29 June 2012
ULIMBOKA WODINI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Madaktari Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka, akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) cha Hospitali ya Muhimbili akitibiwa baada ya kupigwa na watu wasiojulikana waliomteka juzi. (Na Mpigapicha Wetu)
Ulimboka sasa aitesa Serikali *Yashindwa kutoa tamko la waliogoma *Madaktati ICU wapigania maisha yake
Na Waandishi Wetu, Dodoma, Dar
SERIKALI imekiri kuchanganywa na tukio la kutekwa na kujeruhiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, jana alishindwa kutoa tamko la Serikali kuhusu madaktari waliogoma bungeni mjini Dodoma, kama alivyoahidi juzi.
USAJILI WATOTO
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Tanzania (RITA), Bw. Phillip Saliboko, akionesha moja ya vyeti vipya vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa vitakavyotumika kusajili watoto wote nchini walio chini ya umri wa miaka 5. Usajili huo utafanyika hivi karibuni kuanzia ngazi ya mtaa, vijiji na vituo vya afya. Kushoto ni Meneja Usajili wa Wakala hiyo. Bi. Angella Anatory (Picha na Charles Lucas)
Dkt. Shein: Muungano utaendelea kudumu
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, amesema Muungano uliopo utaendelea kudumu ambapo wananchi wenye maoni kuhusu jambo hilo, waisubiri Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili watoe maoni yao..
Kizimbani kwa matumizi mabaya ya ofisi
Na Rehema Mohamed
WATUMISHI wawili wa Ofisi ya Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi, jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa mawili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka.
NGOMA ZA ASILI
Wasanii wa Kikundi cha Ngoma za Asili cha Jembe kutoka mkoani Dodoma wakiburudisha, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam juzi. Miradi mbalimbali ya maendeleo ilizinduliwa. (Picha na Charles Lucas)
Wateja wote TANESCO kuunganishiwa umeme
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema ifikapo kesho litakuwa limekamilisha kazi ya kuunganisha umeme kwa wateja wote walioomba kuunganishiwa nchi nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Mahusiano kwa Umma wa shirika hilo, Bi. Badra Masoud, alisema hatua ni inatokana na vifaa vyote muhimu kuwasili nchini katika ofisi za kanda.
Kesi ya UDA yakwama kusikilizwa
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilishindwa kupanga tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa wa kesi ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kulisababishia hasara Shirika la Usafirisha Dar es Salaam (UDA), sh. billion 2.3, kutokana na mshtakiwa wa pili kutokuwepo mahakamani.
CHADEMA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw Godbless Lema, akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala Dar es Salaam juzi, wakati wa Kampeni ya Ondoa CCM Dar es Salaam, ambapo pia chama hicho kilitoa tamko la kufanya maandamano ya kuunga mkono mgomo wa madaktari nchi nzima. (Picha na Sittu Athumani)
CHADEMA yajipanga kuandamana kupinga kupigwa Dkt.Ulimboka
Darlin Said na Tumaini Maduhu
CHAMA cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kimejipanga kufanya maandamo makubwa kupinga kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka.
Dkt. Ulimboka anadaiwa kutekwa usiku wa kumkia juzi na watu wasiojulikana.
HOSPITALI YA REGENCY
HOSPITALI ya Regency ya Dar es Salam imeanzisha program kabambe ya upasuaji wa maradhi mbalimbali ya tumbo kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kutumia kamera, ambapo mgonjwa hapasuliwi sehemu kubwa.
FIESTA
Mkuu wa Vipindi wa Redio Clouds, Sebastian Maganga (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta Super Nyota ambalo litaanza kufanyika katika mikoa mbalimbali hivi karibuni, katikati ni Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo(Picha na Victor Mkumbo)
Fiesta kufanyika katika mikoa 14
Na Victor Mkumbo
TAMASHA la burudani la fiesta, ambalo hufanyika kila mwaka kwa mwaka huu linatarajia kufanyika katika mikoa 14 ikiwa ni Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo, Mkuu wa Vipindi wa Clouds, Sebastian Maganga alisema tamasha hilo linatarajia kuwa la aina yake kwa mwaka huu.
Yanga yatema wachezaji 11 *Kujipima na Express ya Uganda kesho
Na Elizabeth Mayemba
KATIKA kuimarisha kikosi chake, uongozi wa Klabu ya Yanga umetema wachezaji 11 huku wengine wakipelekwa kwa mkopo katika timu nyingine.
Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema leo wanatarajia kuwasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), majina ya wachezaji ambao wameachwa na wale watakaotolewa kwa mkopo katika timu nyingine.
NGOMA ZA ASILI
Meneja wa bia ya Balimi, Edith Bebwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya ngoma za asili ambayo yataanza kufanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia kesho. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya TBL, Fimbo Buttalah. (Picha na Victor Mkumbo)
Bi. Kidude kupagawisha Temeke leo
Na Anneth Kagenda
NGULI wa muziki wa taarabu nchini, Kidude Binti Baraka 'Bi. Kidude', leo anatarajia kupagawisha wakazi wa Temeke katika shoo maalumu ya usiku wa taarabu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bi. Kidude alisema usiku huo utakuwa wa aina yake kwa kuwa amejipanga vya kutosha kuhakikisha anavurumisha burudani ya nguvu kwa mashabiki wa muziki wa taarabu.
28 June 2012
DKT. ULIMBOKA ATEKWA, APIGWA.Aokotwa msituni Mabwepande akiwa taabani.Afikishwa MOI,Serikali yaamua kutoa tamko
Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakilisukuma gari la wagonjwa namba T 151 AVD, baada ya kuwasili hospitalini hapo, likiwa limembeba, Dkt. Steven Ulimboka (picha ndogo), akiwa amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana na kutupwa kwenye pori la Mabwe Pande, Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)
Tunalaani unyama aliofanyiwa Ulimboka
WAKATI Serikali ikiendelea na jitihada za kuupatia ufumbuzi mgomo madaktari, ili umalizike bila kuathiri zaidi hali ya utoaji huduma katika hospitali zetu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, amejeruhiwa vibaya baada ya kutekwa nyara usiku wa kuamkia jana katika mazingira ya kutatanisha, jijini Dar es Salaam.
TUNAANDAA GAZETI
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Majira, Bw. Imma Mbuguni (kulia) na Msimamizi wa kamera, Bi. Zawadi Kiyungi (wa pili kulia), wakiwaonesha wanafunzi wa Kunduchi Girls Islamic High School, jinsi ya kuandaa gazeti kabla ya kuingizwa mitamboni, walipotembelea Makao Makuu ya gazeti hili, Mtaa wa Lugoda, Dar es Salaam jana. (Picha na Sittu Athuman)
Mbunge: CCM wanataka kuniua *Ushahidi wa majina yao kuwasilishwa bungeni
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Ilemela, mkoani Mwanza, Bw. Highness Kiwia (CHADEMA), amefichua mpango wa kutaka kumuua unaofanywa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jimboni humo.
