Vijijini, amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akitoa ushahidi kwenye Mahakama ya Mwanzo, iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma, anaripoti Mwajabu Kigaza, Kigoma.

  Tukio hilo limetokea Oktoba 17 mwaka huu, saa nne asubuhi na marehemu amefahamika kwa jina la Yusuph Kazirai (65).Akizungumzia tukio hilo, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Bw. David Ngunyale, alisema marehemu alikuwa mlalamikaji katika kesi ya jinai namba 94 ya mwaka 2013.
  Alisema wakati marehemu akitoa maelezo yake juu ya kesi hiyo mbele ya mahakama, ghafla alianza kuishiwa nguvu, kuanguka chini ambapo baada ya kuwahishwa hospitali na kufanyiwa vipimo, ilithibitika tayari amefariki dunia.

No comments:

Post a Comment