15 June 2012
Mulugo: Serikali haiwajibiki kutafuta walimu shule binafsi
WAMILIKI wa shule binafsi zisizo za Serikali, wanawajibika kutangaza ajira za walimu kwa njia ya matangazo au nyingine wanazoona zinafaa na kuwaajiri katika shule husika.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Elizabeth Batenga (CCM).
Bi. Batenga alitaka kufahamu kwanini shule na vyuo vya Serikali havina walimu wa kutosha lakini katika shule na vyuo binafsi kuna walimu wa kutosha, je, waanawapata wapi?
Akijibu swali hilo, Bw. Mulugo, alisema sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995, inafafanua wazi kuwa utoaji elimu nchini utakuwa kwa ushirikiano wa Serikali na taasisi au watu binafsi.
Alisema shule zisizo za Serikali, zinapata walimu kwa kutangaza ajira kupitia matangazo na kupata walimu kutoka vyuoni au nje ya nchi kwa kuhakikisha wanatimiza masharti ya ajira.
Aliongeza kuwa, baada ya kufungua milango ya ajira kwa nchi za Afrika Mashariki, walimu kutoka nchi jirani watapata ajira katika shule zisizo za Serikali hivyo upo uwezekano mkubwa wa shule za Serikali kupata walimu wa kutosha.
Akizungumzia suala la utoaji na ukaguaji maendeleo ya elimu kwenye shule na vyuo vya Serikali na binafsi, Bw. Mulugo alisema jambo hilo linasimamiwa na Wizara yake kupitia idara na taasisi zake ikiwemo ya ukaguzi wa shule, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi pamoaja na Tume ya Vyuo Vikuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ALIYEULIZA SWALI HILI HAFAJAFANYA UTAFITI WA KUTOSHA SHULE BINAFSI HAZILAZIMISHWI KUAJIRI WAALIMU WALIOHITIMU TANZANIA KWENYE SOKO LA AJIRA NI COMPETETION TUNASHINDANISHWA NA WAALIMU WA KENYA ,UGANDA,BURUNDI,RWANDA WAPO PIA WAALIMU WA KUJITOLEA TOKA NCHI ZA NJE KAMA HUNA KIWANGO NYAMAZA HAKUNA ANAYEAJIRI GARASHA
ReplyDelete