Bw. Kiwia aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia hotuba ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.
MASHABIKI
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa makini moja ya mechi za robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Ulaya Euro 2012 kati ya Uingereza na Italia, Jumapili kwenye viwanja wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikionesha mechi za michuano hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. (Na Mpigapicha Wetu)
CHANETA yazitaka timu kuwasilisha usajili
Na Amina Athumani
CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kimezitaka timu zote zitakazoshiriki michuano ya Ligi Daraja la Kwanza ziwe zimesilisha fomu za usajili wa wachezaji kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika Agosti, mwaka huu jijini Mbeya na itashirikisha timu 20 zilizopanda daraja kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Business Times, Jeshi Stars uso kwa uso
Na Elizabeth Mayemba
TIMU ya netiboli ya Business Times LTD, inatarajiwa kucheza Jumapili na timu ya Jeshi Stars katika michuano ya Bandari Chalenji inayotarajia kuanza Jumamosi katika viwanja vya Klabu ya Habours Kurasini, Dar es Salaam.
TAMASHA
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana kuhusu tamasha la wasanii litakalofanyika kuanzia Juni 30 mwaka huu jijini Tanga. Kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam na kulia ni Mkurugenzi wa Sofia Records Mussa Kissoky (Picha na Victor Mkumbo).
Tamasha la filamu kufanyika Tanga
Na Victor Mkumbo
TAMASHA la Filamu la Tanzania Film Festival linatarajia kufanyika Juni 30, mpaka Julai 6 mwaka huu Jijini Tanga.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Consolata Adam alisema tamasha hilo linatarajia kuwa la aina yake kwa mwaka huu kutokana na maandalizi.
Mapya yaibuka kesi ya kusafirisha watu
Na Rehema Mohamed
UPANDE wa mashtaka kwenye kesi ya biashara haramu ya kusafirisha binadamu, umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa walalamikaji walisafirishwa kutoka Yemeni kuja Tanzania kwa msaada wa Shirika la Kimataifa Uhamiaji (IMO).
Viongozi wamejiuzia kiwanda cha korosho Mtwara –Mbunge
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalumu Bi. Christowaja Mtinda (CHADEMA), amesema baadhi ya viongozi serikalini, wamejiuzuia kiwanda cha kubangua Korosho cha Newala One, kilichopo mkoani Mtwara kwa sh. milioni 75 bei ambayo ni sawa na bure na kukigeuza kiwanda hicho kuwa ghala la kuhifadhia korosho.
Mramba, Yona wana kesi ya kujibu
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema washtakiwa wa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 11.7, akiwemo aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Basil Mramba, wana kesi ya kujibu.
TREKTA
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Bi.Christine Mndemw akiwasha moja ya trekta kati ya tisa zilizotolewa kwa mkopo kutoka Benki ya uwekezaji nchini (TID) kwa ajili ya wanachama tasa wa Saccos ya TAKAUMA iliyopo katoka kata ya Bassotu wilayani hapa.Wengine ni baadhi ya wananchi na viongozi ambao walifika kushuhudia makabidhiano hayo juzi.(Picha na Mary Margwe)
Mwanafunzi abakwa na mjomba wake
Na Abdallah Amiri, Igunga
JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Makomero, Kata ya Igunga Mjini, Bw. Nzogya Ramadhani (38), kwa kosa la kumbaka mtoto wa dada yake (jina linahifadhiwa), mwenye umri wa miaka 12, anayesoma darasa la tano katika Shule Msingi Makomero.
Uchaguzi Yanga ngoma nzito
Na Elizabeth Mayemba
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti katika Uchaguzi Mdogo wa klabu ya Yanga na Yono Kevella anayegombea nafasi ya Makamu na Ujumbe, wamewekewa pingamizi kwenye Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Simba kuwatoa kwa mkopo Machaku, Shamte *Jabu, Kago, mikataba yao imekwisha
Na Zahoro Mlanzi
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanika majina ya wachezaji walioachwa na waliositishiwa mikataba yao kwa timu mbalimbali huku Klabu ya Simba, itawatoa kwa mkopo Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura ilieleza kwamba mbali na hao pia wachezaji Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago na Juma Jabu wamemaliza mikataba yao wakati Salum Kanoni mkataba wake utamalizika Juni 30, mwaka huu.
Alisema timu hiyo imewasilisha majina ya wachezaji hao wanne ambao bado wana mkataba na timu hiyo wakiwa na lengo la kutaka wakaongeze viwango vyao.
"Mbali na Simba, pia Azam FC imekatisha mikataba ya wachezaji watatu ambapo ni Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Alisema Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17, wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya ligi msimu huu imeacha wachezaji 11.
Wambura alisema kwa upande wa Kagera Sugar, wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao na kwamba uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 na utamalizika Julai 30, mwaka huu wakati kipindi cha kuacha wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
27 June 2012
Waliofilisi Mashirika wanyongwe-Mbunge *Adai kama wamekufa makaburi yafungwe pingu *Ni TRL, ATCL na NIC, TAKUKURU lawamani
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, mkoani Rukwa, Bw. Ally Kessy (CCM), ameitaka Serikali iwachukulie hatua watumishi waliohusika kufilisi mashirika ya umma pamoja na kuwanyonga.
Alisema kama itabainika wahusika wameshatangulia mbele ya haki (kufa), makaburi yao yafungwe pingu kama ishara ya kukasirishwa na hujuma kubwa walizoifanyia nchi.
Vigogo 'wezi' watajwa *Wadaiwa kuhujumu mikoa ya kusini
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalumu, mkoani Lindi, Bi. Riziki Lulinda (CCM), amewataja kwa majina baadhi ya vigogo waliopo katika halmashauri nchini wanaodaiwa kufanya wizi wa mabilioni ya fedha na kuhamishiwa vituo vya kazi hali inayochangia kukwamisha maendeleo hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
TAKUKURU waingia Maliasili, Nishati
Na Stella Aron
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), inatarajia kuwaburuta mahakamani maofisa wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya rushwa katika Wizara ya Maliasili na utalii, Nishati na Madini pamoja na Idara ya Pembejeo kwa kuisababishia Serikali hasara.
Walioficha pesa Uswisi kuchunguzwa
Na Benedict Kaguo, Dodoma
WABUNGE wameitaka Serikali kufanya uchunguzi wa fedha zilizokamatwa nchini Uswisi sh. bilioni 300, kwenye akaunti za Watanzania sita wakiwemo wanasiasa.
Fedha hizo zinadaiwa kuingizwa katika akaunti hizo na Kampuni za uchimbaji mafuta na madini zilizopo nchini.
MOI waelemewa
Na Waandishi Wetu, Dar na mikoani
UONGOZI wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umekiri mgomo wa madaktari kuathiriwa utoaji huduma za matibabu na kulazimika kutoa huduma za dharura pekee kwa kuwatumia madaktari bingwa.
Ratiba ukusanyaji maoni Katiba Mpya yatolewa
Na Reuben Kagaruki
TUME ya Mabadiliko ya Katiba, inatarajia kuanza kufanya mikutano na wananchi wa mikoa nane kuanzia Julai 2-30 mwaka huu ili kukusanya maoni yao.
Mikoa hiyo ni Dodoma, Kagera, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Manyara, Pwani, Shinyanga na Tanga. Katika Mkoa wa Dodoma, tume itaanza na Wilaya ya Bahi.
Wafugaji walia njaa Ngorongoro
Na Pamela Mollel, Arusha
JAMII ya wafugaji wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha imeelezwa kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula wamefikia hatua ya kuhama ovyo makazi yao.
Pia wananchi hao wameitaka serikali kuwarudishia kilimo chao cha viazi ambacho awali walikuwa wanalima katika Tarafa ya Ngorongoro ili waweze kujikimu katika suala la chakula badala ya kutegemea serikali na chakula chake cha msaada.
KUMBUKUMBU
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Ban Ki-moon akipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (kushoto),Waziri wa Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar Bi.Ftma Freji (wa pili kushoto) wakati alipokuwa katika hafla ya chakula cha jioni,iliyoandaliwa na Rais wa Brazil kwa viongozi waliohudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20)uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil.(Picha na OMR)
Kibanda, wenzake wasomewa maelezo ya awali
Na Grace Ndossa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana iliwasomea maelezo ya awali Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Bw. Absalom Kibanda, mwandishi Bw. Samson Mwigamba na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Bw. Theophil Makunga.
Mwanafunzi abakwa, kuuawa kikatili
Na Theonestina Juma, Bukoba
MWANAFUNZI wa kike anayesoma kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Kaagya, mkoani Kagera, Advea Makanyaga (16), ameuawa kikatili kwa kunyongwa shingo, kuvunjwa taya kwenye shavu la kulia, kubakwa na mwili wake kutupwa shimoni.
TAMASHA
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Shetta pamoja na madansa wake wakiwaburudisha wakazi wa Morogoro wakati wa Tamasha la”WAJANJA”lililofanyika mjini humo,Tamasha hilo linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,litaendelea katika mikoa ya Mtwara na Tanga likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano na kutumia facebook na twitter bure.
Kesi ya Hassanoo yapigwa kalenda
Na Grace Ndossa
KESI inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), Hassan Othman 'Hassanoo' na wenzake wawili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirishwa hadi Julai 27 mwaka huu.
Kesi hiyo iliahirishwa mahakamani hapo jana baada ya Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, Devotha Kisoka kujitoa kutokana na kuwa na majukumu mengine na kuikabidhi kwa Hakimu Theopili Mutakyawa.
El Merreikh, Red Sea zakwama Kagame Cup
Na Mwandishi Wetu
TIMU za El Merreikh ya Sudan na Red Sea ya Djibouti, zimeshindwa kuthibitisha ushiriki wao mpaka sasa katika michuano ya Kombe la Kagame.
Michuano hiyo imepangwa kuanza kutimua vumbi Dar es Salaam kuanzia Julai 14 mpaka 29, mwaka huu ambapo Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Yondani 'out' siku mbili Yanga *The Express kupima vifaa vipya
Na Zahoro Mlanzi
BEKI mpya wa mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga, Kelvin Yondani atakosa mazoezi ya siku mbili kutokana na kuwa na udhuru huku viungo Nurdin Bakari na Nizar Khalfan wameumia mazoezini.
Mbali na hilo, timu ya The Express kutoka Uganda inatarajiwa kutua nchini Jumamosi kwa ajili ya kuwapima wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali.
26 June 2012
Mbunge atoa mpya bungeni *Pinda apiga marufuku magari ya kifahari *Lengo ni kupunguza matumizi serikalini
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Ludewa, Bw. Deo Filikunjombe (CCM), ameshauri fedha za rada zilizorejeshwa nchini na Serikali ya Uingereza, zitambulike kama “Rushwa ya Rada”, badala ya chenji ya rada.
Bw. Filikunjombe aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma baaada ya kuomba mwongozo wa Spika wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia, akiwasilisha mapitio ya kazi kwa mwaka wa fedha 2011/12 na mwelekeo wa kazi kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Waislamu wakubali kushiriki sensa *BAKWATA: Itasaidia kuchochea maendeleo
Na Salim Nyomolelo
BARAZA la Waislamu nchini (BAKWATA), limewataka Waislamu wote kuungana na wananchi wengine kushiriki Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu nchi nzima.
Shekhe Mkuu wa Tanzania, Shaaban Idd Simba alitoa wito huo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko lililotolewa hivi karibuni na Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu linalowataka Waislamu kutoshiriki sensa.
MSINGI
Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa, Bw. Zumo Makame (aliyeinama ndani ya mtaro) akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata kama moja ya kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi ili kupunguza gharama za ujenzi wa Ofisi hiyo.Wengine ni baadhi ya wananchi wakishirikiana pamoja.(Picha na Ramadhan Libenanga)
Hukumu ya Malanda wizi wa bil. 2.2/- kutolewa leo
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa sh. bilioni 2.2 za Akaunti ya Madfeni ya Nje (EPA), iliyopo katika Benku Kuu (BoT), inayomkabili kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Rajabu Maranda na binamu yake Bw. Farijala Hussein.
Washtakiwa hao tayari wanatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa sh. bilioni 1.8 za EPA, katika mahakama hiyo na kuhukumiwa Mei 23,2010.
Wagonjwa waanza kutolewa hospitali
Stella Aron na Rehema Maigala
MGOMO baridi wa madaktari ulioanza Juni 23 mwaka huu, katika baadhi ya hospitali nchini, umeanza kushika kasi na kusababisha baadhi ya ndugu kuhamisha wagonjwa wao baada ya kukosa huduma za matibabu.
Wakizungumza na Majira Dar es Salaam jana, baadhi ya ndugu wenye wagonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), walisema kama mgomo huo utaendelea, utasababisha wananchi wengi kupoteza maisha kwa kukosa huduma.
Mganga wa kienyeji ajipaka kinyesi polisi
Na Said Hauni, Lindi
MKAZI wa Kijiji cha Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, Bw. Abdurahamani Makame, ambaye ni mganga wa kienyeji maarufu “Daktari Majoka”, mwishoni mwa wiki aliharibu hali ya hewa kwenye Kituo cha Polisi mjini Lindi baada ya kujipaka kinyesi mwilini.
Majambazi wavamia TCU, waiba
Stella Aron na Rehema Maigala
KUNDI la watu wanadhaniwa kuwa majambazi, wamefanya uporaji wa mali mbalimbali katika ofisi za Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), baada ya kuwalewesha walinzi wa Kampuni ya Bulwark kwa kuwapa chakula kinachosadikika kuwa na dawa za kulevya.
YANGA WAKIJIFUA
Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi mepesi kando ya ufukwe wa Bahari ya Hindi, Dar es Salaam jana, kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14, mwaka huu. (Na Mpigapicha Wetu)
Amchinja mkewe kwa wivu wa mapenzi
JESHI la Polisi mkoani Dodoma, linamshikilia, mkazi wa Morisheni, Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, Bw. Daniel Lusega (42), kwa tuhuma ya kumchinja mke wake na kumuua.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Zelothe Stephen, alisema tukio hilo limetokea Juni 25 mwaka huu, saa mbili asubuhi, katika eneo la Morisheni Kata, wilayani hapa.
DPP kufikishiwa jarada maiti iliyopotea
Rehema Maigala na Stella Aron
SAKATA la maiti ya mtoto mchanga iliyopotea katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam, limechukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi kulifikisha suara hilo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Eliezer Felesh, kwa uchunguzi zaidi.
Familia iliyopotelewa na maiti hiyo, imechukua uamuzi wa kufungua kesi ya madai kutokana na utata wa suala hilo.
MSAADA WA MAJI
Wachezaji gofu watakiwa kuchangamkia Kenya Open
Na Mwali Ibrahim
CHAMA cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU) kimewataka wachezaji wa mchezo huo kujitokeza kushiriki katika mashindano ya Kenya Open yanayotarajiwa kufanyika Juni 30 hadi Julai Mosi mwaka huu nchini Kenya.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa chama hicho Mbonile Barton alisema hiyo ni nafasi nzuri kwa wachezaji kuweza kujiongezea kiwango na kujitathimini hatua waliyofikia kimchezo.
TBL yajivunia tuzo ya dhahabu
Na Mwandishi Wetu
TUZO ya dhahabu ya kimataifa iliyochukuliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Ndovu Special Multi, imewasili nchini juzi huku kampuni hiyo ikijivunia mafanikio ya bia hiyo kwa kutwaa mara mbili mfululizo.
Sakata la umri wa Lulu,serikali yakimbilia mahakama ya Rufani
Na Rehema Mohamed
UPANDE wa mashitaka katika suala la utata la umri wa Msanii maarufu wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' umewasilisha mahakama ya Rufani maombi ya kuitaka mahakama hiyo ipitie upya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukubali kusikiliza utata wa suala hilo.
Timu ya Kivule veteran yapata vifaa
Na Peter Mwenda
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa ametoa mipira na jezi kwa ajili ya timu ya veteran ya Kata ya Kivule, wilaya ya Ilala.
Akikabidhi vifaa hivyo mwakilishi wa mbunge huyo Ali Mwaiposa alisema amefurahi kuona wachezaji wa zamani wanarudi uwanjani kuweka afya zao vizuri.
Milovan atua na mbinu mpya Simba *Vifaa vipya hadharani leo
Na Elizabeth Mayemba
KOCHA Mkuu wa Simba Mserbia Cirkovik Milovan tayari amewasili nchini usiku wa kuamkia jana, na leo ataanza rasmi mazoezi kwa timu yake kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14, mwaka huu.
25 June 2012
BIASHARA NA MAOMBI
Wana maombi kutoka Sweden, Bi. Danes Kendes (kulia) na mwenzake, Bw. Devis Frankline (kushoto),
wakimfanyia maombi, mfanyabiashara ndogondogo wa ndizi (ambaye jina lake halikupatikana), kando ya Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es Salaam jana. Wana maombi hao wako nchini Tanzania kushiriki mkutano wa ishara na miujiza. (Picha na Anna Titus)
BAADA YA KUKACHA BAJETI Mbunge CCM apasua jipu *Asema hawezi kufunga mdomo hadi kieleweke *Awataka wabunge wote wamuunge mkono
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Kisesa, Bw. Luhaga Mpina (CCM), amefichua siri iliyomfanya atoke nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati mchakato wa kupiga kura za kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13 ukiendelea.
Bw. Mpina ndiye mbunge pekee wa CCM, aliyetangaza ndani ya bunge dhamira yake ya kutoiunga mkono bajeti hiyo kutokaana na sababu mbalimbali.
MTOTO ALIYEIBWA
Wazazi wa mtoto aliteibwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Bi. Modesta Sumbuko (26) na mume, Bw. Emmanuel Matheo (28), wakazi wa Kijiji cha Butende, Kahama wakiwa na mtoto wao mchanga wa siku 5, aliyeibiwa wodini hivi karibuni baada ya kujifungua kwa Operesheni. Kichanga hicho kilibiwa na Bi. Pili Benard (28), aliyekamatwa nacho kwa mganga wa jadi, Bi. Jane Mbalamwezi (54), wa Kata ya Isaka, kilomita 45 kutoka mjini Kahama. (Picha na Patrick Mabula)
Dkt. Mwinyi: Mgomo wa madaktari upo *Atangaza kiama cha kuisafisha MSD, ATME watoa tamko
Na Benedict Kaguo, Dodoma
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Hussein Mwinyi, amekiri kuwepo mgomo baridi wa madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), na Hospitali ya Rufaa mkoani Dodoma.
Alisema hali katika hospitali nyingine nchini, huduma za matibabu zinaendelea kutolewa kama kawaida.
Padri Mapunda aihadharisha CCM
Goodkuck Hongo na David John
UGUMU wa maisha unaowakabili Watanzania wengi ni kielelezo kuwa nchi ipo katika hali mbaya hivyo nafasi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kutawala ipo mashakani.
Padri Baptiste Mapunda ambaye pia ni Mkurungenzi wa Shirika la Farijika la Afrika Mashariki, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa mahubili kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kalori Lwanga, lililopo Yombo, wilayani Temeke.
MSISITIZO
Mbunge wa jimbo la Ilala,Bw. Musa Zungu (katikati) akisisiza jambo katika mkutano wa hadhara na wananchi Kata ya Upanga Mashariki (hawapo pichani), Dar es salaam jana, Kulia Bi. Rukia Ryami ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa waKibasila,wa nne kutoka kushoto ni Diwani wa kata hiyo Bw.SultanSalim na kulia kwake Bw.Mathias Manyemba ambaye ni Katibu Tarafa Kat ya Kariakoo.Picha na Anna Titus
RC: Halmashauri hakikisheni hati chafu zinakoma
Na Allan Ntana, Tabora
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Bi. Fatuma Mwassa, amezitaka halmashauri mkoani hapa kuhakikisha hazipati hati chafu kuanzia mwaka wa fedha ujao.
Alisema hati chafu zinachangia kuleta mashaka ya utendaji kazi wa watumishi katika halmashauri husika na kuharibu sifa zao.
Wafanyabiashada dawa za kulevya sasa kukiona
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
SERIKALI inakusudia kufanya marekebisho ya sheria inayowapa dhamana wafanyabiashara wa dawa za kelevya nchini badala yake watafungwa jela ili kudhibiti mianya ya biashara hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. William Lukuvi, aliyasema hayo mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani inayofanyika Juni 26 kila mwaka. Mwaka huu kitaifa itafanyika Tandale, Dar es Saalam.
Polisi atuhumiwa kuiba gari
Na Peter Ringi, Manyara
JESHI la Polisi mkoani Manyara, linawashikilia watu wawili akiwemo askari polisi Bw. Greison Gasper (26), mwenye namba PC G3629 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), na mwenzake ambaye ni muosha magari Bw. Gabriel Alois (28), kwa tuhuma za kuiba gari aina ya Nissan Terano, yenye namba T993 ASX, mali ya Bw. Mstafa Athuman.
WANAHISA
Wanahisa wa Benki ya CRDB walioshiriki Mkutano Mkuu wa 17, wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Dkt, Charles Kimei (hayuko pichani), wakati akitoa taarifa ya mwaka 2011-2012, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa AICC Jijini Arusha juzi. (Picha na Peter Twite)
Wawili wafariki katika matukio tofauti Dar
Na Jesca Kileo
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam likiwemo la mtoto mdogo kuuungua na moto.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Komba, alisema tukio hilo limetokea Juni 23 mwaka huu, saa tano usiku eneo la Kigogo kwa Msafa, ambapo moto huo ulizuka ghafla katika nyumba ya Bw. Ramadhani Ramadhani.
INUKA yatoa mafunzo kwa wanachama wake
Na Grace Ndossa
TAASISI inayotoa Mikopo kwa Wanawake Wajasiriamali nchini (INUKA), imetoa mafunzo kwa wanachama wake kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
zitaigawa nchi, kuleta machafuko
Na Heri Shaaban
MBUNGE wa Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Philemon Ndesamburo, amesema misingi mibovu ya siasa za udini iliyowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), itaigawa nchi na kuleta machafuko.
Bw. Ndesamburo aliyasema hayo Dar es Salaam juzi katika mkutano wa kampeni ya “Ondoa CCM Dar es Salaam”, uliofanyika Tabata Kimanga.
CUF wataka ofisi ya Tendwa ichunguzwe
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kauli aliyotoa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa, kuwa atavifuta baadhi ya vyama vya mifukoni, inaudhi na kusikitisha hivyo ofisi yake inapaswa kuchunguzwa.
Mkurugenzi ashinda kesi ya kusimamia mali
Na Said Njuki Arusha
MAHAKAMA ya Mwanzo Maroboso mjini Arusha, imemthibitisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Wilson Kabwe kuwa msimamizi halali wa mali ya marehemu ndugu yake aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini Bw. John Mkenga.
Bw. Mkenga alifariki Machi mwaka huu, kwa ajali ya gari ambapo licha ya familia kufanya kikao na kumteua Bw. Kabwe kuwa msimamizi wa marathi, mke wa marehemu Bi. Blandinja Mkenga aliibuka na kupinga uteuzi huo na kufungua kesi mahakamani.
Walalamikia bidhaa kupanda bei kinyemela
Na Salim Nyomolelo
SIKU chache baada ya Serikali kusoma bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13 bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, wameanza kupandisha bei ya bidhaa mbalimbali.
Wakilalamikia hali hiyo, baadhi ya wakazi wa jiji hilo walisema kitendo kinachofanywa na wafanyabiashara hao ni kinyume na utaratibu ili kutaka kujinufaisha.
Walemavu 90 wa macho wapewa mafunzo ya utambuzi wa katiba
Na Mwandishi Wetu
VIJANA 90 wenye ulemavu wa macho katika Wilaya za Temeke na Ilala, jijini Dar es Salaam, wamepatiwa mafunzo yanayohusu utambuzi wa katiba ya sasa ili kubaini kasoro zilizopo na kutumia fursa hiyo kutoa maoni yao katika mchakato wa Katiba Mpya.
21 June 2012
Katiba mpya iwe na dira ya maendeleo
Na Halfan Diyu
KATIBA muongozo ambao taifa lolote limejiwekea jinsi ya kuendesha shughuli za kila siku za taifa lao.
Taifa linakuwa imara linapokuwa na katiba imara na viongozi bora, wenye maono ya kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Taifa lazima lisimamie misingi ya haki na ianishwe katika katiba kwani ni haki pekee huleta watu pamoja na kiondoa misingi yote ya unyonyaji.
Mashujaa kufanya ziara Kanda ya Ziwa
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa 'Wana Kibega', inatarajia kufanya ziara maalumu kwa mashabiki wake wa Kanda Ziwa mwishoni mwa wiki.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter alisema onesho la kwanza litafanyika Ijumaa mjini Kahama, mkoani Shinyanga.
Waziri ataka UMMESETA iunde Twiga Stars B
Na Heri Shaaban, Pwani
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenela Mukangara amesema Mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) ya mwaka huu yatatumika kuunda timu ya pili ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).
SIKU YA MUZIKI
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa (AF), Sullivan Benetier (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi, kuhusu kituo hicho kuandaa Maadhimisho ya Siku ya Muziki Duniani inayofanyika leo, kwa kushirikisha bendi na vikundi mbalimbali vya muziki. Kulia ni Kiongozi wa Bendi ya FM Academia Nyoshi Saadat. (Picha na Charles Lucas)
Ruvuma kamili Copa Coca-Cocala
Na Mhaiki Andrew, Songea
WACHEZAJI 20 na viongozi watatu wa timu ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya mkoa wa Ruvuma, imeondoka jana mjini hapa kwenda jijini Dar es Salaam kushiriki mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2012.
Club E kufanya bonge la pati Dar
Na Mwandishi Wetu
SIGARA ya Embassy kupitia chapa yake ya Club E, inakuja na pati ya Hollywood Glam Night. Pati hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Blue Pearl ulioko Ubungo Plaza kuanzia saa 2 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam juzi na Tumaini Toroka ambaye ni Meneja wa Embassy ilieleza kwamba pati hiyo ambayo itakuwa na maudhui ya Hollywood, ambapo wanachama na wapenzi wa burudani watapata watashuhudia burudani mbalimbali na vivutio vya Hollywood.
SHABIKI BOMBA
Baadhi ya mashabiki wa soka wa klabu za Ligi Kuu ya England, waliojitokeza kwenye kushiriki mashindano ya kumsaka 'Shabiki Bomba' kwenye Castle Lager Superfans yaliyofanyika Kimara jijini Dar es Salaa jana (kulia) ni Msumi Maneno akifanyiwa usaili kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho. Mshindi wa mashindano hayo atakwenda Afrika ya kusini kushuhudia Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. (Na Mpigapicha Wetu)
Said Mwambungu kuibariki Adelahida
Na Mhaiki Andrew, Songea
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Adelahida, ambayo imechezwa na waigizaji wazawa wa mkoa huo. Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Songea Klabu, Julai Mosi mwaka huu.
Vifaa vipya Yanga vyaanza kazi
Na Zahoro Mlanzi
WACHEZAJI wapya wa Yanga, Said Banahuzi na Juma Abdul 'Baba Ubaya', wameanza mazoezi na timu hiyo yanayoendelea katika Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam na kufanya timu hiyo kuzidi kuimarika.
Wachezaji hao wamesajiliwa msimu huu wakitokea Mtibwa Sugar ambapo wameungana na nyota mwingine, Nizar Khalfan katika kuhakikisha wanaimarisha timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Bara.
20 June 2012
QML yaingia ubia na BEML Ltd ya India
Na Godfrey Ismaely
KAMPUNI ya Quality Motors Limited (QML) ambayo ni miongoni mwa kampuni zinazomilikiwa na Kampuni ya Quality Group nchini imeingia makubaliano ya usambazaji wa bidhaa mbalimbali na Kampuni ya BEML Limited kutoka nchini India.
Vodacom yazindua vifurushi vipya vya intaneti
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Mawasilino ya Vodacom Tanzania, imezindua vifurushi vipya vya intaneti ambavyo vitawawezesha wateja wake kupata huduma ya intaneti kwa shilingi 250 kwa siku.
Huduma hiyo ya 'Wajanja Intanet' imeboreshwa zaidi ili kuwawezesha wateja kuelewa huduma za intaneti na kuchagua kikamilifu huduma zitakazowafaa hivyo kuweza kuperuzi na kupata taarifa kwa kasi na kwa bei nafuu kupitia mtandao wa Vodacom.
SHIMMUTA kujadili taarifa za maendeleo
Heri Shaaban na Radhia Adam
SHIRIKISHO la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Tanzanuia (SHIMMUTA), limeandaa Mkutano wa Halmashauri kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya Shirikisho hilo kwa kipindi cha mwaka 2012 na 2013.
Mwinjilisti Kabula kugawa DVD za Nitang’ara Tu
Na Mwandishi Wetu
MWNJILISTI Kabula George, anatarajia kugawa DVD za albamu ya Nitang’ara Tu kwa kila mtu atakayeingia kwenye Ukumbi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Julai 8, mwaka huu wakati wa uzinduzi wake.
SUPER FAN
Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimbo (kulia) akicheza mfano wa mpira wa miguu kwenye uzinduzi wa kampeni ya kumtafuta Shabiki Bora wa Castle kwenye kampeni ya Castle Super Fan, ambapo mshindi atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika timu ya Afrika ya Ushangiliaji (Africa United Super Fan) Afrika ya Kusini. Na Mpigapicha Wetu
Dawa bandia ni tatizo la dunia nzima'
Na Heri Shaaban
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema kuwa suala la dawa bandia ni tatizo la Dunia nzima hivyo amewataka wananchi kushirikiana na serikali kiziba mianya ya uingizaji dawa bandia ili kulinda maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Waliompiga Manji kuwasilisha vielelezo leo
Na Zahoro Mlanzi
WAKATI mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga ukiendelea, wanachama walioweka pingamizi kwa baadhi ya wagombea wanaowania uongozi wa klabu hiyo akiwemo aliyekuwa Mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji wametakiwa kuwasilisha vielelezo vya pingamizi walizoweka kwa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo.
MSANII JUMA NATURE
Msanii wa kundi la Wanaume Halisi, Juma nature akifanya vitu vyake wakati wa tamasha maalumu la kuitambulisha airtel supa5 mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha.
Asamoah apewa 'last chance' Kagame Cup *Nizar aanza kazi, Kiiza naye ndani
Na Zahoro Mlanzi
WAKATI mshambuliaji kutoka Zambia, Davies Mwape akioneshwa mlango wa kutokea timu ya Yanga, imempa nafasi ya mwisho Mghana Kenneth Asamoah kuonesha makali yake katika michuano ya Kombe la Kagame la sivyo naye watamuacha.
Tamasha la Supa5 sasa kufanyika Mwanza
Na Mwandishi Wetu
MATAMASHA ya kuitambulisha huduma Airtel Supa5 utaendelea tena mwishoni mwa wiki ambapo safari hii itakuwa ni zamu ya jiji la Mwanza ambalo wakazi wake watapata burudani katika viwanja vya wazi vya Furahisha.
19 June 2012
Simba yamfungashia virago Machaku
Na Zahoro Mlanzi
KLABU ya Simba, imetangaza rasmi kusitisha mkataba wa kiungo wake, Salum Machaku kwa ajili ya maslahi ya klabu na ya mchezaji mwenyewe.
Mbali na hilo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic anatarajia kutua nchini Ijumaa akitokea mapumzikoni nyumbani kwao Serbia, huku wachezaji wa kigeni 'Maproo' nao wanatarajia kuanza kuwasili siku hiyo.
Wazee Yanga wawajia juu wakorofi *Mwape apewa mkono wa kwakheri
Na Elizabeth Mayemba
WAZEE wa Kamati ya Muafaka ya Yanga wamewajia juu baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambao walikwenda kumtolea lugha chafu Seif Ahmed 'Magari', ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa timu yao baada ya kufanikisha zoezi zima la usajili yeye pamoja na mfanyabiashara Abdallah Binkleb, ambaye amejitosa katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Yanga yaingia msituni rasmi *Berko, Asamoah wanogesha mazoezi
Na Zahoro Mlanzi
TIMU ya Yanga, imeanza rasmi mazoezi jana kwenye Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam ikiwa na wachezaji tisa wakiwemo kipa Yaw Berko na Keneth Asamoah huku kiungo wao mpya, Nizar Khalfan akiwa jukwaani akiangalia.
Poulsen: Tumeshindwa kiume *Watanzania wa Maputo waipa 5 Stars
Na Mwandishi Maalumu, Maputo
KOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema baada ya kupoteza mechi dhidi ya Msumbiji 'The Mambas', sasa atajipanga upya kwa ajili ya mashindano yajayo kwani timu yake imeonesha uwezo mkubwa katika mechi hiyo ya juzi.
MASHABIKI WA STARS MSUMBIJI
Mashabiki wa Taifa Stars wanaoishi nchi Msumbiji wakiishangilia timu yao wakati wa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika iliyochezwa juzi jijini Maputo. Stars ilifungwa kwa mikwaju ya penalti 7-6. Na Mpigapicha Wetu
Diamond kupamba Redd's Miss Dar InterNa Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Adbdul ‘Diamond’ anatarajia kupamba mashindano ya kumsaka Redd's Miss Dar Intercollege 2012, yaliyopangwa kufanyika Juni 22 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
TSA yahimiza vyama kutoa mafunzo
Na Amina Athumani
CHAMA cha Kuogelea Tanzania (TSA), kimewataka wanachama wake 13 kuandaa mafunzo ya kuogelea na uokoaji kama yaliyofanywa na Klabu ya Tanzania Marine Swiming Clab (TMSC), ili kuwasaidia Watanzania wengi kupata mbinu ya kujiokoa.
Wasanii waipongeza bajeti ya serikali
Na Zourha Malisa
SIKU chache baada ya serikali kuwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013, bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wasanii wameipongeza kwa kuweza kutambua mchango wa kazi zao kwa kuwaingiza katika mfumo rasmi utakaolinda kazi zao.
Mh. Temba aja sasa kivingine
Na Amina Athumani
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini Mh. Temba kesho anatarajia kutoka na wimbo wake wa kwanza wa taarab utakayojulikana kama 'Usisemwe kwani wewe nani'.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mtayarishaji wa wimbo huo Haji Ndanda kutoka studio ya HVP iliyopo Kigamboni, alisema wimbo huo wa taarabu ni wa kwanza kuutoa na kwamba ana imani italiteka soko la muziki huo.
Kidunda: Nina nafasi ya kufanya vyema
Na Amina Athumani
MWAKILISHI wa Tanzania katika michezo ya Olimpiki bondia wa ngumi za ridhaa Selemani Kidunda, amesema ingawa amekosa mapambano ya kimataifa bado ana nafasi ya kufanya vyema katika michezo hiyo.
Michuano ya Olimpiki inatarajia kufanyika London, Uingereza Julai 27 mwaka huu ambapo Tanzania itawakilishwa na wanamichezo sita akiwemo Kidunda na wanariadha Zakia Mrisho, Samson Ramadhan, Dickson Marwa na Faustin Musa pamoja na muogeleaji Magdalena Mushi.
EBBS yaibua vipaji kibao Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
PAZIA la mashindano ya Epiq Bongo Star Search (EBSS) kwa Mkoa wa Dodoma, limefungwa rasmi jana huku vipaji vingi vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16, ambao walionekana kuimba vyema na kuwafurahisha hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika Ukumbi wa Royal Village.
KUSAKA MASTAA
Madam Ritha akipokea mtoto kutoka mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla ya kuanza ya kuanza kuimba.
Bonanza vyuo vikuu lafana Dar
Na Victor Mkumbo
BONANZA la michezo mbalimbali la Vyuo vya Elimu ya Juu vya Dar es Salaam lililofanyika juzi lilikuwa kivutio kwa wadau waliojitokeza.
Bonanza hilo lililoshirikisha vyuo saba ambalo lake lilikuwa kuibua vipaji lilifanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.
Lisa Jensen kuwakilisha Tanzania Miss World
Na Victor Mkumbo
MNYANGE Lisa Jensen, ndiye atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Miss World 2012, yatakayofanyika Inner Mongolia nchini China mwaka huu.
Lisa aliibuka kidedea katika mashindano madogo ya Redd's Miss Tanzania, yaliyofanyika juzi katika Ukumbi wa 327 Dar es Salaam.
MSHINDI
Miss tz
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World, Lisa Jensen (wa pili kulia), akivishwa taji na Miss Tanzania Salha Israel,baada ya kutangazwa mshindi katika shindano la Redd's Miss Tanzania lililofanyika juzi, kushoto ni mshindi wa pili Hamisa Hassan na kulia ni mshindi wa tatu Pendo Laiser(Picha na Victor Mkumbo)
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss World, Lisa Jensen (wa pili kulia), akivishwa taji na Miss Tanzania Salha Israel,baada ya kutangazwa mshindi katika shindano la Redd's Miss Tanzania lililofanyika juzi, kushoto ni mshindi wa pili Hamisa Hassan na kulia ni mshindi wa tatu Pendo Laiser(Picha na Victor Mkumbo)
Semina ya kuogelea yamalizika
Na Amina Athumani
KLABU a kuogelea ya Tanzania Marine Swimming Club (TMSC), jana ilimaliza mafunzo ya kuogelea na kujiokoa kwa watu zaidi ya 50 yaliyofanyika katika fukwe za chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na TMSC na kudhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yakilenga kutoa mbinu za uokoaji, kuogelea na jinsi ya kujiweka katika hali ya kusubiri kuokolewa pindi maafa yanapotokea.
ZIFF kuandaa warsha, kongamano
Na Amina Athumani
WAANDAAJI wa tamasha la filamu la Zanzibar International Film Festrival (ZIFF), wameandaa warsha na kongamano kwa waandaaji na watayarishaji wa filamu.
Warsha hiyo itaanza Julai 9, mwaka huu na kushirikisha watayarishaji na waandaaji kutoka nchi mbalimbali, zitakazoshiriki tamasha hilo linalofanyika kila mwaka Ngome Kongwe, Zanzibar.
NIPISHE NJIA
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akiwatoka mabeki wa timu ya Msumbiji katika mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani iliyochezwa jana jijini Maputo. Stars ilifungwa kwa penalti 7-6. (Na Mpigapicha Wetu)
Stars yatolewa kwa mbinde AFCON
Na Mwandishi Wetu, Maputo
TIMU ya Taifa (Kili Taifa Stars), jana imetolewa kiume na Msumbiji 'Mambas' katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo Taifa Stars ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 7-6, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida. Katika hatua hiyo ililazimika kupigiana penalti zaidi ya tano baada ya kila timu kufunga mikwaju yote.
Uchaguzi Yanga waingia 'gundu' *Wagombea wote wawekewa pingamizi
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI wa Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15 mwaka huu umeingia 'gundu' baada ya aliyewahi kuwa Mhazini wa klabu hiyo Ahmed Falcon kuwawekea pingamizi wagombea wote.
Akizungumza Dar es Salaam jana Falcon alisema ameamua kuweka pingamizi kutokana na kwamba uchaguzi unafanyika na katiba ambayo haijasajiliwa na Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo.
15 June 2012
Taifa Stars yapaa Msumbiji *Rais Kikwete awapa baraka zake
Na Elizabeth Mayemba
TIMU ya Taifa (Taifa Stars) imeondoka nchini leo kwenda Msumbiji kwa ajili ya mechi yao ya marudiano dhidi ya nchi hiyo 'Mambas' kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Mbunge aibana serikali muswada wa ushauri
MBUNGE wa Moshi Mjini, mkaoni Kilimanjaro, Bw. Philemon Ndasambulo (CHADEMA), ameitaka Serikali kulieleza Bunge ni lini italeta muswada wa sheria ya Sera ya Taifa ya Ushauri kwenye Viwanda ili iweze kutumika na kuinufaisha nchi kiuchumi.
Bw. Ndesambulo aliuliza swali hilo bungeni mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali na majibu.
Mulugo: Serikali haiwajibiki kutafuta walimu shule binafsi
WAMILIKI wa shule binafsi zisizo za Serikali, wanawajibika kutangaza ajira za walimu kwa njia ya matangazo au nyingine wanazoona zinafaa na kuwaajiri katika shule husika.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Elizabeth Batenga (CCM).
Sakata la Uamsho Z'bar laibukia bungeni
MBUNGE wa Ole, Zanzibar Bw. Rajabu Mbaruk Mohamed (CUF), amemtaka Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kutoa tamkoa la kuunda Tume Huru ambayo itafanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu waliosababisha vurugu zilizotokea hivi karibuni visiwani Zanzibar zikihusishwa na kundi la Uamsho.
MASHINDANO,AIRTEL
Mchezaji Goodluck Mabiriki wa Ilala (kulia) akigombea mpira na mshambuliaji wa timu ya Lindi, Khalfan Malibiche wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Timu za Mbeya zatinga nusu fainali
Na Mwandishi Wetu
TIMU za soka za Mkoa wa Mbeya za wanaume na wanawake zimejihakikishia kucheza nusu fainali ya michuano ya kukuza vipaji wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza leo kwenye Uwanja wa Karume, Jijini, Dar es salaam.
Tuzo za filamu za kibongo kufanyika Julai
Na Zahoro Mlanzi
KAMPUNI ya Bantu inatarajia kuandaa tamasha la utoaji tuzo za filamu nchini (Bantu Film Awards), litakalofanyika kwa mara ya kwanza Julai jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kutambua kazi za wasanii na kuzitangaza kimataifa.
MISS KIGAMBONI
Wanyange wanaowania taji la Redd's Miss Kigamboni 2012 wakiwa katika mazoezi jana, mashindano hayo yanatarajia kufanyika leo katika Ukumbi wa Navy Beach, Kigamboni. (Picha na Victor Mkumbo)
Redd's Miss Kigamboni kulamba 500,000
Na Victor mkumbo
MSHINDI wa kwanza wa taji la urembo la Kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Redd's Miss Kigamboni City 2012', atazawadiwa sh. 500,000 katika mashindano yatakayofanyika leo katika ukumbi wa Navy Beach, Dar es Salaam.
Good Hope kutoa mafunzo ya ukocha
Na Mhaiki Andrew, Songea
SHIRIKA lisilokuwa la Kiserikali la Good Hope Sports Club la mkoani Ruvuma lina mikakati ya kutoa mafunzo ya ukocha na waamuzi kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, ikiwa na lengo la kuibua na kuendeleza michezo mkoani hapa.
Dogo Aslay kuzindua albamu mpya
Na Victor Mkumbo
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Isihaka Nassoro 'Dogo Aslay', anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza Juni 24 mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala.
14 June 2012
Bajeti 2012/13 kutabiri mengi *Wengi wahofia utekelezwaji wake *Lipumba alia na ugumu wa maisha
Na Godfrida Jola
WAKATI bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13, ikitarajia kusomwa leo mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema bajeti ya mwaka 2011/2012 ambayo ilikuwa sh. trilioni 13.5, haijatekelezwa.
POAC yamtaka Mkulu aombe radhi bungeni
Na Peter Mwenda
MBUNGE wa Mwibara, mkoani Mara, Bw. Kangi Lugola, amemtaka aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkulo, alithibitishie Bunge juu tuhuma alizozielekeza kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), na kudai imehongwa na Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC).
UGAIDI
Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Issaya Mungulu, akiwaonesha waandishi wa habari, picha ya mtuhumiwa wa ugaidi, raia wa Ujerumani, Emrah Erdogan, au kwa jina lingine Abdulrahaman Othman (24), aliyekamatwa nchini akituhumiwa kuwa mpiganaji wa kundi la Al-Qaeda aliyehusika katika matukio mbalimbali ya ugaidi, Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)
Polisi Dar wamnasa mfuasi wa Al-Qaeda
Na Salim Nyomolelo
JESHI la Polisi nchini, linamshikiria raia wa Ujerumani aliyefahamika kwa jina la Bw. Emrah Erdogan, ambaye aliyekamatwa jijini Dar es Salaam, Juni 10 mwaka huu.
Bw. Erdogan ambaye kwa jina lingine anaitwa 'Abdulrahaman Othman', inadaiwa ni mfuasi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Waandishi, wachapishaji kufaidika na kazi zao
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Muungano wa Vyama vya Wazalishaji na Wachapishaji Maarifa (KOPITAN), Bw. Abdullah Saiwaad, amesema kanuni na muongozo wa tozo kwa kazi zinazorudiwa utasaidia kuliongozea Taifa mapato.
MAZUNGUMZO
Mbunge wa Tabora Mjini Bw. Aden Rage (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Maji Dkt Binilith Mahenge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mjini Dodoma jana. (Picha na Vicent Tiganya-Maelezo)
Chanzo cha ajali za ndege chatajwa
Na Willbroad Mathias
TATIZO la ubovu wa miundombinu katika viwanja vya ndege na ukosefu wa mafunzo kwa marubani, linadaiwa kuwa chanzo kikuu cha ajali nyingi za ndege zinazotokea nchini.
Wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini, waliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wao uliolenga kujadili na kutafuta njia mbadala ya kuimarisha usalama wa safari za ndege.
Mpinga akiri 'uchakachuaji' leseni
Na Anneth Kagenda
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, amekiri kuwepo vitendo vya uchakachuaji leseni ambavyo ni moja ya sababu inayochangia ongezeko la ajali nchini.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda Mpinga alisema kuwa madereva wengi wanadanganya kuwa wamesea udereva katika vyuo mbalimbali kikiwemo VETA.
WANAHABARI
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali kutoka Mikoa ya Iringa,Mbeya na Dar es salaam ambao walishiriki katika utafiti na ukibua kero mbalimbali za wananchi wa kata ya Ijombe wakiwa pamojana Waraghbish wa Mtandao wa Jinsia TGNP hivi karibuni.
Madiwani Namtumbo ibueni miradi ya maendeleo -M/kiti
Na Kassian Nyandindi, Namtumbo
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wametakiwa kuibua miradi ya kimaendeleo ambayo itakuwa na tija kwa wananchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
